Kailima Ramadhan: Uchaguzi 2015 ulikuwa huru na wa haki, CHADEMA imeshindwa kihalali! Hakuna upendeleo kwa CCM, NEC ni Tume huru

Wanabodi,

Baada ya figisu figusu za uchaguzi wa marudio wa madiwani, nimebahatika ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, yaliyofanyika ofisini kwake jioni hii, kuhusu uchaguzi huo, katika kipindi cha Habari Zaidi ya Habari na PPR, ambacho kinarushwa kupitia Vituo 5 vya TV, TBC, ITV, STAR TV, Channel Ten, Azam TV, Clouds TV na kwenye Youtube.

Hizi ni Baadhi ya Dondoo za Mahojiano Hayo.
  • Zoezi la Uchaguzi limekwenda vizuri kwa asilimia 95%, hakukuwa na kasoro yoyote kubwa kuathiri uchaguzi huo, hivyo uchaguzi umekamilika na taarifa rasmi, itatolewa punde itakapokamilika.
  • Uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki, licha ya kutokea mapungufu madogo madogo, lakini matokeo ni matokeo halali, aliyeshinda ameshinda kihalali kwa haki, aliyeshindwa, pia ameshindwa kihalali kwa haki.
  • Hakuna hata chama kimoja, kilicholalamikia jambo lolote kuhusu uchaguzi huo, mpaka sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haijapokea malalamiko yoyote, kutoka chama chochote, au mgombea yoyote kwa mujibu wa utaratibu wa kujaza fomu za malalamiko.
  • Hakuna chama kilichojitoa rasmi, ila kama ilivyo kushiriki uchaguzi ni hiyari, vivyo hivyo vyama viko huru kujitoa wakati wowote, lakini mpaka zoezi la uchaguzi linamalizika, hakuna chama kilichojitoa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kujitoa.
  • Mawakala wa vyama, wanapatikana kwa mujibu wa sheria, taratkanuni, mtu ambaye hajakidhi taratibu za uchaguzi, hawezi kuruhusiwa
  • Ameelezea kuwa Tume yake ni Tume huru, inayoendesha chaguzi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, hakuna chama chochote, kimewahi kulalamikia kipengele chochote cha uchaguzi kinachonyima haki, kitakachoifanya tume isiwe huru.
  • Amesisitiza Tume yake haijawahi kuingiliwa na chombo chochote, wala kupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa yeyote.
  • Tume yake haijawahi kufanya upendeleo wowote kwa chama chochote, hata CCM nayo pia inailalamikia tume yake, hata uchaguzi wa Madiwani CCM Arusha wamelalamika.
  • Pia nimeuliza kuhusu Mkurugenzi, Mwenyekiti wa NEC na makashna kuteuliwa na rais ambaye ni mwenyekiti wa chama kimoja, wataweza kutenda haki?, pia amelijibu.
My Take.
Its high time vyama tuanze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, tukubali kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani, badala ya kutafuta visingizio.

Kama hali ya uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania, jee hali itakuwaje uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye sanduku la kura, kuna hatari ya CCM, kuyarejesha majimbo yote ya upinzani mwaka 2020, hivyo Tanzania kuanza safari ya kuelekea kuwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini ukweli tunaelekea kuwa nchi ya chama kimoja.

NB. Kipindi kikiwa tayari, nitakipandisha humu umsikilize mwenyewe.

Wasalaam.

Paskali

Huyu jamaa wampeleke mahakamani tu, mawakala wanafukuzwa, wanazuiwa kuingia, mkurugenzi siku 3 hapatika ni simu imezimwa, halafu anakuja tu kutamka ati ulikuwa wa huru na haki na sasa baadhi ya wabunge, mawakala wako lokapu, aisee inauma sana aisee, yote hayo hayaoni,
 
Sasa wewe ndiyo umesema ukweli WA wanalumumba wenzako....kweli mmeamua kutumia dola kuliko demokeasia
Tumebadilishana sera,demokrasia mchukue nyie,vurugu tuchukue sisi,fisadi mchukue nyie waadilifu waje kwetu,kulinda kura tuna linda sisi nyie mlalamike,ukanda tunachukua sisi nyie mbaki na waswahili,Kiki zote tumechukua sisi sasa nyie mnabaki na tweeter.
 
Unaweza Ona Watu Wanacheza Ngoma Lakini Husikii Sauti Ya Ngoma, Ukadhani Ni Vichaa Kumbe Wewe Ndio Kiziwi.!!

Wakati Mnataka Kuaminisha Umma Kuwa Upinzani Hatuna Hoja, Turejee Hoja Kuu Mbili za Msingi Bunge Live na Mikutano ya Kisiasa (Uhuru wa Kutoa Maoni), Hapa Ndipo Sehemu Sahihi ya Kupimana Kwa Hoja.

Nani alitudanganya kazi za vyama vya siasa ni kupambana na ufisadi na kuleta maendeleo? Hizo ni mojawapo ya kazi za serikali. Chama tawala kuishauri serikali yake, vyama vya upinzani kushauri na kuikosoa serikali na chama tawala. Hakuna ukomo wa maendeleo

Wale Wanasifia Kila Kitu Kinachofanywa Na Serikali!! Hawa wanaponda kila kitu kinachofanywa na serikali!! Halafu eti Wanachekana Na Kuzomeana Wakati Wako Kwenye Kundi Moja.

Then nakuomba kesho uandike thread ya kupinga mauaji kwenye uchaguzi.

mr mkiki.
Inasikitisha sana wewe hoja ya msingi kwako ni BUNGE LIVE na mikutano, watanzania hawataki kusikia hoja za kijinga namna hii. Endeleeni kupasha benchi joto mpaka mtakapopata akili.
 
Tume ya Uchaguzi imesema haijapokea barua rasmi ya malalamiko kutoka chama chochote kile..

Sasa Chadema badala ya kupeleka malalamiko NEC wanampelekea Da'Mange....upuuzi mtupu.
Hawaoni wakakemea, hawa jamaa watatupeleka na kutuingiza pabaya,
 
Hivi kweli kwa jinsi huyu mtu alivyo biased anaweza sema tofauti kweli
 
Upinzani wa wakina mbowe upinzani uchwara kinachosikitisha ni vijana wetu wengine very smart wamejikuta wanashabikia kampuni ya mtu wakidhani ni chama cha siasa (asante Mungu wenye akiri wametambua mapema na kurudi ccm) kama demokrasia haipo Tanzania wao wameshidaje wakawa wabunge?
Akili za fisi wewe
 
Mkuu BAK, uchaguzi ni process yenye sheria, taratibu na kanuni, zikiwemo taratibu za kuripoti malalamiko yoyote, kama hayo yote yametokea na hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, hadi uchaguzi unakamilika, hakuna yoyote aliyelalamika!, na hata kule kujitoa kwa Chadema, haikujitoa bali ilisusa tuu, kama ilivyo kanuni, unakuwa mgombea kwa kujaza fomu, na kujitoa ni kwa kutoa taarifa rasmi ya maandishi, na sio kuwaambia tuu waandishi wa habari. Tangazo lile ya kujitoa, lilipaswa kufuatiwa na kujaza fomu ya malalamiko, na kutoa taarifa rasmi ya kujitoa. Kama hakuna malalamiko yoyote registered, then tume iko right, no one complained!.

Paskali
Kwa hivyo wangejitoa wakati vitimbi vimeanza baada ya uchaguzi kuanza? Shameless kabisa
Ninyi stahiki yenu ni hii

20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
Isaya 5 :20

Kwenu mtu akifa huwa mnasubiri daktari aandike ripoti kuwa huyu kafa? Si we mwenyewe unaona tu mtu kweli kafa na dokta anakwambia tu kafa then taarifa baadae?

Ninyi ndiyo waandishi mnaotuharibia nchi hii sio siri.

Nimeongea nikiwa huru sina kadi ya chama hapa
 
Upinzani wa wakina mbowe upinzani uchwara kinachosikitisha ni vijana wetu wengine very smart wamejikuta wanashabikia kampuni ya mtu wakidhani ni chama cha siasa (asante Mungu wenye akiri wametambua mapema na kurudi ccm) kama demokrasia haipo Tanzania wao wameshidaje wakawa wabunge?
Kwamba serekali makini ya CCM inatoa ruzuku kwa kampuni?
 
Uchaguzibwa madiwani ushapiya, mawakala wamepigwa, wamelazwa lockup, wamezuiwa kuingia, kura hewa zimeongezwa, hivyo muwaache wafanye kazi lakini sidhani kama zitafanyika bila ushirikiano wa wananchi wanaongozwa, mi naona tutegemee zile sporadic attack, kwani wale waliopigwa ndugu zao sidhani kama watakaa kimya
 
Inasikitisha sana wewe hoja ya msingi kwako ni BUNGE LIVE na mikutano, watanzania hawataki kusikia hoja za kijinga namna hii. Endeleeni kupasha benchi joto mpaka mtakapopata akili.
Hii kitu chukulieni maguzi lakini madhara yake sio kwa mihemko tujione kwa kuwa ni ccm basi haina madhara kwetu. Madhara yetu ktk chama yako wazi yaani hatujuamini kutokana matendo yetu ndo yanatutafuna
 
Huyo jamaa Mungu amlipe kadri apendavyo maana ni Mungu pekee anayejua moyo wake unavyoitazama damu ya wengine. Anachonishangaza ni kuongea bila kupepesa kumbe anaongea kinazi,
 
Sawa ila msisahau kitisho kilichotolewa na mkuu kuwa "Mkurugenzi atumie raslimaliza serikali hii ya CCM halafu athubutu kumtangaza wa Upinzani kama mshindi"
 
Wanabodi,

Baada ya figisu figusu za uchaguzi wa marudio wa madiwani, nimebahatika ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, yaliyofanyika ofisini kwake jioni hii, kuhusu uchaguzi huo, katika kipindi cha Habari Zaidi ya Habari na PPR, ambacho kinarushwa kupitia Vituo 5 vya TV, TBC, ITV, STAR TV, Channel Ten, Azam TV, Clouds TV na kwenye Youtube.

Hizi ni Baadhi ya Dondoo za Mahojiano Hayo.
  • Zoezi la Uchaguzi limekwenda vizuri kwa asilimia 95%, hakukuwa na kasoro yoyote kubwa kuathiri uchaguzi huo, hivyo uchaguzi umekamilika na taarifa rasmi, itatolewa punde itakapokamilika.
  • Uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki, licha ya kutokea mapungufu madogo madogo, lakini matokeo ni matokeo halali, aliyeshinda ameshinda kihalali kwa haki, aliyeshindwa, pia ameshindwa kihalali kwa haki.
  • Hakuna hata chama kimoja, kilicholalamikia jambo lolote kuhusu uchaguzi huo, mpaka sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haijapokea malalamiko yoyote, kutoka chama chochote, au mgombea yoyote kwa mujibu wa utaratibu wa kujaza fomu za malalamiko.
  • Hakuna chama kilichojitoa rasmi, ila kama ilivyo kushiriki uchaguzi ni hiyari, vivyo hivyo vyama viko huru kujitoa wakati wowote, lakini mpaka zoezi la uchaguzi linamalizika, hakuna chama kilichojitoa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kujitoa.
  • Mawakala wa vyama, wanapatikana kwa mujibu wa sheria, taratkanuni, mtu ambaye hajakidhi taratibu za uchaguzi, hawezi kuruhusiwa
  • Ameelezea kuwa Tume yake ni Tume huru, inayoendesha chaguzi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, hakuna chama chochote, kimewahi kulalamikia kipengele chochote cha uchaguzi kinachonyima haki, kitakachoifanya tume isiwe huru.
  • Amesisitiza Tume yake haijawahi kuingiliwa na chombo chochote, wala kupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa yeyote.
  • Tume yake haijawahi kufanya upendeleo wowote kwa chama chochote, hata CCM nayo pia inailalamikia tume yake, hata uchaguzi wa Madiwani CCM Arusha wamelalamika.
  • Pia nimeuliza kuhusu Mkurugenzi, Mwenyekiti wa NEC na makashna kuteuliwa na rais ambaye ni mwenyekiti wa chama kimoja, wataweza kutenda haki?, pia amelijibu.
My Take.
Its high time vyama tuanze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, tukubali kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani, badala ya kutafuta visingizio.

Kama hali ya uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania, jee hali itakuwaje uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye sanduku la kura, kuna hatari ya CCM, kuyarejesha majimbo yote ya upinzani mwaka 2020, hivyo Tanzania kuanza safari ya kuelekea kuwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini ukweli tunaelekea kuwa nchi ya chama kimoja.

NB. Kipindi kikiwa tayari, nitakipandisha humu umsikilize mwenyewe.

Wasalaam.

Paskali

Pasko tafuta kweli nayo kweli itakuweka huru nawe utakuwa huru kweli kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom