Kaisho secondary-karagwe, wafanya vurugu kubwa chanzo ccm

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,941
900
Habari za uhakika zinasema wanafunzi jana usiku wa kuamkia leo wamefanya vurugu kubwa kaisho secondary wilayani karagwe huku wakivunja na kuharibu mali kubwa za shule na magari ya walimu.
vituo vitatu vya polisi ,kaisho ,kagenyi na murongo viitwa kutuliza ghasia ambazo chanzo cha awali ni wanafunzi kutooneshwa matangazo ya tv kama ilivyo kwenye ratiba.

Lakini habari za uhakika ni kwamba wafanyabiashara mjini Isingiro ambao ni wafuasi wakubwa wa ccm wanahusika kwa karibu zaidi baada ya Jimbo katoliki la Kayanga kumhamisha Headmster wa shule hiyo na kuweka uongozi mpya baada ya wazazi kulalamika kuwa wanakamuliwa hela nyingi ambazo uishia kuwanufaisha wafanyabiashara hao kupata tenda za "kifisadi". Wafanyabiashara hao hawataki aondoke wakiofia kupoteza miradi yao iwapo uongozi mpya utaingia.
Mmoja wa wafanyabiashara hao ni diwani wa kata ya Rutunguru ambaye ni amekuwa akipewa tenda za vyakula,kuni,kusafirisha wanafunzi na vifaa vya ujenzi.

Mkuu wa wilaya na uongozi wa shule wanafanya kikao sasa ukizingatia Pinda karibia atatia timu
 
Nduli JK kwann anafanya hivo jamani! lakini nia ya kumng'oa tunayo! sababu tunayo! nguvu ya umma tunayo!
 
HAbari nilizozipata kutoka radio FADECO hivi punde, ni kwamba kuna bweni limeungua.

Sikujua chanzo ni nini.:disapointed:
 
Mi nashindwa kuielewa shule hii. Miaka2 nyuma ishakuwa tishio ktk kufaulisha sasa imeshuka ghafla,zen migomo tangu mwaka jana kwa kwenda mbele! Hapa kuna hatari!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom