Kaimu Mhariri wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali akalia ofisi bila ya mkataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaimu Mhariri wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali akalia ofisi bila ya mkataba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jameswilliam, Mar 30, 2012.

 1. j

  jameswilliam New Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya serikali, inayofahamika kama TSN, amekuwa kwenye bila ya mkataba mpaka sasa kwa takribani miaka miwili na miezi kadhaa kwani mkataba wake kwa cheo cha msingi ambacho ni Naibu Mhariri Mtendaji ulishaisha tangu mwaka 2009.

  Hata hivyo si Bodi, waziri wala Mheshimiwa raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete walioweza kulishughulikia suala lenye ufisadi wa namna yake.

  Mhariri huyo mpaka sasa bado ndio Mtendaji mkuu wa Taasisi hiyo kongwe na nyeti ya serikali ilihali hana mkataba huku akiendelea kujiidhinishia malipo ya mishahara pamoja na kuingia mikataba mbalimbali kwa niaba ya Kampuni hiyo ya Serikali.

  Katika hili kuna haja ya vyombo vinavyosimamia taasisi hiyo nyeti ya serikali kuangalia namna ya kulishughulia kwani linathibitisha udhaifu mkubwa ndani ya serikali na taasisi zake.

  Hata hivyo Mhariri huyo amekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa takribani miaka miwili sasa bila kuidhinishwa au kuteuliwa Mhariri Mtendaji wa Taasisi hiyo. Hili limepigiwa kelele na wabunge kwa muda mrefu mno lakini mheshimiwa raisi mpaka leo ameshindwa kumteua Mhariri wa chimbo hicho cha serikali.
   
 2. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,752
  Trophy Points: 280
  Wanajuana hao!
   
 3. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wenyewe wanajua kinachoendelea !! Haiwezi kuwa inafanyika kwa kusahau au kwa bahati mbaya !!
   
Loading...