Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili afanya mabadiliko hospitali ya Taifa Muhimbili

HPLC

Senior Member
Jul 29, 2015
186
133
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof.Lawrence Museru ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo kuanzia leo June 23, 2016 ili kupisha uchunguzi kutokana na kushindwa kusimamia vizuri maiti wakati wa kuzitoa kwa ndugu mara mbili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa na Hospitali kwa ujumla.

Prof. Museru amemteua Dkt.Flora Lwakatare Mkuu wa idara ya Radiolojia kukaimu nafasi hiyo.Kurugenzi ya Tiba Shirikishi inasimamia idara ya mionzi na idara ya Maabara ambapo kitengo cha kuhifadhi maiti kipo chini maabara.

Vilevile Prof. Museru ametengua uteuzi wa Mkuu wa kitengo cha kuhifahi maiti Hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Innocent Mosha na kumteua Dkt Herbert Nguvumali kukaimu nafasi hiyo.
 
Kumbe kuna watu wanatamani kuteuliwa hadi kitengo cha kusimamia maiti?
 
Jamani tuombee Mungu kwa hayo yaliyo mpata na uchunguzi huo ufanyike kwa haki na busara
She is a very good Dr
Pole sana Mama yangu Dr Ogweyo Mungu akupe moyo mkuu my beloved Mother
 
Huko kwa wenzetu husubiri kutenguliwa ofisi yako ikifanya vibaya unakaa pembeni mwenyewe.
 
Back
Top Bottom