KAKA KUMUHARIBIA DADA YAKE ASIWE BILIONEA KWA ROHO MBAYA NA WIVU

BAFA

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
3,072
2,000
Wakuu hili jambo limeniskitisha sana ni kisa cha uhalisia kinatrend huko marekani (US).

Tajiri namba moja duniani Jeff bozos (mmiliki wa Amazon), Mwenye ukwasi wa USD 137 billions, alishtua dunia alipotangaza yeye na mke wake wa miaka 25 (waliojaliwa watoto watatu) wanatengana.
Hili lilishtua dunia kwa muda sababu bezos ni mtu mkubwa sana na hili watu na wachambuzi wakawaza kupungua kwa utajiri wa bezos nusu kutokana na sheria za ndoa huko.
Ghafla siku ya pili gazeti la national enquiry wao wakaja na taarifa halisi kwanini bezos anatengana na mke wake ni sababu alikuwa anacheat na dada mtangazaji Lauren Sanchez wakiwa na ushahidi wa picha na text msg.
Kwa wenzetu huko ughaibuni swala la kucheat ni fedheha kubwa nahisi hili la taarifa kuvuja alilijua mapema bwana bezos akaamua tu na mkewe wafikie kutengana kuepuka aibu kbla gazeti halijatangaza.

Sasa likaja swala la bwana bezos kuchunguza nani amevujisha taarifa hizi hali ya kuwa mahusiano hayo yalikuwa na siri kubwa mno.
Basi mchunguzi akaingia kazini na alichokikuta ni kitu cha ajabu kuwa uvujaji wa taarifa umetoka kwa Michael Sanchez kaka yake wa damu ni Lauren Sanchez na huwezi amini sababu kubwa ya kufanya hvo ni kuwa tu anamkomesha bezos kwa kuwa bezos anamchukia trump, huku bwana Michael akiwa ni mfuasi mtiifu wa trump.

Sasa wamenyea kambi bezos yuko mbali na dada yake Michael na huku Michael akilia na kukataa hilo swala lakini amepata fedheha kubwa mno.
Hakika nimegundua hawa walatini wako na roho mbaya kama waafrika dada yake alikuwa na 48 yrs ni mpambanaji (mdangaji wa Hollywood), single mom aliolewa akaachika, ndio anaoibeba familia ambayo huyo kakaake ameajiriwa na dada yake. Kapata bwana ambae huenda angekuja muoa na akawa bilionea lakini kwa roho mbaya na bila kufikria yanayokuja Michael kamchomesha sister wake.
Na huyu Michael alikuwa kama meneja wa dada yake akawa ana access na vitu vingi vya dada yake.
La kujifunza tuwe makini sana na Ndugu zetu wa damu tusjiachie kwao Kwa kila jambo.

Picha hapo chini Lauren Sanchez akawa na mama yake na kaka yake Michael Sanchez siku bezos alivowaalika ofisi kwake amazon. Hakika mtu mpaka anakualika na familia yako ofsn kwake ujue alikuwa na imani na nyie na very deeply in love
9479740-6675379-image-m-21_1549482691628.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom