Kahoho apeleka ombi Mahakama kuu kuwakamata DOWANS, wameuza mitambo kinyume na agizo

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Taarfa ya iliyoeleza kuwa mitambo ya kufua umeme ya kampuni tata ya DOWANS kwa kampuni ya Kimatekani ya Symbion Power kumesababisha Mwandishi wa habari mwandamizi Bw. Timoth Kahoho awasilishe maombi ya dharura katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba wakurugenzi wa DOWANS Holdings SA na DOWANS Tanzania Limited wakamatwe na kutiwa gerezani kwa kulidharau agizo la Mahakama.

Bwana Kahoho ambaye pia alipinga Tuzo waliyopoewa DOWANS na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) aliwasilisha ombi hilo jana mchana kufuatia wamiliki wa DOWANS kuuza mitambo yao kinyume na kauli ya mahakama iliyotaka kampuni hiyo kutoa taarifa mahakamani kwa chochote ikatakachotaka kufanya.

Mnamo Machi 3, mwaka huu, Jaji Emilian Mushi anayesikiliza kesi ya kuomba kusajiliwa kwa tuzo ya DOWANS alitoa amri ya kutaka pande zote mbili katika kesi hiyo 'kuacha mambo yote kama yalivyo' na endapo watataka kufanya jambo lolote wangepaswa kuomba kibali cha mahakama.

Katika maombi hayo, Bw. Kahoho alidai kuwa taarifa za madai ya kuuzwa mitambo ya Dowans ziliandikwa na gazeti la The African la Mei 21 mwaka huu, lilichapisha habari mitambo ya DOWANS imeuzwa kwa kampuni ya Symbion Power ya Marekani kwa thamani ya dola za Marekani 120.

Sambamba na ombi hilo, pia Bw. Kahoho anaiomba mahakama itoe amri ya kuwataka wadaiwa hao waweke dhamana dola la Marekani 120 kama dhamana, na walimpe gharama za kesi hiyo aliyoifungua jana.

Ombi hilo bado haijapangiwa jaji wa kuanza kuisikiliza.

Katika kesi ya msingi ya kupinga kusajiliwa tuzo ya Dowans itatajwa Julai 28, mwaka huu mbele ya Jaji Mushi, mbali na Bw. Kahoho wengine wanaopinga tuzo hiyo ni Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu (LHRC), Shirika la Umeme (TANESCO), ambao wanapinga tuzo ya Dowans isisajiliwe.

Mapema Januari 25 mwaka huu, Dowans iliwasilisha ombi lake la kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania isajili tuzo waliyopewa na ICC na siku chache baadaye Tanesco, LHCR, Kahoho wakawasilisha hati ya nia ya kupinga ombi hilo la kutaka tuzo hiyo isajiliwe kwa kuwa mahakama hiyo ya kimataifa haikuzingatia sheria za nchi katika hukumu yake.

Mahakama ya ICC, ilitoa hukumu ya kesi ya Dowans dhidi ya TANESCO, Novemba 15 mwaka jana, na kuitia hatiani Tanesco kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans na ikaimuru iilipe fidia ya shilini bilioni 94.
 
Hivi tanzania kuna mahakama tena za kuwafunga watu kama RACHEL?
 
Hivi tanzania kuna mahakama tena za kuwafunga watu kama RACHEL?
Kama mitambo imenunuliwa na wamerekani na balozi kubariki hapo hamna kesi wala nini,kama kawaida Rostam katupiga bao la kisigino.
 
Back
Top Bottom