Wakuu wenye utaalamu katika fani ya tiba nisaidieni hapa.
Nimeongea na rafiki yangu aliyeko Tz kaniambia kuwa last week kaachana na mkewe baada ya kumfumania akifanya ngono na KAKA yake. Ndiyo, kaka yake kabisa baba mmoja mama mmoja, yaani namaanisha kaka na dada wamefanya mapenzi, na huyo kaka ndio mdogo kwa huyo mke.
Mara nyingi mke wake alikuwa anaenda kwao kusalimia na siku zote jamaa anasema kweli alikuwa anaenda kwao, wala hakuwahi kumtilia shaka lolote. Na huyo shemeji yake alikuwa anakuja nyumbani kwao hasa wakati fulani alipokuwa high school, na ni kijana mwenye heshima tu.
Sasa jamaa karudi nyumbani jumapili mchana baada ya safari yake (ya ndege) kuahirishwa kajaribu kumpigia simu mkewe kumtaarifu anarudi ikawa haipatikani. Kafika nyumbani, hakuna mtu, akafungua mlango sebuleni, kufika chumbani lahaula! Kakuta wako kwenye session, shemeji yake jasho linamtoka!
Cha kushangaza ameniambia amegundua baadae kwamba hata shemeji yake mwingine (dada wa huyo mkewe, kwao wako wasichana wawili tu), alikosana na mchumba kutokana na tabia ya kufanya mapenzi na kaka yao mwingine, na inadaiwa bado wanaendelea ingawa huyo kaka ameshaoa. Hiyo tabia iko kwenye hiyo familia! Inashangaza sana anasema, kwani wazazi wao ni watu wa dini sana, huyo baba yao ni mzee wa kanisa na ni watu wenye uwezo kifedha na elimu nzuri.
Huyo dada mkubwa aliyeachwa na mchumba, alikuwa analala na kaka yake wakati yeye (dada) akisoma chuo kikuu, kaka yake alikuwa anamfuata bwenini analala huko, na wasichana wenzake ndio walioanza kumgundua. Sasa jamaa yangu baada ya kusikia kuhusu hii ya dada mkubwa, akahisi huenda ni ugonjwa, si bure.
Zaidi ya kashfa za kulala na kaka zao, hao mabinti wa huyo mzee ni watulivu sana kwa sura, tabia, mienendo na hata mavazi yao, kwa ujumla katika muonekano wa nje ni wacha-Mungu kama wazazi wao. Anasema hajawahi kumwona, kumhisi wala kusikia popote kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote, hadi siku hiyo alipokuta kituko hicho. Wana miaka 2 kwenye ndoa na mtoto wa mwaka 1.
Nauliza wataalamu, ati kuna ugonjwa kama huo? Na kama upo, tiba yake ni nini?