Mbali na kupokea na kukabidhi kadi kwa wanachama wapya 283 katika Mkoa wa Mjini Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Ndugu Shaka Hamdu Shaka amezindua pia madaftari maalum ya wanachama kwa ajili ya kusajili upya wanachama wa UVCCM na kuhuisha takwimu zilizopo za wanachama. Vile vile aliyafungua rasmi mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wakuu wa UVCCM kuanzia matawi, wadi, Jimbo, wilaya na mkoa.
Ndugu Shaka aliwasisitiza viongozi hao kuchapakazi kwa bidii, uadilifu, nidhamu na utii kwa kufuata kanuni, katiba na miongozo mbalimbali itokanayo na vikao vya CCM. Aliwahimiza kuhakikisha wanayatembelea makundi ya vijana waliopo nje ya UVCCM ili kuwaelimisha na kuwahamasisha juu ya madhumuni ya UVCCM, siasa na itikadi ya CCM, umuhimu wa kulinda na kudumisha mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wetu.
Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanasikiliza kero na changamoto zinazowakabili vijana wote na kuzipatia ufumbuzi. Kwa kufanya hivyo aliwaeleza kutaiongezea CCM marafiki, wakereketwa na wanachama wapya kutoka kundi hili la vijana ambalo kitakwimu ni wengi zaidi hivyo kukipa Chama Cha Mapinduzi matumaini makubwa ya ushindi katika kila chaguzi.
Ndugu Shaka aliwataka viongozi hao wawe mstari wa mbele kufuatilia utekelezaji wa ilani katika maeneo yao pamoja na kusemea utekelezaji wake kwa wananchi Alieleza kuwa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli na Dkt Ali Mohamed Shein wanafanya kazi nzuri sana ya kutuletea maendeleo ni jukumu letu kuwatetea, kuwasemea na kuwalinda dhidi ya wapingaji wa kila jambo.