Kaka yangu anataka kunioa

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Tumsaidieni huyu dada jamani....

Mimi ni msichana wa miaka 23, nina kaka yangu baba mmoja na mama tofauti. Yeye ananipenda na mimi nampenda na tumekwisha wahi kufanya mapenzi mara kadhaa. Yeye ameahidi kuwa atanioa. Sisi ni Waislamu, je ni sawa tunachokifanya kama sio sawa tufanyeje?"
 
Mhh nendeni kawaelezeni wazazi wenu nia na madhumuni yenu, majibu wakatayo wapa ni motisha tosha kabisaa!
 
Ndoa gani yawezekana kati ya kaka na dada? Haikubaliki kwa sababu za kiafya na kimaadili. Ninyi ni maharimu hamuwezi kufunga ndoa licha ya kwamba mlishafanya ngono. Yafaa kuamua kwa dhati ya kuacha tabia hiyo isiyompendeza Mungu, wazazi na jamii kwa ujumla. Tokeni nje, wamejaa wadada na wakaka; mkaoe na kuolewa nao.
 
Hiyo ni dhambi ya kutosha. Ingekuwa enzi za zamani wote mngepigwa mawe hadi kufa. Acheni TAFADHALI.
 
Ndoa gani yawezekana kati ya kaka na dada? Haikubaliki kwa sababu za kiafya na kimaadili. Ninyi ni maharimu hamuwezi kufunga ndoa licha ya kwamba mlishafanya ngono. Yafaa kuamua kwa dhati ya kuacha tabia hiyo isiyompendeza Mungu, wazazi na jamii kwa ujumla. Tokeni nje, wamejaa wadada na wakaka; mkaoe na kuolewa nao.

Ni kweli, mimi mwenyewe nilipopata kisa hiki nikashauri kuwa ndoa ya namna hii haiwezi kufungwa kwani kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania ndoa ya dizaini hii haikubaliki na pia mahusiano yeyoye ya kingono kati ya ndugu ni kosa la jinai linaitwa INCEST.,lakini huyu dada ametekwa kabisa na penzi la huyu ndugu yake na almost hasikii la mtu, labda tukiongea wengi hapa anaweza kuelewa.
 
Kwani ndoa ni nini? Maana kama weshakula tundi asa kwa nini anataka ushauri? Si angetaka ushauri kabla hajafanya hizo mara kadhaa? Ah jamani

Sijui pengine dini yake inamruhusu maana nimeshayaona ya hivi mengi tu kwa hawa ndugu zetu
 
Hili ni jambo la kutaka ushauri wakati liko wazi kabisa?? Tuache utani wakuu. Labda utuambie kuwa hawa kaka na dada ni punguani hawana ikili. Kwanza kitendo cha kufanya ngono na ndugu ndiyo ukichaa wenyewe kama siyo wendawazimu. Labda ungeniambia kuwa mmoja wao alizaliwa nje na hawakufahamiana mpaka walipokutana na kupendana. Na kama ni hivyo basi ni kosa kwa wazazi kutowatambulisha wale watoto haramu tangu wakiwa wadogo ili wafahamiane. Ukifanya siri basi siku utaletewa mjukuu wa mtoto wako. Hivi utamwita nani? Mjukuu au mtoto? Kazi kwenu wazinzi wasiokuwa na speed governor??!!
 
Ndoa ni zaidi ya kumegana kaka, wakifunga ndoa ina maana wanataka sheria iwatambue kuwa wao ni wanandoa halali.
 
That is incest! It is againist God and all religion! soma hapa

"Cursed is the man who sleeps with his sister, the daughter of his father or the daughter of his mother." Then all the people shall say, "Amen!" Deuteronomy 27:22.

It is againist all African cultures, it pervet, crooknedness. it is nasity, How can you even think of that filthy act.
 
Ni kweli, mimi mwenyewe nilipopata kisa hiki nikashauri kuwa ndoa ya namna hii haiwezi kufungwa kwani kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania ndoa ya dizaini hii haikubaliki na pia mahusiano yeyoye ya kingono kati ya ndugu ni kosa la jinai linaitwa INCEST.,lakini huyu dada ametekwa kabisa na penzi la huyu ndugu yake na almost hasikii la mtu, labda tukiongea wengi hapa anaweza kuelewa.

Washauri waende kwenye maombi. Japo hatutakiwi kuhukumu lakini naona kama hii ni dhambi na wanachokifanya hakimpendezi Mwenyezi Mungu, waambia waache mara moja
 
Hili ni jambo la kutaka ushauri wakati liko wazi kabisa?? Tuache utani wakuu. Labda utuambie kuwa hawa kaka na dada ni punguani hawana ikili. Kwanza kitendo cha kufanya ngono na ndugu ndiyo ukichaa wenyewe kama siyo wendawazimu. Labda ungeniambia kuwa mmoja wao alizaliwa nje na hawakufahamiana mpaka walipokutana na kupendana. Na kama ni hivyo basi ni kosa kwa wazazi kutowatambulisha wale watoto haramu tangu wakiwa wadogo ili wafahamiane. Ukifanya siri basi siku utaletewa mjukuu wa mtoto wako. Hivi utamwita nani? Mjukuu au mtoto? Kazi kwenu wazinzi wasiokuwa na speed governor??!!

Ni kweli lipo wazi lakini unadhani mambo haya hayapo kwenye jamii zetu?.,unadhani hawa wanaoyafanya hawajui kuwa wanachokifanya ni kosa?.,sasa tujiulize tatizo ni nini,ni mara ngapi tumesikia kaka na dada wapo kwenye mahusiano ya kingono tena wala hawaishi mbalimbali na wanafahamiana vizuri sana.,kuna kale ka mchezo ka 'binamu nyama ya hamu' kwenye baadhi ya makabila huwa wanachukulia poa tu lakini ikiachiwa hii mwisho wake ndio huu wa ndugu kuoana.
 
Kwani ndoa ni nini? Maana kama weshakula tundi asa kwa nini anataka ushauri? Si angetaka ushauri kabla hajafanya hizo mara kadhaa? Ah jamani

Sijui pengine dini yake inamruhusu maana nimeshayaona ya hivi mengi tu kwa hawa ndugu zetu

...mnh,
Mydear nawe ushaanza 'siasa kali?' :)
Dini ya Uislamu hairuhusu ndugu wa baba/mama mmoja kuoana, wala kujamiiana,...
 
kwani wakati wanamegana hawakujua kwamba wao ni ndugu?
utakuta bado wanaendelea kuvunja amri ya 6 tu!
 
Back
Top Bottom