Kaimu Katibu Mkuu TFF, Kidau acha Uongo. Nitaweka ushahidi wa sauti

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Jana 16/11/2017 Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Wilfred. Kidau alifanya mkutano na waandishi wa habari kukanusha Madudu niliyoyaibua juzi 15/11/2017 ya Kamati ya Utendaji ya TF (EXCOM) kupitisha maazimio ya malipo ya posho yenye thamani ya tsh. Mil. 438 kwa mwaka.

Rejea hapa: TFF wakanusha taarifa za kujillipa mamilioni. Majina ya watu 10 waliosambaza habari hizo kupelekwa Polisi

Leo sitakuwa na.mengi ila tu napenda Kidau ufahamu kuwa mimi niliyetoa taarifa hii ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji (EXCOM) iliyoshiriki kupitisha maazimio ya agenda hiyo ambayo iliwasilishwa na Makamu wa Rais wa TFF, michael Wambura tarehe 28/10/2017 pale SEA SCAPE Kunduchi Beach. Usipokanusha madai yako ndani ya masaa 48 nitaweka hadharani mazungumzo ambayo niliyarekodi.

Ijumaa njema Wadau
 
Hii nchi sijui ni wapi pana nafuu, maana kila sekta ni madudu, alafu bado tuna ndoto
 
Shida sana mpira wa bongo kuendelea! kila mtu akiingia anaangalia maslahi yake
 
Back
Top Bottom