Kahama: Watu Wawili wakutwa wamekufa Porini, Pori lachomwa moto

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
FB_IMG_1496875190400.jpg

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni madereva bodaboda wa mjini Kahama wamekutwa wakiwa wamekufa katika Shamba la miti linalomilikiwa na mkulima, Marco Nkuli katika eneo la Nyakato wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Watu hao ambao majina yao hayakufahamika mara moja, wamekutwa katika eneo hilo kufuatia msako uliofanywa na madereva bodaboda katika mashamba hayo wakimtafuta dereva mwenzao aliyekuwa amepotea na kukutwa ameuawa kwenye msitu huo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Baada ya kukuta miili hiyo waendesha bodaboda wameamua kuchukua uamuzi wa kuteketeza kwa moto mashamba ambako miili hiyo imekutwa.

Baadhi ya madereva bodaboda wamesema kuwa miili hiyo imekutwa ikiwa na majeraha sehemu mbali mbali huku viungo vingine vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa eneo vikiwa katika eneo hilo.

Wakiongea mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya, Madereva hao wameiomba serikali kumnyang’anya mmiliki huyo eneo hilo kwani limekuwa likitumika kama kichaka cha kujifichia wahalifu wanaowateka na kuwaua madereva bodaboda na kuchukua pikipiki zao.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida madereva hao wamevamia na kuchoma moto mashamba hayo ya miti yanayokadiriwa kuwa na ukubwa wa heka 50 huku wakisema kuwa uamuzi huo umelenga kusafisha eneo hilo ambalo linadaiwa kuficha wahalifu.

Nao baadhi ya majirani wanaoishi kuzunguka mashamba hayo wamepongeza uamuzi huo wa madereva boda boda kuchoma eneo hilo, na kuongeza kuwa wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na uwepo wa vichaka hivyo.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha upelelezi Polisi Kahama, George Bagemu amesema watuhumiwa watatu wa mauaji hayo wamekamatwa Kakonko mkoani Kigoma na watasafirishwa kuletwa Kahama kwa ajili ya hatua zaidi za upelelezi.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la matukio ya kutekwa kwa madereva bodaboda na pikipiki zao kuibiwa wilayani Kahama.
 
Kahama vibaka ni wengi sana...na kama u mgeni ukifikia gesti hakikisha unakagua madirisha kama yamefungwa kabla ya kulala.
 
muuaji inabidi asakwe kwa garama zozote na yeye apate stahiki yake, inasemekana amekimbilia geita/katoro...!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom