Kaimu Mkurugenzi mpya Arusha ampa adhabu Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaimu Mkurugenzi mpya Arusha ampa adhabu Lema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 21, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kaimu Mkurugenzi wa mji wa Arusha, Estomi Chang’ah jana alianza kazi rasmi kwa kasi ya aina yake, baada ya kukubali malalamiko ya Chama cha Mapinduzi (CCM) juu ya mgombea wa Chadema Jimbo la Arusha, Godbless Lema kuendesha kampeni za uchochezi na hivyo kumpa onyo kali na kumpiga faini ya Sh 100,000/-

  Maamuzi malalmiko hayo ya CCM ambayo ni sehemu ya malalmiko ambayo Mkurugenzi wa zamani Raphael Mbunda aliyehamishiwa ghafla mkoani Kigoma alishindwa kutolea maamuzi.

  Kaimu M kurugenzi mpya alitoa adhabu hiyo kufuatia kikao cha kamati ya maadili ya uchaguzi kilichofanyika jana ofisi za tume ya uchaguzi, Arusha.

  Kwa mujibu wa maamuzi hayo, kama mgombea huyo wa Chadema ataendelea tena kutoa lugha chafu atapigwa marufuku kupiga kampeni hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika Octoba 31 mwaka huu.

  Katika kikao hicho cha maadili, ambacho kilihudhuriwa na viongozi wa vyama vyote, CCM walikuwa wakimlalamikia mgombea huyo wa Chadema kutokana na kuendesha kampeni chafu dhidi ya mgombea wa CCM, Dk Batila Burian ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira.

  Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao hicho, maneno yaliyomtia hatiani Lema ni kutumia lugha za matusi.

  Chanzo: Mwananchi ya leo.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nilisoma humu JF kwamba CCM walikuwa wamemtarget kumnunua. Inavyoelekea imradi huo ulishindikana na ndo maana wakaja na strategy hii ya kumuondoa Mkurugenzi wa zamani.

  By the way, hizi kamati ya maadili za tume ya uchaguzi zinaundwa na watu gani? Siyo makada wa CCM? Maana hawa wasimamizi wa uchaguzi ni wateule wa serikali ya chama tawala -- CCM -- kwa hivyo huwezi kutegemea kada wa Chadema akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Hilo CCM wenyewe hawawezi kulipnga.

  Isitoshe hayo 'Matusi" aliyoyatoa Lema hayajawekwa bayana, kwani kwa CCM, tuhuma kwao ni matusi. Tuliona kwa Marando kule Jangwani.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu M.

  Hivi kwa nini CCM wasikate rufaa kwa NEC (makao makuu) iwapo waliona malalmiko yao yalikuwa yanapuuzwa na huyo Mkurugenzi wa zamani, badala ya kumhamisha? Hii kweli ni haki?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  makosa mengine kutoka CCM, kila unapodhani utanyamazisha nguvu ya hoja kwa vitisho adhamu na maonyo, mara nyingi unakua unachochea zaidi hali halisi

  Its unfortunate baadhi ya viongozi hawaoni kwamba zile zama za vitisho zinakaribia kuisha

  Nakumbuka zamani ulikua ukikutana na gari ya waziri unampa saiti, siku hizi humpi na hawezi kukwambia kitu kwani sheria za barabarani hazina waziri wala mkuu wilaya
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Tungeyapata hayo matusi ingesaidia sana.......hapo kwenye maamuzi kuna mgongano wa maslahi.....mkurugenzi ni serikali...mgombea wa CCM ni serikali....natamani sana katiba mpya ambayo itakuwa na independent electoral mechanisms na kuzuia office bearers kuwa wagombea at the same time
   
 6. e

  emalau JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tulishajua kwamba ameletwa kufanya uzandiki, tutakula naye sahani moja
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mafisadi bwana matusi gani
   
 8. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huyo Mkurugenzi ni wale wanaoamini kwamba CCM ina hatimiliki ya nchi hii. Ole wake CHADEMA ishike madaraka!
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Weka hadharani hayo matusi ? Ingawa mimi naona yatakuwa manenp ya kashfa na sio matusi.

  Ingekwa matusi basi moja kwa moja angefikishwa mahakamani kwa mtusi shemeji yetu.
   
 10. l

  luciano maganga New Member

  #10
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yana mwisho
   
 11. Kidege

  Kidege Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ama kweli! Hii ndiyo kasi zaidi yao! Issue hii ingepewa uzito ikawa publicized ingeweza kumpa shavu sana Jamaa wa Chadema. Sema Media ipo silent sana hasa TV
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo mratibu wa tume ya uchaguzi mkoani arusha ni huyo mkurugenzi?
  Kama ndivyo. naanza kuondoa tumaini la upinzani kushinda sehemu nyingi. Hawa mbweha wakurugezi wa manispaa, wilaya, halimashauri pamoja na wakuu wao ni MAKADA wa CCM pyua bila maji. Lema akate rufaa kwani rule of natural justice haikuzingatiwa kwenye sahuri lake. Bora ukutane na hakimu mwenye kadi ya ccm akuhukuhumu maana unaweza kukata rufaa kuliko hawa manyang'au wanaopapatikiwa na TUME YA UCHAGUZI kusimamia uchaguzi kwenye kanda hizo.
   
Loading...