Kaizer Chiefs wafungwa katika mechi ya ligi kuu PSL

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,688
45,001
Muda mchache uliopita, wapinzani wa Simba katika robo fainali ya Caf Champions League, Kaizer Chiefs wamefungwa goli 2-1 na Tshakhuma Fc inayofundishwa Dyran Kerr aliyewahi kuifundisha Simba miaka ya nyuma. Ikumbukwe Tshakhuma Fc inashika nafasi ya 14 katika ligi kuu ya Afrika Kusini (PSL).

Kaizer Chiefs maarufu kama Amakhosi, wamepoteza mchezo huo huku mchezaji wao akilambwa kadi nyekundu na kuwaacha wakishika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi kuu ya Afrika Kusini.

Nafikiri Simba Sc watakuwa wamefatilia mchezo huu kwa uzuri kabisa, na nimegundua udhaifu mkubwa katika idara ya ulinzi ya Kaizer Chiefs.

IMG_8423.jpg

IMG_8424.jpg
 
Mimi yanga... namuombea mtani njaa.. ila sioni kaizer chiefs akimtoa simba hii kwa mechi mbili home and away... sioni beki wa kumzuia miqquissone asisumbue , huku chama huku morrisson na hapo hapo sioni mshambuliaji wa kumzidi akili josh onyangoo... hao watu niliowataja ni wakubwa sana kwa kaizer chiefs..

Simba siipendi ila ina watu wawili ambao ni level ya juu sana kucheza ligi ya Tanzania . Watu hao ni luis miqquissone na josh onyango... hawa wakicheza at their best no one can stop them
 
Muda mchache uliopita, wapinzani wa Simba katika robo fainali ya Caf Champions League, Kaizer Chiefs wamefungwa goli 2-1 na Tshakhuma Fc inayofundishwa Dyran Kerr aliyewahi kuifundisha Simba miaka ya nyuma. Ikumbukwe Tshakhuma Fc inashika nafasi ya 14 katika ligi kuu ya Afrika Kusini (PSL)...
Na ligi inakaribia kuisha
 
Back
Top Bottom