Kaka na dada kufanya mapenzi ni ugonjwa?

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
207
Wakuu wenye utaalamu katika fani ya tiba nisaidieni hapa.

Nimeongea na rafiki yangu aliyeko Tz kaniambia kuwa last week kaachana na mkewe baada ya kumfumania akifanya ngono na KAKA yake. Ndiyo, kaka yake kabisa baba mmoja mama mmoja, yaani namaanisha kaka na dada wamefanya mapenzi, na huyo kaka ndio mdogo kwa huyo mke.

Mara nyingi mke wake alikuwa anaenda kwao kusalimia na siku zote jamaa anasema kweli alikuwa anaenda kwao, wala hakuwahi kumtilia shaka lolote. Na huyo shemeji yake alikuwa anakuja nyumbani kwao hasa wakati fulani alipokuwa high school, na ni kijana mwenye heshima tu.

Sasa jamaa karudi nyumbani jumapili mchana baada ya safari yake (ya ndege) kuahirishwa kajaribu kumpigia simu mkewe kumtaarifu anarudi ikawa haipatikani. Kafika nyumbani, hakuna mtu, akafungua mlango sebuleni, kufika chumbani lahaula! Kakuta wako kwenye session, shemeji yake jasho linamtoka!

Cha kushangaza ameniambia amegundua baadae kwamba hata shemeji yake mwingine (dada wa huyo mkewe, kwao wako wasichana wawili tu), alikosana na mchumba kutokana na tabia ya kufanya mapenzi na kaka yao mwingine, na inadaiwa bado wanaendelea ingawa huyo kaka ameshaoa. Hiyo tabia iko kwenye hiyo familia! Inashangaza sana anasema, kwani wazazi wao ni watu wa dini sana, huyo baba yao ni mzee wa kanisa na ni watu wenye uwezo kifedha na elimu nzuri.

Huyo dada mkubwa aliyeachwa na mchumba, alikuwa analala na kaka yake wakati yeye (dada) akisoma chuo kikuu, kaka yake alikuwa anamfuata bwenini analala huko, na wasichana wenzake ndio walioanza kumgundua. Sasa jamaa yangu baada ya kusikia kuhusu hii ya dada mkubwa, akahisi huenda ni ugonjwa, si bure.

Zaidi ya kashfa za kulala na kaka zao, hao mabinti wa huyo mzee ni watulivu sana kwa sura, tabia, mienendo na hata mavazi yao, kwa ujumla katika muonekano wa nje ni wacha-Mungu kama wazazi wao. Anasema hajawahi kumwona, kumhisi wala kusikia popote kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote, hadi siku hiyo alipokuta kituko hicho. Wana miaka 2 kwenye ndoa na mtoto wa mwaka 1.

Nauliza wataalamu, ati kuna ugonjwa kama huo? Na kama upo, tiba yake ni nini?
 
******Mkuu kwanza mimi sio mtaalamu wa haya mambo ila nachangia tuu mawazo yangu****

Mzee majibu yote yako kwenye hiyo story uliyo tupa. Kwanza nampa pole sana huyo rafiki yako bwana Dr. Kithuku.

Unajua chanzo cha hayo mambo ni kwa sababu ya kupenda sana dini na malezi ya kuchungwa na wazazi wao hao wacha Mungu.
1. Mwanadamu huwa anakuwa na hatua za kukua kama ilivyo kwa kiumbe yeyote. wanafika mahali wanakuwa na hamu ya kuwa na mwenza kutokana na hisia za mwili sasa kama watoto unawafungia sana na kuwachunga sana ndio maana wanajikuta wako na uhusiano wenyewe kwa wenyewe na wala sio ugonjwa hilo ni tatizo tuu la kisaikolojia. Unakuta kaka na dada walivunjana bikra kwasababu hawakuwa na access ya watu wengine.

Hii huwa inatokea sio kwa dada na kaka tuu bali pia hata kaka kwa kaka wakaingiliana kimwili au dada na dada wakasagana. Kwa hiyo kilichocangia hapo ni kwa sababu ya kuwa watoto wa get kali sana na ndio maana hawakuweza kujichanganya na wengine. Kungekuwa na House boy au house girls wangetiana tuu ila ina elekea huyu rafiki yako mkewe walibikiriana hata na kaka yake kwa hiyo bado wote wana feeling wakati mwingine hutokea hata kaka na dada wakazaa mtoto.

Inabidi kama ni kuwasaidia ni kuwapa conceling maana ni tatizo la kisaikolojia na linatokana na malezi. Wataalamu wanasema mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake so inawekana nao walikula kutokana na kuwa wamefungiwa tuu. Mfano magerezani watu wanatiana kwa sababu hamna wanawake na wanawake wanasagana hata mashuleni kwa sababu hawana access na wanaume na hiyo taibia ikishakolea huwezi acha ni kama kupiga mustarbation ukishazoea ni basi mkuu. Sasa watafute mshauri wa kisaikologi awashauri na pia ni muhimu sana kwa hao kaka na dada kuishi mbali mbali.

Pia huyo rafiki yako inabidi ampe mke wake penzi kali sana hata iibidi kunyonya chanel O anyonye inawezekana dada anapata penzi tamu zaidi kwa dada kuliko bwana wake. Kithuku unajua sisi wanaume ni waajabu sana ukichukua mlupo au demu asiye wako unamtia kwa hasira zote na kumaliza utundu wako lakini ukifika kwa mkeo unamptia kwa kubembeleza ila aone unamheshimu hapo ndio huwa tunafanya kosa la kiufundi.

http://www.youtube.com/watch?v=1d1qaKUDndU
 
Unajua chanzo cha hayo mambo ni kwa sababu ya kupenda sana dini na malezi ya kuchungwa na wazazi wao hao wacha Mungu.
1. Mwanadamu huwa anakuwa na hatua za kukua kama ilivyo kwa kiumbe yeyote. wanafika mahali wanakuwa na hamu ya kuwa na mwenza kutokana na hisia za mwili sasa kama watoto unawafungia sana na kuwachunga sana ndio maana wanajikuta wako na uhusiano wenyewe kwa wenyewe na wala sio ugonjwa hilo ni tatizo tuu la kisaikolojia. Unakuta kaka na dada walivunjana bikra kwasababu hawakuwa na access ya watu wengine.

..hii ndio ilikuwa kichwani baada ya kusoma!na kwa makisio yote sababu hii ina nafasi kubwa!

..kwa kuongezea ni tatizo la kifamilia pia!yap!baba na mama zao wanahusika!na inawezekana wanajua,japo yaliyotokea awali!

Inabidi kama ni kuwasaidia ni kuwapa conceling maana ni tatizo la kisaikolojia na linatokana na malezi. Wataalamu wanasema mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake so inawekana nao walikula kutokana na kuwa wamefungiwa tuu. Mfano magerezani watu wanatiana kwa sababu hamna wanawake na wanawake wanasagana hata mashuleni kwa sababu hawana access na wanaume na hiyo taibia ikishakolea huwezi acha ni kama kupiga mustarbation ukishazoea ni basi mkuu. Sasa watafute mshauri wa kisaikologi awashauri na pia ni muhimu sana kwa hao kaka na dada kuishi mbali mbali.

..ushauri nasaha pekee hautoshi!inabidi wakatubu dhambi zao na kula kiapo mbele ya mungu wao!ndio!wao si ni watu wa dini!itabidi waapizwe,wote!

Pia huyo rafiki yako inabidi ampe mke wake penzi kali sana hata iibidi kunyonya chanel O anyonye inawezekana dada anapata penzi tamu zaidi kwa dada kuliko bwana wake. Kithuku unajua sisi wanaume ni waajabu sana ukichukua mlupo au demu asiye wako unamtia kwa hasira zote na kumaliza utundu wako lakini ukifika kwa mkeo unamptia kwa kubembeleza ila aone unamheshimu hapo ndio huwa tunafanya kosa la kiufundi.

..kama ulivyobainisha huko juu,hawa wanatatizo la kisaikolojia,hivyo hata jamaa akifanya lipi,lazima hao wataendeleza tu!hiyo ishakuwa laana tayari!na haifutiki mpaka wakaombewe na kula kiapo hao!

..ushauri binafsi,ni kwa jamaa kuongea na wazazi wake[au watu wa makamo wenye busara wanaoifahamu hiyo familia,wenye kutunza siri]juu ya hili. pili awajulishe wazazi wa mkewe juu ya hili[achukue tahadhari anapowajulisha,wasimgeuzie kibao]na kuwataka wafanikishe kufanyika kwa hayo niliyoeleza juu!

..option nyingine,ambayo ni radical,ni kwa huyo bwana kwenda kwa wazee wake,awajulishe,na pia kuwaeleza nia ya kuachana na mkewe,ndio,amwache....asije mwingizia laana zaidi kwenye familia!huu ni uamuzi mgumu,ila,kama hayo ya juu hayatafanikiwa,atakuja kuachana nae tu,kwa costs kubwa zaidi,hasa kwa kuchanganywa maisha!

..kitu kikioza,unajaribu kuondoa sehemu iliyooza,kama kimeoza sana,unakitupa,hata kama ni kitamu!uking'ang'ana kukila utaharisha!au pata ugonjwa wa tumbo!
 
Kazi kweli kweli!! Hiyo kweli imetokana na malezi ya geti kali. Na wakati mwingine uzungu mwingiii?! Unakuta dada na kaka wanalala chumba kimoja hadi wanakuwa teens!
 
Binafsi nakubaliana na wachangiaji wenzangu hapo juu, kwa upande wa kwanza, kwamba tatizo kubwa la mahusiano haya ni la kisaikolojia zaidi, kwamba mizizi yake ni kwa wazazi ambao huenda hawakuwapa watoto wao mazoea ya kushinda na kucheza na watoto wa familia nyingine.

Upande wa pili ni wa kisayansi zaidi. Hairuhusiwi ndugu wa familia moja kuwa na mahusiano, hasa kuzaa! Hii inatokana na kwamba hawa ndugu kibiolojia huwa na nasaba (gene) zinazofanana, kwa sababu chanzo chao ni kimoja, yaani wazazi, kwa hiyo kama kutakuwa na hitilafu katika nasaba hizi (na hii hutokea mara nyingi tu) basi huenda zikawaathiri sana watoto watakaotokana na matunda ya ndugu hawa. Mfano, iwapo katika ukoo huo wana magonjwa ya akili, uzeruzeru (sina lengo la kuwabagua), anaemia ama kifafa, basi matatizo haya yatabakia katika familia husika na kuathiri sana uzao wao.

Hii ndio sababu hasa inayofanya wataalamu wa uzazi wasisitize sana watu kuoa mbali na familia zao, lengo likiwa ni kupunguza uwezekano wa kutokea matatizo tajwa, kama mmojawapo wa wanandoa anayo.

Binafsi nimesikitishwa sana na mahusiano ya ndugu hawa, hatuna uhakika kama baada ya akina dada hawa "KUUA" ndoa zao rasmi wataoana na kaka zao ama la (Mungu aepushie Mbali lana hii).
 
Asalamu alaykum.

Tobaaa Mungu ataunusuru na upotevu wa aina hiyo atuepushe na vizazi vyetu ya Rabbi.

Ni tukio la kusikitisha sana kwa sababu linatokana na mazingira ya kisaikolojia hata mimi nimeshawahi kushuhudia suala kama hilo lakini ni tofauti kidogo tu. kulikuwa na wanafunzi katika chuo kikuu kimoja ya nchini Kenya watoto hao wakapendana sana wakiwa chuoni na wlaipomaliza pia waliendelea kama mtu na mpenziwe na wakakaa pamoja na wakazaa watoto wawili na baada ya muda wakaamua kwenda kuwatembea wazazi wao kijijini hapo tena ndipo ilipotokea siri kuibuka.

vijana wale walipofika kwa wazazi kutambulishana na mtoto wa kike alikuwa amefanana sana na yule mama wakati atakuwa ni mkwewe lakini yule mama alimuuliza mtoto wa kike unaitwa nani? na mama yako anaitwa nani yule msichana akataja jina lake na la yule mama yake anayemlea hapo yule mama akaondoka akaingia ndani na kulia.

wale watoto walikaa pale kwao siku tatu lakini katika siku tatu hizo yule mama alikosa amani pale nyumbani na ndipo alipomwambia mumewe kwamba mimi siko tayari kukubali hii harusi ifanyike wakati nikiwa hai. wale watoto wakashangaa sana na yule kijana wa kiume akamwambia baba yake 'dady mathey anakusudiaaaa? hivyo hataki mimi nimerry why? yule baba akamwambai mtoto wake sujui amekusudia nini mammaaa lakini tutazunguza tu na usijali.

Baba akajaribu kumdadisi yule mama lakini yule mama kimya anatafakari tu mwisho walikwenda kanisani kuomba msaada ili mkewe aweze kusema kitu alichonacho moyoni ndipo yule mama aliitwa na kuuliza kuna nini? na walikwenda mama na baba na watoto maharusi watarajiwa wakiwa nje lakini baadae wakaitwa nao.

Basi yule mama alikaa kimya muda mrefu huku ameinamisha kichwa chini na aliponyanyua kichwa alisema 'Ngai? Hakii nimefanya makosa makubwa mimi na sijui kama nitasamehewa na na Mungu Yesu wangu nisamehe mimi? hawa watoto ni ndugu wote nimewazaa mie huyu wa kike nilimtupa tu nikampa mtu amlee sasa leo hii wamekutana na kutaka kuoana jamani nipo wapi mimi?watoto wakashangaa

Karuka mtoto wa kiume Ngai haiwezekani hilo haliwezekani kabisaaa yaani huyu ni sister wangu hapana.
basi walihangaika kwa watu wa dini kuulizia kama wanafaa kuoana lakini kila wanapokwenda wanaambiwa haiwezekani na wanakataliwa kuozeshwa kwa sababu wao ndugu lakini point yao walikuwa wakisema kuwa wao hawahusiki na dhambi ya wazazi wao kwa hivyo wataendelea kukaa pamoja hata kama hawajaoana kwa sheria za ndoa.
basi wameendelea kukaa tu mie nilipoondoka wapo pamoja lakini na sidhani kama wataweza kuachana kwa sababu wanasema watoto wawili waliowazaa wanawajibu wa kuhudumiwa na amama na baba yao na hawataki kufanya makosa kama waliyoyafanya wazazi wao wa kuwatupa watoto

Mungu ataukinge
 
Hizi kesi zipo Nyingi sana...M/Mungu azinusuru familia zetu. Kimsingi hata hizo DINI hazifuatwi ni matatzio ya Malezi..lkn wapo wengine kutokana na HALI mbaya ya MAISHA watu wana chumba kimoja, basi inakuwa issue. Dada na Kaka wanalala pamoja hadi wanakuwa wakubwa..
Mie kuna kesi nimeisikia imetokea Nje ya Tanzania lkn waloyatokea hao ni waswahili..Kaka na Dada wamezaa...bahati mbaya au nzuri MTOTO kawa BUBU...suppose angekuwa anajua kuzungumza ingekuwaje?

Wazazi tuwe makini...
 
Kwa uzoefu wa maisha nilionao nahisi hao watu walianza mambo hayo tangu walipokuwa wadogo, wakaendelea na hako kamchezo kao mpaka wamepevuka sasa, na hawajui watajinasua vipi na laana waliyomo.

Kuna visa vingi vya aina hii, vya ndugu wa damu kufanyana mambo hayo ya aibu..Kuna kisa kimoja ambacho mvulana alikuwa na tabia ya kuvaliana nguo, especially makufuli, na dada zake tangu alipokuwa mdogo..Mtu huyo akaizoea hali hiyo, akabidi sasa hata alipooa na kuwa mtu mzima, awe anawapigia simu dada zake kila anapohitaji 'huduma' hiyo, anaenda kwao anavaa makufuli yao, akifarijika anarudi anaendelea na mambo yake..

Kwa mtazamo naona tunahitaji msaada wa kimungu kujinusuru na mambo kama haya, siamini kama kuna mzazi au daktari awezaye kukabiliana na mambo kama haya..Hii ni dalili kuwa dunia inaelekea ukingoni...Tunahitaji kuvua vidani vyetu na mavazi yetu ya thamani na kumpigia magoti M/Mungu wetu kwa toba na kujitakasa..

Hayo ndio yangu machache.
 
@ Kithuku, Chuma,
Simulizi zenu zinaendana kabisa na tukio hili hapa chini.
Hili ni tukio la kweli kabisa ambalo limetokea hapa hapa Tanzania.
Soma zaidi.

Kaka mtu amjaza mimba mdogowe

*Wako shule moja kaka darasa la 7, dada la 4
*Yadaiwa wazazi wanawalaza chumba kimoja

Na Theonestina Juma, Bukoba

MWANAFUNZI wa darasa la nne katika ya shule ya msingi Rukurungo wilayani Misenyi, kata ya Budandika, anadaiwa kupachikwa mimba na kaka yake wa tumbo moja, ambaye anasoma pia darasa la saba shuleni hapo.

Habari zilizopatikana shuleni hapo zilieleza kuwa sababu ya watoto hao mtu na kaka yake kufanya mapenzi hadi kufia hatua ya kupeana mimba ni kutokana na wazazi wao kuwalaza katika chumba kimoja.

Watoto hao ambao ni wanafunzi wa kiume ana umri wa miaka 17 na msichana ana umri wa miaka 14 wote wanafunzi wa shule ya msingi Rukurungo.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa kijiji kimojawapo katika kata ya Bugandika ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa usalama wake binti huyo alibainika kuwa na ujauzito Julai 21 mwaka huu, wakati mimba ikiwa ya miezi saba tangu.

Aliendelea kusema kuwa mimba hiyo iligunduliwa na uongozi wa shule ya Rukurungo baada ya mwenendo wake kitaaluma kushuka kila siku, bila kujulikana sababu na hivyo kuwatia wasiwasi walimu wake.

Ofisa huyo alisema kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule haukuridhika na mwenendo wake kitaaluma, hivyo ulimwita mtoto huyo wa kike kwa lengo la kumuliza nini kinachomsibu katika masomo yake ya darasani.

Mwanafunzi huyo aliwaeleza walimu hao kisa chote, kwamba ana mimba na kuwa aliyempa ni kaka yake, ambaye anasoma shuleni hapo.

Naye mtoto wa kiume alipoitwa mbele ya walimu, alikiri kumpa mimba mdogo wake huyo.

Baada ya uongozi wa shule kuridhika na taarifa zilizotolewa na ndugu hao wawili, walimwita baba yao mzazi, ambaye alifika shuleni na kuelezwa matatizo ya watoto wake, lakini baba alitaka mambo hayo yasiende mbele alitaka yaishie hapo shuleni.

Hata hivyo, baada ya uongozi wa shule kubaini hilo, waliamua kutoa taarifa katika ofisi za kata na za vijiji ili hatua za haraka na za kisheria ziweze kufuatwa, hatua za kisheria zilifuatwa ambapo kijana huyo alipelekwa katika ofisi za kata na hatimaye Polisi.

Hata hivyo, kitu kinachowashangaza watu wengi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka shule hiyo ni kwamba kijana huyo anaendelea na masomo huku mdogo wake akiwa amesimamishwa masomo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi wakazi wa kijiji cha Rukurungo ambao hawakutaka majina yao yatajwe, waliliambia gazeti hili kuwa vijana waliopachikana mimba licha ya udugu wao uhusiano wao ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwafanya watu wawe na wasiwasi juu yao.

Walidai kuwa pamoja na kuwa ndugu, wazazi wao walikuwa wanawalaza chumba kimoja, kitu ambacho ni kinyume na maadili ya mtu ambaye ameishakuwa na matamanio.

Walisema kuwa hii si bahati mbaya, bali ni kama wazazi wa watoto hao walichangia tatizo hilo kwa asilimia kubwa.

Hata hivyo, juhudi za gazeti hili kumpata mzazi wa watoto hao ili kutoa maelezo zaidi ya malalamiko ya wananchi kudai kuwa alikuwa akiwalaza watoto hao chumba kimoja, ziligonga mwamba na hata hivyo gazeti hili bado linafanya jitihada ya kumpata mzazi wa watoto hao.
Chanzo cha Habari: Gazeti La Majira, 02/09/2007
 
aliyesema kuwa mbuzi na chui hawawezi kuchungwa pamoja alisema kweli. Mambo haya yanabadilika mnapoanza utani utani wa kingono. Unamuona dada yako kapendeza unatoa comment ya kisex... dada anafurahia na yeye anajibu kiutani, mwisho mguso, mwisho mtu katumbukiza, mwisho ni siri ya familia mwisho mtu "kapigwa chini kavimba juu".. na matokeo wazee tunaitwa kufanya kile kiitwacho "kivunja undugu"...
 
Mkjj.
Huenda na umasikini wa kipato wa familia nyingi unachangia sana utovu wa kimaadili kama huu. Mfano, familia nyingi zisizo na kipato kizuri hasa mijini huwalaza vijana wa rika kama hili la hao waliojazana mimba, chumba kimoja, kwa sababu hawana pesa za kukodi nyumba kubwa yenye vyumba kadhaa ili kuwe na utenganisho wa malazi kati ya vijana wa kiume na wale wa kike! Sasa kama unavyoelewa, vijana wanapofikia umri wa balehe matamanio huwa makubwa sana, na huenda wanasimuliana kile ambacho wanakihisi kimebadilika miilini mwao. Matokeo yake ndio hayo, kuonja tunda lililokatazwa!
Labda hapa kingine cha kujadili ni kwamba, tufanye nini ili kuzuia aibu kama hizi majumbani mwetu? Kwa sababu kaka kuzaa na dada mtu, mtoto atamwita huyu mwanaume nani yake? Mjomba ama baba?
Tuendelee kulumbana na kuelimishana!
 
Wakuu wenye utaalamu katika fani ya tiba nisaidieni hapa.

Nimeongea na rafiki yangu aliyeko Tz kaniambia kuwa last week kaachana na mkewe baada ya kumfumania akifanya ngono na KAKA yake. Ndiyo, kaka yake kabisa baba mmoja mama mmoja, yaani namaanisha kaka na dada wamefanya mapenzi, na huyo kaka ndio mdogo kwa huyo mke.

Mara nyingi mke wake alikuwa anaenda kwao kusalimia na siku zote jamaa anasema kweli alikuwa anaenda kwao, wala hakuwahi kumtilia shaka lolote. Na huyo shemeji yake alikuwa anakuja nyumbani kwao hasa wakati fulani alipokuwa high school, na ni kijana mwenye heshima tu.

Sasa jamaa karudi nyumbani jumapili mchana baada ya safari yake (ya ndege) kuahirishwa kajaribu kumpigia simu mkewe kumtaarifu anarudi ikawa haipatikani. Kafika nyumbani, hakuna mtu, akafungua mlango sebuleni, kufika chumbani lahaula! Kakuta wako kwenye session, shemeji yake jasho linamtoka!

Cha kushangaza ameniambia amegundua baadae kwamba hata shemeji yake mwingine (dada wa huyo mkewe, kwao wako wasichana wawili tu), alikosana na mchumba kutokana na tabia ya kufanya mapenzi na kaka yao mwingine, na inadaiwa bado wanaendelea ingawa huyo kaka ameshaoa. Hiyo tabia iko kwenye hiyo familia! Inashangaza sana anasema, kwani wazazi wao ni watu wa dini sana, huyo baba yao ni mzee wa kanisa na ni watu wenye uwezo kifedha na elimu nzuri.

Huyo dada mkubwa aliyeachwa na mchumba, alikuwa analala na kaka yake wakati yeye (dada) akisoma chuo kikuu, kaka yake alikuwa anamfuata bwenini analala huko, na wasichana wenzake ndio walioanza kumgundua. Sasa jamaa yangu baada ya kusikia kuhusu hii ya dada mkubwa, akahisi huenda ni ugonjwa, si bure.

Zaidi ya kashfa za kulala na kaka zao, hao mabinti wa huyo mzee ni watulivu sana kwa sura, tabia, mienendo na hata mavazi yao, kwa ujumla katika muonekano wa nje ni wacha-Mungu kama wazazi wao. Anasema hajawahi kumwona, kumhisi wala kusikia popote kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote, hadi siku hiyo alipokuta kituko hicho. Wana miaka 2 kwenye ndoa na mtoto wa mwaka 1.

Nauliza wataalamu, ati kuna ugonjwa kama huo? Na kama upo, tiba yake ni nini?

Huu ni upumbavu si ugonjwa wala nini,mtu wa aina hiyo anatakiwa aombewe sana
 
Hapo kumesha haribika.
Ilafu siku hizi sijui kamdudu gani kameingia!
Msitake kusingizi a haringumu ya maisha ndio chanzo mie NAKATAA....Kabisa!
Kwanini nakataa...!
Kwa wazee wenzangu ambao mmezariwa siku nyingi huko vijijini na hata hapa Dar hivi kulikua na nyumba ya vyumba sita nyuma kama sio MSONGE tu kwa wale wa vijiji?
Kwa wale tulio zaliwa hapa Mzizima hasa wa wale wa Sinza mnakumbuka kulikua na nyumba zile za bati,yaani juu bati chini bati zilikua zinaitwa SULU SUTI (FULL SUIT)homo sawa na kua ndani ya msonge yani njee kama nyumba ndani Bwalo halina vyumba wala nini baba,mama na watoto wote wakike na kiume wanalala sehemu moja na fully maadili yalikuwepo.
Sasa sikuhizi watu wanalala vyumba tofauti alafu hayo yanatokea eti mnasingizia hali ngumu wakati mnalala kwenye magodoro kila mtu na chumba chake!please embu kuweni serious na mrete hoja sio hiyo ya hari ngumu.
 
Ama ni utandawazi unachangia??? Maana utakuta baba na binti yake wako sebuleni wanaangalia picha zenye kuamsha hisia bila aibu. Hapo vipi???
 
Nilishawahi kumshuhudia mzee mmoja na mwanae wanabishana kuhusu epsode itakayofuata ya "Days of our Lives". Kipindi hicho nilikuwa natoka zangu kijijini, ninaijua TV lakini michezo kama hiyo kwangu ilikuwa anasa. Niliona kama kituko, lakini ni kweli yanatokea, na hayo ndiyo hayo anayoeleza mdau hapo juu kwamba baba na binti wanaangalia film au whatever the programme ambayo inaleta hisia za mapenzi.
 
Mnashangaa nini kuna madada wa mvuto wa kufa Mtu, kama Baba anaweza kula Mwanae wa kumkojoa Mwenyewe, inakuwa kaka kumla dadaye.
Hivi umebahatika kuzaliwa katika familia ya kaka mmoja na madada lukuki tena BOMMBA.

We Acha tu.
 
Hayo ni mambo ya kisaikolojia,na huwa zinatokea nyingi tuu,kama baba na mtoto kufanya mapenzi zipo nyingi tuu,mimi kuna mzee mmoja namjua,anamahusiano ya kimapenzi na binti zake wawili,mke wake kakimbilia Sweden,binti mmoja keshampa mimba na huyo mwingine keshahongwa gari na baba yake,sasa hapa ukitaka kuoa hiyo mahali itapokelewa kweli?
 
Jamani binti akipita barabarani na gari alilonunuliwa na baba yake mzazi utasema kahongwa?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom