Kainerugaba Msemakweli na ziara za JK

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Leo nimepata bahati ya kusoma kile kitabu cha Orodha ya Mafisadi wa Elimu Toleo la kwanza kilichoandikwa na Bw. Kainerugaba Msemakweli.,humo amewaandika waheshimiwa wote ambao wanatuhumiwa kuwa wameghushi sifa zao za taaluma tena kwa kinaga ubaga.,paliponichekesha sana ni katika pg. ya 19 na 20 alipokuwa akimzungumzia Dr. Mary Nagu, I quote....

"......anafanya yote haya akiwa anajua kuwa boss wake Rais Kikwete ni Laiser Affair President, anajua kuwa rais wetu hana muda wa kushughulikia mafisadi wa ndani kwa sababu muda mwingi yupo safarini Ulaya na Amerika.
Rais Kikwete amesafiri dunia hii kuliko Vasco Da Gama wa Ureno aliyegundua Cape Town ya Afrika ya Kusini, Mombasa na India. Kwa safari amempiku Christopher Columbus aliyegundua Amerika...."


Kwa kweli paragraph hii imenifurahisha sana,lakini pamoja na hilo ikanifanya nifikirie upya safari za Mheshimiwa.,inawezekana kweli anazunguka sana dunia na kusahau matatizo ya ndani?.,yeyote anaweza kunisaidia kunijuza ni kitu gani 'tangible' ambacho sisi kama wananchi tumeishanufaika nacho kutokana na hizi trips......?
 
ASILANI HUWEZI KUJENGA TAIFA LAKO KWA KUOMBA OMBA, WAJENGE MISINGI imara kwa resources zilizoko kisha waone tunafika wapi, eti Rais anaenda kuganga njaa, wakati DHAHABU , ALMAS, TANZANITE , zinaibwa na wezi wakizungu kutoka Canada, SA, USA..
kama tungetumia vizuri na kwa uadilifu raslimali zetu kweli tungekua mbali sana.
 
Hongera sana Kainerugaba nimecheka mpaka basi.......kwamba mzee JK amempiku hata columbus aliyegundua amerika.
 
Ameongeza kwa kusema kwa kipindi cha miaka michache tu tu Rais amesafiri mra 22 nje ya nchi wakati Kagame amesafiri mara 5 na Museveni mara 6 tu.
 
Huyu jamaa ana address mzizi wa fitina (kuwa n bodi inayotambua na kutotambua vyuo na ku enforce tambuzi hizi) au analeta vichekesho ambavyo tushavizoea?

Tusije kuwa tunachekelea jambo la hatari.
 
Kwani maudhui ya kijitabu hicho ni safari za mkuu au ufisadi wa elimu???

Maudhui sio safari, ila huenda msemakweli anaona kuwa watendaji wake wanatumia nafasi ya rais kutokuwa na muda wakutosha awapo nchini kuweza kushughulikia kero za wananchi na hapohapo kupekua undani wa watendaji wake. Si unajua wakati mwingine inabidi pia ufahamu nini kilimfanya rais kwenda kukagua daraja la kwenda msumbiji akiwa na taarifa kuwa limekamilika matokeo yake akishia kucheki jinsi mitumbwi inavyojikata?
 
Back
Top Bottom