kaka ama dada asiye na kazi huku majuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kaka ama dada asiye na kazi huku majuu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by qwest, Sep 12, 2010.

 1. qwest

  qwest Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: May 9, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  wenzangu ninatafuta suluhisho.

  sisi tuko huku ugenini pekee yetu, mzazi peke yake nyumbani africa.

  kaka kapoteza kazi lay off. miezi minne sasa ameishi na mimi. ameishiwa heli, gari imechukuliwa. Twaishi in the South. unemployment imezidisha.

  mie nimechoka kumweka kwangu. hana senti hana cho chote. ana vyeti vyake.

  tumejaribu kumuarifu arudi africa atafuta njia nyingine. mama naye anataka mtoto mmoja arudi akae naye. kaka sioni dalili za kuondoka huku ugenini.

  nifanye vipi. mwezi ujao ninataka kumhamisha. nitamtafutia pa kukodisha. nitamlipia mwezi wa kwanza na pengine wa pili halafu nitamwacha ajipambanie. je huu ni ukorofi.

  ningependa either atafute njia ya kupambana mwenyewe mie nina shida zangu, au aone kurudi nyumbani kama suluhisho. haya maisha ya ugenini ni magumu sana hasa kama huna hela wala gamba............

  nisaidieni!!!!

  namtakia wema naona ni kama anajiwaste akikaa hapa bila nothing.
   
 2. S

  Sylver Senior Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh huo kweli mtihani.
  Ila kabla ya kurudi bongo make sure anafanya utaratimu mzuri bila pesa wala kitu cha kufanya bongo ni noma pia ukizingatia watu wanachua unakuja na hela,so kama anenda huko aanze ku apply online at least awe anachua wapi pa kuanzia na interview.

  Kuna job agents nyingi bongo siku hizi ....radarrecruitment.com,tzonline, and so on just google.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  mtu mwingine anapokuwa na uhakika wa kulala na kula hana shida ya kupata tabu au kupambana. Nimeona mimi kwangu, jamaa same type anakuwa yupo yupo na nzuri zaidi mi napiga kazi toka asubuhi narudi saa nne usiku nakuta jamaa hata menu hajaandaa anaona aibu kwenda sokoni! Duh kazi kweli kweli!

  Mwaambie kabisa aache utozi, hakuna kubweteka apige kazi yeyote ile ilimradi anapata pesa. Ajichanganye kwa kasi, aongee na watu mbali mbali, jawabu lako siyo ukorofi ila jamaa akipata matatizo we ndo wa kwanza pia kukuathiri, lakini cha msingi mwambie kama anaweza arudi home bongo atafute kazi nyingine haijakaa vizuri sana.
   
 4. qwest

  qwest Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: May 9, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sylver asante. shida hachukui serious kutafuta kazi kwingine. si state nyingine, si nchi nyingine. kwangu naona mtu akikosa mahali comfortable pa kulala, pa kuwatch tv, pa kusurf internet, pa kurelax, atajilazimisha kuSINK or SWIM. ndio sababu lazima nimhamishe. ana cheti cha masters pia, shida tu gamba. pia ni yule anapangia kazi za kiofisi kumwokoa. miye nimechoshwa na haya yote ninazo shida zangu mwenyewe.:confused2: nitaamrifu juu ya agents......... pengine atarespond.....

  RedDevil.........kweli UMENENA! ndivyo navyofikiri.
   
 5. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  naona kama mkenya weye, ila huyo bro wako ame-relax ndiyo maana hajibidiishi kusaka majob, we mpangishie mwezi mmoja au miwili then atajiju, lazima atie akili, sasa na masters yake nini kinamshindwa kwanini asirudi huku kwetu tuendeleze kilimo kwanza
   
 6. qwest

  qwest Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: May 9, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kipilipili, tutajaribu............ inaonekana kuondoka AFrica ni harusi............kurudi ni matanga kwa wengine.......... tutajaribu
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu kuna websites za relief organizations, they may help kwa yeye kutoka kama anataka kutoka states... wengi wa hawa relief org. wanapenda waliosoma huko kwenu mlipo...

  maadam hujasema ana makaratasi ya nini, si vibaya kusearch generally tu!! pamoja na hayo, you have to be string and bold.... mpe ukweli tupu
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwani mkuu mpo majuu nchi gani?
   
 9. qwest

  qwest Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: May 9, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tuko Marekani................ uchumi umekua mgumu

  nimempa mawaidha yenu halafu mwezi ujao ni atapambana mwenyewe.
   
 10. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwambie tena kwa upole kuwa arudi nyumbani kaka! . Watu wenye Master Degree wanapata kazi tu tena sana isipokuwa kama ni mtu wa kuchagua tu kazi ya aina moja tu.
  Ikionekana ni shida kabisa basi Msaidie ili arudishe (asafirishwe) kwa nguvu maana kheri lawama kuliko fedheha kwa kuwa hata nauli ya kurudia anaweza kuwa hana sasa.
   
 11. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Ungekua umemfikishia ujumbe kama ulivyoufikisha hapa Jamvini. leo angekua ashafika Bongo. Wasi wasi wangu ni kwamba ujumbe unamfikishia kimafumbo, ila yeye anajifanya haelewi.
   
 12. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Ana vyeti vyake? Arudi nyumbani, hatakosa kazi. Elimu haiozi, ni amali isiyochoka. Bora nyumbani kuliko kuishi ugenini kama mtumwa au popo ajifichaye mchana.
   
 13. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wee unasubiri nini mlipue tu.....kwani atajua,
   
 14. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Acha matani amlipue ndugu yake. Huu mpango wa kumpangishia naona huyu ndugu anajiongezea matatizo, hiyo pesa iwe nauli ya kurudi bongo. Akikataa kurudi mpatie notice ya kuhama atafute pa kwenda.
   
 15. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35

  Kumpangishia siyo jambo jema hata kidogo. Utamfanya awe shoga bila kupenda. Huyo ni wa kurudi Bongo tu. Maisha ya mbele huko hivi sasa hayafai. Cha msingi kupambana hapa. Tunamkaribisha sana kwa elimu yake anaweza hata kuwa Diwani
   
 16. A

  Audax JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  undugu kazi-na ni ngumu kufanya maamuzi ktk masuala kama haya,ila ugenini bila kazi-hapatoshi
   
 17. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Does he have papers? If so, does he have MBA, MSc or MA? In what area of specialization? Let me have the full details, and then I'll see what we can do next.
  Thanks
   
 18. qwest

  qwest Member

  #18
  Sep 27, 2010
  Joined: May 9, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  RAJ PATEL JR shida hana papers. mwenzangu anasema hawezi kuondoka bila papers. sasa anapoteza wakati bila kazi na mwishowe pengine atapata kazi not the degree studied. sitaki kumwongezea stress, lakini kusema kweli nimechoka! :confused2: hata nilimwambia bahati ya kila mtu si marekani, pengine ni kokote kwingine, lakini hawanisikii.......... pengine i am being impatient lakini nikimwona mtu in their prime akipoteza time hivi nashindwa kuelewa.

  kuna wakati alikuwa tayari halafu akaongea na watu wengine nao wote wakamtia hofu kurudi nyumbani. walimwambia heri azidi kujuta hapa siku moja mambo yatakuwa sawa. nauliza, hiyo siku ni lini. nchi hii ni rahisi sana kuketi ukitarajia na maisha yanakataa kubadilika! utaamka miaka kumi imekupita na hauna maendeleo!
   
 19. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Arudi home, au vipi ajichanganye kwenye kazo yeyote tu. Maana anaonekana anachagua eeh!!!
   
 20. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Forthrightly push the guy arudi home….si kasoma vema bana? So why anaogopa to face the music? Ana Masters's ya nini? I can advice….
   
Loading...