Kajubi mukajanga na gazeti la wakati ni huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kajubi mukajanga na gazeti la wakati ni huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chibhitoke, Jun 4, 2010.

 1. c

  chibhitoke Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika miaka ya 90's kulikuwa na gazeti moja matata, makini na jasiri likiitwa Wakati ni Huu, nakumbuka Mkajanga alikuwa nafikiri ndiye mhariri mkuu. Kwa kweli lile gazeti lilikuwa linatoa habari za uhakika na moto moto sana. Kulikuwa na safu ya Meku Madarubini ilikuwa ni kiboko ya njia ilikuwa nikisoma hadi naogopa jinsi alivyokuwa anawapa vidonge vya wakubwa.

  Baadaye gazeti hilo lilipotea na Mukajanga akapewa ulaji fulani hivi, basi ikawa ndio mwisho wa gazeti hilo.

  Hivi huyu Meku Madarubini hawezi kuandika tena kama vile? au na yeye kisha kuwa Lamwai, Tambwe, Magoba au Charles Charles?
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Meku Madarubini nadhani ndiye 'Papaa Mawani' anayeandika kwenye Mwananchi Jumapili. Lilikuwa gazeti zuri. Mimi kuna bwana mmoja nilikuwa nafurahia tu jina lake, Bantulaki Bilango, sijui ziku hizi yuko wapi kwenye fani ya uandishi!

  ...hata hivyo, nadhani Kajubi Mukajanga hakuwa 'Wakati ni Huu' bali gazeti lake mwenyewe la 'Heko', au nimechanganya somo?
   
 3. c

  chibhitoke Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba Desi,
  Duu umenikumbusha Bantulaki Bilango!!!! nahisi lilikuwa jina magirini kama vile Naandika Mashauri, Atakalo Soko n.k

  Heko lilikuwa linamilikiwa na Ben Mtobwa
   
 4. R

  Rubuyemajaliwa New Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi! mkimtaja kajubi mnanikumbusha mbali sana ndani ya riwaya zake,tafadhali kama kuna mtu ana namba yake ya simu anipatie,
   
Loading...