Kaka angu anataka kumwita mtoto wake 2PAC

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,801
Kaka yangu ni mpenzi sana wa muziki wa hip hop. Mke wake ni mjamzito, Ijumaa walienda kufanya ultra sound na wameambiwa mtoto anayekuja ni wa kiume.

Sasa kumekuwa na ubishani wa hali ya juu mpaka wamenuniana mpaka leo, kisa ni kwamba kaka anataka mwanae aitwe 2pac wakati mke wake anasema atoe jina lolote lile lakini sio hilo. Anadai kuwa hilo ni jina ni la kihuni sana.

Kaka ameshaanza kujiita ''Baba 2Pac'', kwenye social media amebadili majina anajiita ''Baba 2Pac'' ndio hapo mke wake anazidi kununa hatari.

Imepostiwa na,
Mdogo wa Baba 2pac
 
Asee skuhiz watoto wa kiume ni adim,majaa wanazaa madem tu,mwache mwana amwite jina lolote atakalo bana,furaha ya baba hyo...hahaha,ila hlo jina nuksi kwel,hahaha
 
2pac siku amepigwa risasi polisi aliwahi kumsaidia na sentensi ya mwisho aliyoitoa huyo Tupac kwa huyo polisi ni "f☆ck you"

Hapa tunaongelea jina la msanii aliyekuwa na kipaji mno lakini pia kiongozi wa genge la kihuni na uhuni wake ukaendelea mpaka saa anakufa. Azazi tuwe makini na utoaji wa majina kwani husababisha kurithishana tabia mbovu.
 
2pac utitle wake hapa duniani kuwa alikuwa msela mavi na inasadikika kuwa ndo yeye mhasisi wa kata kund u dressing style.Braza wako aache mihemko ya bangi jina kwa mtoto lina nguvu sana katika kuunda tabia yake.
 
Sioni tabu yoyote naye ndie kamzaaa na jina sio kama ni jina la kishetani.
Nyie mshaurini jina la pili labda la kilugha mfurahie.
 
Tupak amaru alikuwa mfalme wa wahindi wekundu(red indians) huko amerika ambaye alipinga utawala na uvamizi wa kikoloni uliofanywa na wahispania
 
Tupac Amaru shakurrrrr mbona jina amazing sana...hata mimi nimepata idea hapo

Tena mtoto atakua anakubalika balaa manake Tupac nae alikua mtu wa watu
Nishafanya maamuzi. Chochote ukiandika nakupa likes..... upande wowote wa arguments utakaokua I will be next to you.... safari yoyote utakayoifunga niangalie mbele yako ntakua huko. Ila niambie... kaishia wapi yule aliedai yuakuchukia saanaa
 
Nishafanya maamuzi. Chochote ukiandika nakupa likes..... upande wowote wa arguments utakaokua I will be next to you.... safari yoyote utakayoifunga niangalie mbele yako ntakua huko. Ila niambie... kaishia wapi yule aliedai yuakuchukia saanaa
Shukurani mkuu,nazisubiri hizo likes:D
Yule aliyenianzishia thread juzi kati hanipendi mixer kunichukia?

Kama ni huyo sifahamu kwa kweli
 
Kuna jamaa Kenya anaitwa eko dyda ni msanii,,,ana watoto wawili ,wa kwanza anaitwa Keep it real favour dyda na wa pili anaitwa Am Blessed dyda,,,,
 
Mwambie amuite JOSELELA Hatajutia!!
Ikishindikana hata JERRY, POLEPOLE, TOM, POMBE!!
Kila la kheri!
 
Back
Top Bottom