Kaka yangu na mkewe wananikwaza.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,781
Wameoana kwa ndoa ya Kikristo na kubahatika kupata watoto wawili, wote wa kike.
Tatizo ni kwamba mtoto mmoja yuko upande wa kiumeni na mwingine upande wa kikeni.
Pia baba na mama licha ya kuwa wana nyumba ya familia, kila mmoja ameikimbia na kwenda kupanga jirani na nyumba yao.
Na kibaya zaidi ukiwauliza habari za utengano wao wanakuwa wakali kuliko mwiba wa mbasa, sijui sisi kama ndugu tufanye nini ili kuinusuru ndoa hii.?
 
Kuna jambo kubwa zaidi ya ujuavyo au unavyowaona
Na kama ni ndoa washaiona nyumba yao chungu ndo maana wameamua kukaa mbali kila mmoja ]
Maana wameona separation ni nzuri kuliko kuendelea kuvumilia
 
Kitanda usichokijua hujui kunguni wake ndugu yangu.....
Inabidi watafutwe watu wazima, wenye saikolojia na uzoefu wa hayo maisha wawatafute hao watu mmoja baada ya mwingine....
Wakishapata yalowasibu watafute njia ya kuwashauri........waongee nao wakiwa pamoja, wakiwakumbusha umuhumu wa ndoa yao na familia watapata suluhu......

Inaniuma mimi sana kuachana haswa nikiwaangalia wanangu lol, namwomba Mungu aepushe mbali haya mambo ya kuachana kwa wanandoa jamani
 
pole na kukwazika. life is abt choices,ukiwauliza ww unawakwazaje utashangaa kuwa huwapendezi hata kiduchu.as long as watoto wako salama, ungejali biashara zako
 
unamaanisha nini mtoto mmoja yupo upande wa kiumeni mwingine kiukeni??? unamaanisha majina waliyopewa au nini!!!
 
Mi nadhani hutakiwi kuingilia ndoa ya kaka yako hata siku moja ukizingatia we mdogo wako, unachoweza kutoa tu advice na kuendelea na maisha yako
 
unataka na sisi tuwakwaze utuweke jf jamvini eehh??
aku tatueni huko huko mpwa
 
1. Tafuta watu wazima waongee na kila mmoja wao tofauti na kisirisiri ili waweze kujua chanzo (ingawa kila mtu atajipendelea/kuvutia upande wake).
2. Wakishajua chanzo au tatizo la ndoa hiyo wawakalishe kikao cha pamoja yaani mke, mume na hao wazee wajadili nini kifanyike ili kuisuluhisha ndoa hiyo na watoto wao.
3. Hiyo itakuwa ni juhudi ya ndugu kutaka kuwaunganisha tena ila mkumbuke ya kuwa maamuzi ya mwisho yapo mikononi mwao hao wanandoa.
 
huna haja ya kukwazika.mambo mengine kama wenyewe wanaona sawa,kwani wenyewe ndio wanajuana zaidi,ni bora yawe hivyo hivyo,kuliko kuishi kwa kulazimishana kisa jamii itakwazika
 
Kama hujaoa, kaoe kisha uifanye ndoa yako imara na ya kuvutia, wataiga mfano na kurudiana. Raha ngoma uingie ucheze.
 
Wameoana kwa ndoa ya Kikristo na kubahatika kupata watoto wawili, wote wa kike.
Tatizo ni kwamba mtoto mmoja yuko upande wa kiumeni na mwingine upande wa kikeni.
Pia baba na mama licha ya kuwa wana nyumba ya familia, kila mmoja ameikimbia na kwenda kupanga jirani na nyumba yao.
Na kibaya zaidi ukiwauliza habari za utengano wao wanakuwa wakali kuliko mwiba wa mbasa, sijui sisi kama ndugu tufanye nini ili kuinusuru ndoa hii.?

Mkuu hapo hakubna cha kunusuru. Wameamua kutumia lugha ya picha kufikisha ujumbe. pengine kama ukifuatilia unaweza ambiwa hiyo nyumba washauza na kila mmoja kachapa lapa na chake. Ndoa ni noma kweli
 
Back
Top Bottom