Kajala, Paula wahojiwa polisi wakidaiwa kusambaza picha za Harmonize

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
16,534
2,000
Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Kajala na mwanaye Paula wamehojiwa kwa saa kadhaa polisi na kuachiwa kwa dhamana wakidaiwa kusambaza picha za utupu zinazodaiwa kuwa za msanii wa Bongofleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Aprili 20, 2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa na kuachiwa kwa wawili hao baada ya kutua nchini wakitokea Dubai.

Taarifa za kukamatwa kwao zilianza kusambaa mitandaoni jana na leo Mambosasa amethibitisha na kufafanua kuwa walikamatwa usiku wa kuamkia jana na kuhojiwa lakini waliachiwa kwa dhamana siku hiyo saa 1 usiku.

Kamanda huyo ameyataja makosa wanayotuhumiwa nayo ni kusambaza picha za utupu mitandaoni zinazodaiwa kuwa za Harmonize na msanii huyo ndiye mlalamikaji.

“Ni kweli tuliwakamata Kajala na Paula tukawahoji baada ya mlalamikaji Harmonize kuleta malalamiko kituoni lakini tayari tumeshawaachia kwa dhamana,” amesema Mambosasa.

Amesema wawili hao wataendelea kuripoti polisi mpaka hapo jalada la upelelezi wa kesi yao litakapokamilika na kufikishwa mahakamani kwa kuwa kesi za aina hiyo huchukua muda mrefu kuzifanyia uchunguzi.

Katika hatua nyingine Kamanda Mambossa amesema wasanii Rayvanny, Baba Levo na Juma Lokole nao wamelalamikiwa na Harmonize kwa kosa hilo la kusambaza picha za utupu na tayari wamehojiwa na polisi na upelelezi bado unaendelea.

Siku tano zilizopita, Harmonize kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram alisema atawafikisha mahakamani na kuwadai fidia waliochafua jina lake mitandaoni kwa kusambaza picha hizo zinazodaiwa kuwa ni zake.

Chanzo: MwananchiPIA SOMA:
"...kesi za aina hiyo huchukua muda mrefu kuzifanyia uchunguzi..."

Nime maliza kunukuu.
 
glory to yhwh

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
839
1,000
Huyu unapiga nusu kuuwa mwenyewe anakaa kwenye mstari,na hii kuzaa zaa hovyo kujidanganya matunzo nitakuwa namtumia mama yake acha anilelee mtoto wangu ndo mwisho wanazusha mabalaa kama haya.

Kama huyu angezaliwa ndani ya familia akakua ndani ya familia possibility ya kuharibika kiasi hiki ingekuwa ndogo sana hawa singo moms ni hatari wanaharibu sana kizazi!
Mkuu kuwa mwangalifu watoto wa siku hizi ukiwapiga kufa ni dk 0 wa zamani unapiga hadi unamtundika kichwa chini miguu juu lakini bado liko hai tu
 
Ngwasa Omuyaya

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
2,190
2,000
Mume wake yuko jela kwa money laundering

Miaka ka 8 iliyopita Kajala aliponea chupuchupu kwenda jela , baada ya Wema kumlipia faini ya Sh Mil 13

kwa kosa la kuuza Nyumba iliyowekwa kizuizini na takukuru.

Maji uwa hayasahau baridi alishindwa kujifunza kutokana na lile tukio ,mambo anayofanya na umri wake hayaendani naye.
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
8,485
2,000
Next ni Harmonize kupoteza mvuto kabisa wa kisanii na kuanza kutafuta mchawi. Game yake hii alivyoicheza haimuongezei kitu kwenye kazi yake bali anazidisha maadui na kufuta kila nguzo ya kumpa sapoti.
Harmonize analinda ugali wake, ni balozi wa makampuni makubwa akikaa kimya reputation yake itaharibika, wewe endelea kumsubiri apoteteze mvuto
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
161,354
2,000
Ni huyu au kuna mwingine?? View attachment 1758582

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
JamiiForums413876472.jpg
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,987
2,000
Rafiki yangu mmoja bint yake alipofika form 5 shuleni wakaanza kupaka make up. Kila mtu ana make up kit na pencil kit kwenye begi la shule. Si mnajua yake mambo ya shuke form 5 mnajiona mmekua.

Wanafundishana kupaka contour na maskara. Sasa huyu shost alikua ana mdrop shule asubuhi na kum pick mchana. Siku hiyo anaenda kumpick anamkuta mdada ana lipsticj, maskara, eyeshadow. Alimwambia nenda ukanawe kabla hujaingia kwenye gari yangu.
 
Hahahaha
 
Christine1

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
14,186
2,000
Rafiki yangu mmoja bint yake alipofika form 5 shuleni wakaanza kupaka make up. Kila mtu ana make up kit na pencil kit kwenye begi la shule. Si mnajua yake mambo ya shuke form 5 mnajiona mmekua.

Wanafundishana kupaka contour na maskara. Sasa huyu shost alikua ana mdrop shule asubuhi na kum pick mchana. Siku hiyo anaenda kumpick anamkuta mdada ana lipsticj, maskara, eyeshadow. Alimwambia nenda ukanawe kabla hujaingia kwenye gari yangu.
Safi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom