Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Rufiji aliyemdanganya Rais atupwa Lupango

1596422227633.png

Ameandika mmoja wa watumishi wa afya

Napenda kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kugundua kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Bw. Brighton Kilimba alitoa taarifa za uongo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli kuwa gari ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Ikwiriri haiwezi kutembea kwa sababu ni mbovu na inahitaji matengenezo makubwa.

Nikiwa mtumishi wa Wilaya hii niliumia sana kwa sababu nilikuwa najua ni uongo wa mchana kweupe na niliumia zaidi kwa kuwa aliyekuwa anadanganywa ni Rais wangu ninayempenda Dk. John Pombe Magufuli.

Hata hivyo nilifurahi muda mfupi baadaye nilipomuona kwenye mitandao ya kijamii Bw. Brighton Eliud Kilimba, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji akiwa kwenye pingu na bango linaonesha anatuhumiwa kumdanganya Rais. Nikasema kweli vyombo vya ulinzi na usalama sasa hivi vipo makini na havijalala.

Ukweli ni kwamba gari ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Ikwiriri ipo na viongozi waliamua tu kuipaki wakati wananchi wanahangaika kupeleka wagonjwa wao Jijini Dar es Salaam pale wanapohitaji matibabu ya rufaa.

Gari hilo ni zuri, ni aina ya Toyota Landcruizer namba STL 940, ni gari imara na limekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi kabla viongozi hawajaamua kulipaki na kuwaacha Wananchi wanahangaika kukodi magari kwa gharama kubwa na wakati mwingine kupanda bodaboda, ni jambo la kusikitisha sana kwa viongozi kutotekeleza wajibu wao kiasi hiki.

Kumbe siku ile Mheshimiwa Rais alipopita Rufiji na kulalamikiwa na wananchi juu ya ukosefu wa gari la wagonjwa, gari lilikuwepo na lilikuwa limetelekezwa katika Kituo cha Afya Ikwiriri likiwa halina tatizo lolote zaidi ya kuhitaji kufanyiwa service ya kawaida ya kubadilishwa oil na pengine kubadili matairi yake.

Kaimu Mkurugenzi Bw. Kilimba alipokuwa anamdanganya Rais kuwa gari ni bovu sana na haliwezi kutembea, Rais kwa machale akaamua kuagiza gari hilo lipelekwe TEMESA mara moja, nikajua hapa siri lazima itafichuka.

Kwa kuwa gari halikuwa gereji kama Bw. Kilimba alivyosema hadharani, alichofanya Bw. Kilimba ni kupiga simu na kuagiza gari hilo lipelekwe gereji mara moja ili maafisa watakapofuatilia wakute lipo gereji, jamaa wa gereji waliposikia hivyo machale yakawacheza wakakataa kulipokea na ndipo maafisa wakagundua kuwa gari halikuwa gereji ambako Rais aliambiwa na halikuwa bovu kama Rais alivyoambiwa. Ni michezo tu ya viongozi.

Navipongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa kugundua mchezo huu, na kisha kumkamata na kumweka ndani Bw. Kilimba ambaye ni Afisa Kilimo wa Wilaya.

Aidha, nampongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua siku ileile hata kabla hajafika Dar es Salaam kwa kumtumbua Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Bw. Juma Njwayo ambaye ndio alikuwa anaongoza kutoa taarifa za uongo kuhusu ubovu wa magari. Hawa wote ni tatizo kubwa sana hapa Rufiji na yapo mengi ya hovyo wanayafanya, endapo uchunguzi wa kina utafanyika yatabainika vizuri.

Naamini hili litakuwa funzo kwa viongozi wengine kuwajibika ipasavyo katika kuwatumikiwa wananchi kama ambavyo Mheshimiwa Rais Magufuli anasema kila siku, kuwatumikia wanyonge vizuri badala ya kuwaacha wanahangaika wakati Serikali inajitahidi kuhakikisha inapeleka huduma kwa wananchi.

Msimamo wa Mheshimiwa Rais wa kuagiza gari hilo litengenezwe ndani ya wiki 1 na wakati gari linatengenezwa gari la Mkurugenzi ndilo litumike kubeba wagonjwa ni ujumbe tosha kuwa sisi watumishi ni lazima tuweke maslahi ya wananchi mbele na tuwatumikie kama ambavyo tunapaswa kufanya.

Asante Mheshimiwa Rais kwa uongozi wako makini unaojali watu hasa wanyonge.

Pichani ni Bw. Brighton Kilimba na gari la wagonjwa la Kituo cha Afya Ikwiriri.

Ni mimi Mtumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.
02 Agosti, 2020.
 
When things went south ndio huwa kifo cha nyani miti yote huteleza

Imagine jamaa kaongopa akijua kuwa atafix uongo wake kwa kulipeleka gari garage Gereji napo wameogopa kuingizwa kwenye dhoruba ya kujitakia na wao Wamemtosa

Ukisikia kukataliwa duniani mpaka kuzimu ndio huku sasa
 
watumishi wa nchi hii walizoea kufanya ubadhirifu hapo gari iliegeshwa ili wajiuzie wenyewe na watenge bajeti ingine ya kununua gari lingine ,big up Magufuli
 
Kaimu mkurugenzi wilaya ya Rufiji bwana Brighton Kirimba aliyemdanganya Rais atupwa Lupango!
Kaimu mkurugenzi huyo alitenda kosa hilo baada wananchi kutoa malalamiko mbele ya Rais kwamba Wilaya ya Rufiji haina gari la wagonjwa!
Yeye alipotakiwa kutoa ufafanuzi huo, alidai kwamba Gari wanalo na ni bovu Sana lipo gereji kwa matengenezo!

Wasaidizi wa mkurugenzi hawakufurahishwa na Kitendo Cha uongo huo!
wakaamua kutonya gari lilipohifadhiwa (ambako si gereji)

Gari Hilo limeonekana halikuwa Bovu Bali lilihitaji kufanyiwa service tu ya kawaida (kumwangwa oil) pamoja na kubadilishiwa Matairi ili kuongeza ufanisi!
IMG_20200803_095753.jpg
IMG_20200803_095801.jpg

Je; Kaimu mkurugenzi ni mkweli au alidanganya ? Kama japan wanatuuzia magari chakavu je ili Gari liwe bovu Tanzania linatakiwa kufa nini!
 
Hakuna la maana awekwe tu, manake ata wilaya ya nachingwea, hosipitali ya Wilaya gari haijulikanj haipo. Shida sana nafikiria kuwachoma tu aisee.
 
Jamaa kasema ukweli kuwa gar ni bovu, wao wanaojipendekeza wanasema gari siyo bovu ila matair yameisha ni kumwaga oil tu na service ndogo,, sasa uongo wa kaimu uko wap hapo
 
Mkuu kwa kaufahamu kadogo tu ni hivi.

Kila baada ya Kilometa kadhaa kitaalamu gari hutakiwa kufanyiea service ambayo mainly huwa kumwaga oil, kubadili oil filter, kusafisha air cliner, kupiga gris (katika msimu wa mvua mara nyingi), kubadilisha rubber nk.

Gari kuwa mbovu inahusisha vitu spair parts, injini, Gia Box, Deef nk.

NOTE
Uchakavu wa Tairi hauwezi kuiweka gari katika orodha ya magari mabovu.
 
Gari lililo chakaa matairi haalipaswi kutembea ukizingatia hiyo ni ambulance huwa zinaendeshwa kwa spidi,

Ilo gari ni bovu mpaka matairi yawekwe mapya lasivyo mna hatarisha maisha ya dereva hata raia pia
 
Soma tena tafsiri ya ubovu wa gari na service
 
View attachment 1525530
Ameandika mmoja wa watumishi wa afya

Napenda kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kugundua kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Bw. Brighton Kilimba alitoa taarifa za uongo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli kuwa gari ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Ikwiriri haiwezi kutembea kwa sababu ni mbovu na inahitaji matengenezo makubwa.

Nikiwa mtumishi wa Wilaya hii niliumia sana kwa sababu nilikuwa najua ni uongo wa mchana kweupe na niliumia zaidi kwa kuwa aliyekuwa anadanganywa ni Rais wangu ninayempenda Dk. John Pombe Magufuli.

Hata hivyo nilifurahi muda mfupi baadaye nilipomuona kwenye mitandao ya kijamii Bw. Brighton Eliud Kilimba, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji akiwa kwenye pingu na bango linaonesha anatuhumiwa kumdanganya Rais. Nikasema kweli vyombo vya ulinzi na usalama sasa hivi vipo makini na havijalala.

Ukweli ni kwamba gari ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Ikwiriri ipo na viongozi waliamua tu kuipaki wakati wananchi wanahangaika kupeleka wagonjwa wao Jijini Dar es Salaam pale wanapohitaji matibabu ya rufaa.

Gari hilo ni zuri, ni aina ya Toyota Landcruizer namba STL 940, ni gari imara na limekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi kabla viongozi hawajaamua kulipaki na kuwaacha Wananchi wanahangaika kukodi magari kwa gharama kubwa na wakati mwingine kupanda bodaboda, ni jambo la kusikitisha sana kwa viongozi kutotekeleza wajibu wao kiasi hiki.

Kumbe siku ile Mheshimiwa Rais alipopita Rufiji na kulalamikiwa na wananchi juu ya ukosefu wa gari la wagonjwa, gari lilikuwepo na lilikuwa limetelekezwa katika Kituo cha Afya Ikwiriri likiwa halina tatizo lolote zaidi ya kuhitaji kufanyiwa service ya kawaida ya kubadilishwa oil na pengine kubadili matairi yake.

Kaimu Mkurugenzi Bw. Kilimba alipokuwa anamdanganya Rais kuwa gari ni bovu sana na haliwezi kutembea, Rais kwa machale akaamua kuagiza gari hilo lipelekwe TEMESA mara moja, nikajua hapa siri lazima itafichuka.

Kwa kuwa gari halikuwa gereji kama Bw. Kilimba alivyosema hadharani, alichofanya Bw. Kilimba ni kupiga simu na kuagiza gari hilo lipelekwe gereji mara moja ili maafisa watakapofuatilia wakute lipo gereji, jamaa wa gereji waliposikia hivyo machale yakawacheza wakakataa kulipokea na ndipo maafisa wakagundua kuwa gari halikuwa gereji ambako Rais aliambiwa na halikuwa bovu kama Rais alivyoambiwa. Ni michezo tu ya viongozi.

Navipongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa kugundua mchezo huu, na kisha kumkamata na kumweka ndani Bw. Kilimba ambaye ni Afisa Kilimo wa Wilaya.

Aidha, nampongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua siku ileile hata kabla hajafika Dar es Salaam kwa kumtumbua Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Bw. Juma Njwayo ambaye ndio alikuwa anaongoza kutoa taarifa za uongo kuhusu ubovu wa magari. Hawa wote ni tatizo kubwa sana hapa Rufiji na yapo mengi ya hovyo wanayafanya, endapo uchunguzi wa kina utafanyika yatabainika vizuri.

Naamini hili litakuwa funzo kwa viongozi wengine kuwajibika ipasavyo katika kuwatumikiwa wananchi kama ambavyo Mheshimiwa Rais Magufuli anasema kila siku, kuwatumikia wanyonge vizuri badala ya kuwaacha wanahangaika wakati Serikali inajitahidi kuhakikisha inapeleka huduma kwa wananchi.

Msimamo wa Mheshimiwa Rais wa kuagiza gari hilo litengenezwe ndani ya wiki 1 na wakati gari linatengenezwa gari la Mkurugenzi ndilo litumike kubeba wagonjwa ni ujumbe tosha kuwa sisi watumishi ni lazima tuweke maslahi ya wananchi mbele na tuwatumikie kama ambavyo tunapaswa kufanya.

Asante Mheshimiwa Rais kwa uongozi wako makini unaojali watu hasa wanyonge.

Pichani ni Bw. Brighton Kilimba na gari la wagonjwa la Kituo cha Afya Ikwiriri.

Ni mimi Mtumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.
02 Agosti, 2020.
Yaani Umeshindwa kuumia Tundu Lissu kupigwa risasi16, pia ukashindwa kuumia nyumba za serikali kupewa michepuko na ndugu za Bwana Albashiri, pia hukuumia kupotea kwa fedha tirioni 1.5 ktk katika ofisi ya huyo Albashiri, unakuja kuumia ktk mambo ya utopolo.
 
Back
Top Bottom