Kaimu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Diwani wa Kata ya Kikatiti Mhe.Elisa Mungure anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi Usariver

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kaimu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Kikatiti Mhe.Elisa Mungure anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi Usariver kwa takribani siku ya pili sasa.

Mhe.Mungure siku ya Jumanne Disemba 4, 2018 akiwa anatekeleza majukumu yake katika ofisi ya kijiji cha Nasholi alifungiwa ndani ya ofisi hizo na watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa ccm baadae akakamatwa na Polisi na kufikishwa katika kituo cha polisi Kikatiti na kuhamishiwa Usariver.

Mhe.Mungure siku ya jana Jumatano Disemba 5, 2018 alifikishwa katika Mahakama ya Mwanzo King'ori na kusomewa mashtaka matatu (3) ambayo ni Kutishia kuua, Uvunjifu wa amani na na kutoa lugha za kuudhi. Hakimu wa Mahakama hiyo alisema dhamana ipo wazi na alitoa masharti ya dhamana ambapo walihitajika wananchi raia wawili wenye utambulisho wa mtendaji wa kata kwa sehemu wanayoishi angalau kila mmoja awe na mali isiyohamishika ya thamani ya Tshs 50 Milioni na Mtumishi mmoja wa serikali ili amdhamini Kiongozi huyo. Utaratibu wa kumdhamini ulifanyika kama masharti yalivyojieleza na alipatikana mtumishi wa Serikali ili amdhamini lakini Hakimu alihitaji barua ya dhamana itiwe saini na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru na sio Mtendaji wa Kata. Viongozi walifika katika ofisi ya Mkurugenzi ili aweze kutia saini barua ya dhamana kama walivyoelekezwa na Hakimu, Mkurugenzi aligoma kusaini barua hiyo ya utambulisho.

Tunatoa Rai Sheria zifuatwe, Mahakama imeweka wazi na tunafahamu dhamana ni Haki ya mtuhumiwa. MUDA HUU Mhe. Mungure amepelekwa mahabusu gereza la Kisongo kwa namna ya uonevu na mchezo uliopangwa kabisa wa kunyima haki ya dhamana. Maekelezo ambayo yanaitwa yametokea juu yamemfunga mikono Mkurugenzi ambaye naye amekuwa tayari kufungwa na anafurahia kufungwa mikono yake ashindwe kusaini tu barua ambayo kimsingi ni ya kumtambulisha mtumishi wa serikali ili amuwekee dhamana Mhe Mungure. Tunaendelea kushauriana Mawakili wetu wasomi wa Chama ili kuona ni hatua gani za kuchukua sambamba na jitihada za kutaka Mkurugenzi asaini barua kwa watumishi wa serikali ambao wamejitokeza wengi sana na wamekuwa tayari kumdhamini Mhe Mungure. Aidha tunamtaka Mkuu wa Wilaya (DC) ya Meru asiingilie uhuru wa mahakama na aache vitendo vyake na tabia za hila kutumia mamlaka yake vibaya (Abuse of Power) kwa sababu vitendo vyake ni mwendelezo wa kupandikiza chuki na uadui baina ya watu wa Meru ambao amewakuta wakiwa na amani na mshikamano.
 
Viongozi wote wa upinzani walioko wilaya ya Arumeru ni lazima kua makini maana Muro ameletwa kwa kazi mojo tu...
 
Back
Top Bottom