Kaimu Mkuu wa mkoa Dar kawakosea nini waandishi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaimu Mkuu wa mkoa Dar kawakosea nini waandishi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Feb 25, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Asubuhi nilisikiliza sehemu ya kipindi cha baragumu cha channel 10. Alikuwepo kaimu mkuu wa mkoa wa Dar, bw, Said Mecky Sadiq na waandishi wa habari wawili, pamoja na mwandishi aliyekuwa anaendesha kipindi. Sehemu nilipokikuta kipindi, ilikuwa watazamaji wanapiga simu, na simu nyingi zilikuwa zinamlaumu mkuu huyo wa mkoa kwa kauli yake. Pia katika kuhitimisha mtangazaji (Salum Mwalimu), alimuuliza Bw. Sadiq, Je kutokana na maoni ya wapiga simu na waandishi waliopo studio, anakubali kuwa aliteleza kwenye kauli yake, na kuwa anai-withdraw?

  Mkuu wa mkoa aligoma kuwithdraw kauli yake pamoja na kubanwa sana na waandishi waliokuwa wanamwambia kuwa kauli yake iliwaudhi.

  Sasa mimi sikuweza kusikiliza kipindi tokea mwanzo ili nijue ni kauli gani aliwahi kutoa huyu jamaa. Kama kuna mtu ana details please anipe japo kwa ufupi...
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nasikia alimtusi mwandishi mmoja wakati wa tukio la Goms.......alitumia neno baya sana dhidi ya mwandishi yule

  leo alikuwa mdogo ka pilitoni
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Aliwatukana kuwa hawana lolote la maana kuwasaidia walopata shida g'mboto!
   
 4. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,967
  Trophy Points: 280
  kama nitakosea nisahihishwe kuna waandishi wa habari walikuwa kama wanamtetea muadhirika mmoja wa mabomu aliekua akidai kuwa misaada inatolewa kwa upendeleo ndipo muheshimiwa huyo akawageukia waandishi na kuwaeleza wasichonge wenyewe hawana uwezo wa kuchangia hata kilo moja.cha kushangaza pamoja na mapungufu yao haoni kweli mchango wa waandishi? hao ndio watu wa mkwere ukichunguza sana unaweza kuta alimsaidia wakati anamkimbia sayore monduli mie hadi kichwa kinauma.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  yeah,aliwaambia hvohvo,but kova ndo aliwatuliza waandish,coz walichukizwa,NDIO ULEV WA MADARAKA,yeyote asiyethamini mchango wa waandish kwenye lile tukio ana mtindio wa ubongo
   
 6. c

  carefree JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Sidhani kama ni tusi aliwaambia waandishi nao wachangie wahanga hao hilo ni tusi ? waandishi wanapoandika habari wako kazini wanalipwa kwa hilo sasa wanapoambiwa na wao hawajatoa mchango wowote kwa wahanga wanahamaki wanadai wamekashifiwa kwa kuwa wamekuwa wakiriport matukio
  ACHENI HIZOO mna wajibu wa kuchangia kama wananchi wengine
   
 7. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ha ha haaa, hapo kwenye red umenivunja mbavu. Asante mama mkubwa
   
 8. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Kuna tatizo la uelewa juu ya mchango; Nijuavyo mimi katika hali kama hii ya Goms, Inatakiwa Mchnago wa hali na Mali.. sasa inapotokea mtu hutambui mchango Hali bali kutambua mchango wa mali huo ni ukosefu wa fikra, hekima, busara na utu wema!
  Waandishi wa habari pamoja na vyombo vyao wametoa mchango wa hali ambao mwisho wa siku unafanya msukumo wa waathirika wa Goms kupata msaada wa mali.

  N
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwani kuchangia wahanga ni lazima? mi nilijua kuwa mchango unatokana na ALTRUISM ya mtu. Kimsingi kabisa wananchi au watu wengine hawana haja wala ulazima wa kuchangia maafa yoyote yale yanayotokana na uzembe kama ya Gongo la mboto. Ilitakiwa mzembe alipe fidia kwa waathirika na ilitakiwa kila mtu aliyepoteza maisha alipwe at least TZS 100,000,000 na wale waliopoteza au kufanyiwa uharibifu wowote kwenye nyumba zao at least TZS 50,000,000 on top of loss of life kama ipo. Majeruhi wote walipoteza viungo wapatiwe matibabu ya hali ya juu na wakipona serikali iwalipe Tshs 500,000 kila mwezi kwa muda wa miaka hamsini kama watakuwa hai adjustable to inflation kufidia kupoteza uwezo wa kufanya kazi. na wale waliopata misukosuko kama kuchubuka n.k kila mmoja apate TZS 1,000,000 on top of nyumba zao kama ziliharibika na wakufanya hivi ni serikali iliyokuwa na wajibu wa kuwalinda maisha yao na usalama. Kama tungefanya hivyo kwenye majanga zembe kama hili la Gongo la mboto Tahadhari zitakuwa zinachukuliwa na watawala kuepusha matumizi kama haya ya kodi za wananchi. Na yeyote atakayebainika ni chanzo cha uzembe kwa njia moja ama nyingine adhabu ni kifungo cha maisha, maana tukimnyonga ataenda pumzika na matatizo ya dunia.

  Ukiona viongozi wanalazimisha michango basi ujue wameshindwa wajibu wao na hawajui kwa nini wao ni viongozi. Waandishi wa habari wana wajibu na mchango mkubwa sana zaidi ya kutoa kilo moja ya unga na maharage yenye yaliyobunguliwa ili kupigwa picha kuwa wanatoa msaada. Mimi tokea nianze kuona picha za watoa misaada sijaona sehemu waandishi wa habari wanajipendelea kuonekana bali wanahabarisha jamii juu ya yale yanayotokea. Viongozi kama huyu mecky sidiki ndiyo wanaotufanya tuwe ombaomba kila siku kwa mawazo yao ya saidia dada! saidia kaka! saidia mama, saidia baba! saidia masikini!.
  -
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  hivi kwani amewatak radhi waandishi au amechuna tu

  anaonekana hawezi kazi huyo jamaa maana ameonyesha udhaifu mkubwa sana
   
 11. c

  carefree JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  waandishi kureport yale yaliyo/yanayotokea gongo la mboto na kwinepo ni wajibu wao wameajiriwa kwa hilo na wanawajibu wa kuhakikisha wanahabarisha :mullet:
   
Loading...