Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Rufiji aliyemdanganya Rais atupwa Lupango

Dawa ya masnitch kama nyie ni kuwa piga kipapai tu..
Mtu mzima apaki gari kwa faida gani?
 
Dawa ya masnitch kama nyie ni kuwa piga kipapai tu..
Mtu mzima apaki gari kwa faida gani?

Kweli mkuu .. haingii akilini kuwa watu wazima eti waamue gari lipaki tu bila sababu ya msingi ?

Labda atuambie kuna tatizo au sababu zingine lakini zilizoelezea hapa zinaleta maswali mengi kuliko majibu .

1. Kwanza naamini Tatizo la kusema uongo ni kosa la load ministrations Na Idara yake ya kazi inatakiwa kujilizisha na kumadhibu kinidhamu Na sio kumuweka lupango .

Nadhani wanasheria wanaweza kutusaidia hapa !
 
Taarifa yako bado haijakaa sawa..

Inawezekana gari ikawa imepaki kwa kufikisha km za service lakini kwa macho ni nzima...
Wao walifaidika nini kudanganya gari mbovu wakati nzima?
 
Stuoid, sasa unafurahia nini? We kesho yako unaijua? Akimaliza kwetu anakuja kwenu, by TAL
 
Kama kweli amewekwa rumande sio kwa kudanganya huenda ni kwa uzembe wa kuacha wananchi wakihangaika huku gari ipo

Viongozi sio vichaa waseme hakuna gari huku ni zima, huenda lilikua bovu

Umeshasema lilihitaji service ndogo, sasa kitu kizima hakiwezi kuhitaji service

Naamini angesema ukweli asingekaa mahabusu

Umesema vizuri. Gari kukosa matairi ni issue kubwa..ndiyo ubovu wenyewe huo. Kama halmashauri haina pesa za kununulia hayo matairi asemeje sasa. Jamaa mchonganishi sana.
 
Kwahio Bw.Kilimba anashtakiwa kwa kosa gani?kusema gari bovu?

Hebu tuambie kama gari lilikuwa zima kwanini walilipaki?sababu ilikuwa nini?

Kama gari imepaki na haifanyi kazi kama ulivyosema inahitaji service na kubadilisha vipuri maana yake ni mbovu hio.
 
Hajachongewa na mtu ila usidhani unaweza kumdanganya Rais halaf mfumo usifuatilie ukweli
Unapoongea maafisa walioko field kuanzia ofisini mitaani hata huko gereji wanarudisha meseji kuwa gari iko hapa haiko gereji chapchap .Raisi anacheki ishara kwa msaidizi wake aliyejifichav katikati bya mikutano anmwonyesha alama ya Siri ya No muongo huyo .
 
Umesema vizuri. Gari kukosa matairi ni issue kubwa..ndiyo ubovu wenyewe huo. Kama halmashauri haina pesa za kununulia hayo matairi asemeje sasa. Jamaa mchonganishi sana.
Angesema ukweli yasingemkuta

Maana sio kweli kama alivyosema mleta mada eti waliamua kulipaki halafu wakasema halipo
 
Kwahio Bw.Kilimba anashtakiwa kwa kosa gani?kusema gari bovu?

Hebu tuambie kama gari lilikuwa zima kwanini walilipaki?sababu ilikuwa nini?

Kama gari imepaki na haifanyi kazi kama ulivyosema inahitaji service na kubadilisha vipuri maana yake ni mbovu hio.
Mtoa mada anasema Bw.Kilimba alisema hawana gari
 
Napenda kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kugundua kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Bw. Brighton Kilimba alitoa taarifa za uongo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli kuwa gari ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Ikwiriri haiwezi kutembea kwa sababu ni mbovu na inahitaji matengenezo makubwa.

Nikiwa mtumishi wa Wilaya hii niliumia sana kwa sababu nilikuwa najua ni uongo wa mchana kweupe na niliumia zaidi kwa kuwa aliyekuwa anadanganywa ni Rais wangu ninayempenda Dk. John Pombe Magufuli.

Hata hivyo nilifurahi muda mfupi baadaye nilipomuona kwenye mitandao ya kijamii Bw. Brighton Eliud Kilimba, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji akiwa kwenye pingu na bango linaonesha anatuhumiwa kumdanganya Rais. Nikasema kweli vyombo vya ulinzi na usalama sasa hivi vipo makini na havijalala.

Ukweli ni kwamba gari ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Ikwiriri ipo na viongozi waliamua tu kuipaki wakati wananchi wanahangaika kupeleka wagonjwa wao Jijini Dar es Salaam pale wanapohitaji matibabu ya rufaa.

Gari hilo ni zuri, ni aina ya Toyota Landcruizer namba STL 940, ni gari imara na limekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi kabla viongozi hawajaamua kulipaki na kuwaacha Wananchi wanahangaika kukodi magari kwa gharama kubwa na wakati mwingine kupanda bodaboda, ni jambo la kusikitisha sana kwa viongozi kutotekeleza wajibu wao kiasi hiki.

Kumbe siku ile Mheshimiwa Rais alipopita Rufiji na kulalamikiwa na wananchi juu ya ukosefu wa gari la wagonjwa, gari lilikuwepo na lilikuwa limetelekezwa katika Kituo cha Afya Ikwiriri likiwa halina tatizo lolote zaidi ya kuhitaji kufanyiwa service ya kawaida ya kubadilishwa oil na pengine kubadili matairi yake.

Kaimu Mkurugenzi Bw. Kilimba alipokuwa anamdanganya Rais kuwa gari ni bovu sana na haliwezi kutembea, Rais kwa machale akaamua kuagiza gari hilo lipelekwe TEMESA mara moja, nikajua hapa siri lazima itafichuka.

Kwa kuwa gari halikuwa gereji kama Bw. Kilimba alivyosema hadharani, alichofanya Bw. Kilimba ni kupiga simu na kuagiza gari hilo lipelekwe gereji mara moja ili maafisa watakapofuatilia wakute lipo gereji, jamaa wa gereji waliposikia hivyo machale yakawacheza wakakataa kulipokea na ndipo maafisa wakagundua kuwa gari halikuwa gereji ambako Rais aliambiwa na halikuwa bovu kama Rais alivyoambiwa. Ni michezo tu ya viongozi.

Navipongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa kugundua mchezo huu, na kisha kumkamata na kumweka ndani Bw. Kilimba ambaye ni Afisa Kilimo wa Wilaya.

Aidha, nampongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua siku ileile hata kabla hajafika Dar es Salaam kwa kumtumbua Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Bw. Juma Njwayo ambaye ndio alikuwa anaongoza kutoa taarifa za uongo kuhusu ubovu wa magari. Hawa wote ni tatizo kubwa sana hapa Rufiji na yapo mengi ya hovyo wanayafanya, endapo uchunguzi wa kina utafanyika yatabainika vizuri.

Naamini hili litakuwa funzo kwa viongozi wengine kuwajibika ipasavyo katika kuwatumikiwa wananchi kama ambavyo Mheshimiwa Rais Magufuli anasema kila siku, kuwatumikia wanyonge vizuri badala ya kuwaacha wanahangaika wakati Serikali inajitahidi kuhakikisha inapeleka huduma kwa wananchi.

Msimamo wa Mheshimiwa Rais wa kuagiza gari hilo litengenezwe ndani ya wiki 1 na wakati gari linatengenezwa gari la Mkurugenzi ndilo litumike kubeba wagonjwa ni ujumbe tosha kuwa sisi watumishi ni lazima tuweke maslahi ya wananchi mbele na tuwatumikie kama ambavyo tunapaswa kufanya.

Asante Mheshimiwa Rais kwa uongozi wako makini unaojali watu hasa wanyonge.

Pichani ni Bw. Brighton Kilimba na gari la wagonjwa la Kituo cha Afya Ikwiriri.

View attachment 1524897View attachment 1524898View attachment 1524899Ni mimi Mtumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.
02 Agosti, 2020.
Una roho mbaya sana wewe
 
Mimi najiuliza, gari zima ila wameamua kulipaki, wanafaidika na nini?
Ni kawaida kwa taasisi nyingi. Baada ya muda, gari hilo angeuziwa mtu kwa bei ya kutupwa. Kuna taasisi moja ya elimu ya juu iliuza gari la wagonjwa kwa milioni 15 wakati ni zima kabisa!!
 
Hata usoni alionekana haongei ukweli, hee yule DC nae kapigwa chini?
 
ahaaaahaaa yani kuna watu watakua wanajilaumu kwanini hawakwenda kwenye gombania goli kutia nia
saizi mtu akitumbuliwa anashukuru mi naishi na hawa wateuliwa hawana raha kabisa na nafasi zao
 
Eti niliumia zaidi kwa kuwa aliyekuwa anadanganywa ni Rais wangu ninayempenda Dk. John Pombe Magufuli

Mataga bana yaani mnajipendekeza kijinga kabisa
 
Kama halmashauri ina mapato madogo watakuwa wanakwepa gharama za mafuta wananchi wakuambiwa wachangie wanaona ni rushwa na ikwiriri muhimbili parefu
 
Back
Top Bottom