Kairuki: Waliosingiziwa kugushi vyeti wakate rufaa, ila wakikutwa na makosa tena ni adhabu kali

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Waziri anayehusika na utumishi wa umma amesema watu wengi wamepiga simu wakisema kuwa wamewekwa kimakosa kuwa wameghushi vyeti ila wakibanwa vizuri wanakuja kukiri kuwa wameghushi vyeti mahali flani



Ila amesema kwa wale ambao wana uhakika kuwa wameonewa wanatakiwa kuandika barua kwa katibu mkuu ofisi ya rais utumishi wa umma nakala iende kwa baraza la mtihani na ipitishwe kwa muajiri na iambatanishe vyeti vilivyo kwenye jalada lake la utumishi
mwajiri akivipitisha atavipeleka NECTA na vingine katibu mkuu utumishi, ila kwa watakaotumia fursa hiyo ya rufani na wanajua kweli wameghushi vyeti na matokeo yao yakarudi vilevile basi adhabu itakuwa kali kuliko ya mwanzo

Utumishi pia wamefafanua zaidi kauli hiyo ya waziri

 
Huyu nae, adhabu kali ya nn tena? ,je ikiwa kweli wakapatikana walioonewa kwenye orodha hiyo, wakawekwa kwenye media na kuingia gharama kuprove je serikali itajipa adhabu gani? je itachapisha majina yao kwenye media kuwasafisha?.
 
Awamu hii inaongoza kwa mikwara, vitisho na matamko.
Nadhani wanafikiri tuko zama za kikoloni

Nae atuambie ikigundulika kwa huyo mlalamikaji baada ya huo uhakiki mpya kufanywa na kukutwa hana hatia, ni adhabu ipi au hatua ipi itachukuliwa kumsafisha maana ameshadhalilishwa kwa kutangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa ni muhalifu?

Mambo mengine yanaitaji busara kwani kwa watu zaidi ya 9900 lazima makosa yatakuwepo
Sio kila jambo linahitaji mikwara na vitisho
Kasome defamation kuhusu actions or utterances pursuant to public interests! Hutokuja kuzungumza humu tena kuhusu kuzalilishwa.
 
Je ni afisa gani wa NECTA atakayekuwa tayari kutoa taarifa tofauti na ile ya mwanzo hata kama kweli wamegundua wamemjumuisha kimakosa mtumishi. Hii itamanisha hawakuwa makini katika uhakiki na hivyo kibao kugeuka na wao kutumbuliwa. Hivyo kwa wale mlioonewa msitegemee matokeo tofauti na taarifà iliyokwishatolewa. JJIULIZE WANAOAPEAL MI TITANIUM KUNA ANAYEFANIKIWA KUPATA ALAMA TOFAUTI N'A ALIZOPATA MWANZO? Mbaya zaidi unapopeleka malalamiko kuhusu cheti walichokwambia kuwa kina utata hawakai na wewe muhusika ili wakuulize kuhusu utata huo. Mungu wape waHanga mioyo migumu la sivyo kwenye kundi la watu 9932 tutarajie vifo, magonjwa ya mayo, uwendawazimu, ndoa kukualika, kuna uwezekano mkubwa pia madhara hayo kuwakumba watoto,wazazi na wategemezi wa wahangà wa suala hili E MUNGU FANYA MIUJIZA ILI HAYO YASITENDEKE. AMINA.
 
So sad mkuu hivi hakunaga utaratibu wa kurenew vyeti baraza la mitihani as longer as taarifa zako zipo
 
Kwa kila aliyemo kwenye orodha jina lake likiandikwa katika Google linatokea kuwa ameghushi cheti.
 
Hivi hukumu hii itakuwa ya haki wakati waathirika hawajapewa haki ya kusiklizwa kuhusu yaliyomo kwenye rufaa zao. Ingefaa wakapewa nafasi ya kujieleza kwasababu wapo tayari kwa lolote ili kutetea haki zao.
 
Back
Top Bottom