Kajala, Paula wahojiwa polisi wakidaiwa kusambaza picha za Harmonize

Alaa laki tano duuh

Ngoja tujichange change hizi hela za kuuza maji kwenye madumu na vyuma chakavu huku Manzese

Plus trip moja unajilipua unabeba sembe mpka China
 
Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Kajala na mwanaye Paula wamehojiwa kwa saa kadhaa polisi na kuachiwa kwa dhamana wakidaiwa kusambaza picha za utupu zinazodaiwa kuwa za msanii wa Bongofleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Aprili 20, 2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa na kuachiwa kwa wawili hao baada ya kutua nchini wakitokea Dubai.

Taarifa za kukamatwa kwao zilianza kusambaa mitandaoni jana na leo Mambosasa amethibitisha na kufafanua kuwa walikamatwa usiku wa kuamkia jana na kuhojiwa lakini waliachiwa kwa dhamana siku hiyo saa 1 usiku.

Kamanda huyo ameyataja makosa wanayotuhumiwa nayo ni kusambaza picha za utupu mitandaoni zinazodaiwa kuwa za Harmonize na msanii huyo ndiye mlalamikaji.

“Ni kweli tuliwakamata Kajala na Paula tukawahoji baada ya mlalamikaji Harmonize kuleta malalamiko kituoni lakini tayari tumeshawaachia kwa dhamana,” amesema Mambosasa.

Amesema wawili hao wataendelea kuripoti polisi mpaka hapo jalada la upelelezi wa kesi yao litakapokamilika na kufikishwa mahakamani kwa kuwa kesi za aina hiyo huchukua muda mrefu kuzifanyia uchunguzi.

Katika hatua nyingine Kamanda Mambossa amesema wasanii Rayvanny, Baba Levo na Juma Lokole nao wamelalamikiwa na Harmonize kwa kosa hilo la kusambaza picha za utupu na tayari wamehojiwa na polisi na upelelezi bado unaendelea.

Siku tano zilizopita, Harmonize kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram alisema atawafikisha mahakamani na kuwadai fidia waliochafua jina lake mitandaoni kwa kusambaza picha hizo zinazodaiwa kuwa ni zake.

Chanzo: Mwananchi



PIA SOMA:
Du jamani hizo picha ziko wapi mbona mimi sijaziona? Naomba mwenye nazo anirushie PM naona nimepitwa na hili tukio.
 
Back
Top Bottom