Kahama, Shinyanga: Waandishi wa habari wafikishwa Mahakamani kwa kujifanya Maafisa Usalama na kutapeli mganga wa jadi

Zakamwamoba

Senior Member
Jul 28, 2016
177
609

Waandishi wa habari watano wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa mahakamani wilayani Kahama kwa makosa ya kujifanya maafisa usalama wa taifa na kujipatia fedha shilingi Milioni 1 kutoka kwa mganga wa jadi.

Waandishi hao wa habari ambao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru,Raymond Mihayo- Habarileo,Shaban Njia Jamboleo, Simon Dioniz – Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama leo Jumatano Januari 10,2018.

Waandishi hao walikamatwa jana saa saba na nusu mchana na jeshi la polisi wakijifanya maafisa wa usalama wa taifa kutoka Dar es salaam,Kigoma,Kagera,Shinyanga na Kahama kisha kujipatia shilingi 1,000,000/- kutoka kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi (46) mkazi wa kitongoji cha Ng’wande kata ya Mwaluguli wilayani Kahama baada ya kumtishia kuwa anapiga ramli chonganishi.

Walikamatwa baada ya kuwekewa mtego kwani waliahidiwa fedha zingine tena shilingi milioni 1 na mganga huyo wa jadi baada ya kuchukua shilingi milioni 1 tarehe 6.1.2018.

Waandishi hao wa habari Shaban Njia,Paul Kayanda,Simon Dioniz na Raymond Mihayo wamepelekwa gerezani baada kushindwa kutimiza masharti ya dhamana huku George Maziku akiendelea kutafutwa kwani bado hajapatikana,alishiriki kuchukua fedha 6.1.2018,jana hakukuenda kuchukua fedha.

Chanzo; MTILAH BLOG
 
waandishi+pic.jpg

Shinyanga/Mwanza. Wanahabari wanne wa vyombo mbalimbali vya habari wilaya ya Kahama wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujipatia Sh1milioni kutoka kwa mganga wa jadi baada ya kujifanya maofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza leo Januari 10, 2018 Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amewataja waandishi hao na vyombo vyao katika mabano kuwa ni Paul Kayanda (gazeti la Uhuru), Shaban Njia (Nipashe), Simon Dionis (Radio Kwizera) na Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo, huku mmoja akikimbia.

Amesema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo jana Januari 9 saa 7 mchana katika kitongoji cha Ng’wande kijiji cha Bani wilayani Kahama baada ya kumtishia mganga huyo, Jane Mbeshi (46) kuwa wao ni maofisa usalama kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kagera, Shinyanga na Kahama.

Amebainisha kuwa baada ya kujitambulisha, walimtaka mganga huyo kuwapa kiasi cha Sh2 milioni ili wasimtie mbaroni kwa kosa la kupiga ramli chonganishi.

“Januari 6 watuhumiwa walipokea Sh1 milioni kutoka kwa mganga huyo kwa makubaliano kuwa kiasi kingine kilichosalia wangepewa siku nyingine,” amesema Haule na kuongeza,

“Baada ya kupokea taarifa hizo polisi waliweka mtego na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa watatu kati ya watano waliofika nyumbani kwa mganga huyo kupokea kiasi cha fedha kilichosalia.”

Amesema waliokamatwa kwenye eneo la tukio ni Kayanda, Njia na Dionis huku Mihayo akijisalimisha mwenyewe polisi jana, kwamba mtuhumiwa wa tano, George Maziku anaendelea kusakwa na polisi.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanaccm mmoja wa Arusha alijifanyaga. Nahisi DPP aliishiwa nia ya kuendelea na ile kesi. Akaachiwa

Habari Leo,Uhuru.
 
image.jpeg

. KAHAMA, SHINYANGA: Jeshi la Polisi limewakamata waandishi wa habari 5 kwa tuhuma za kujifanya usalama wa taifa na kutapeli fedha kiasi cha Sh. milioni moja kutoka kwa mganga wa kienyeji.

Waandishi hao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru, Raymond Mihayo wa Habarileo, Shaban Njia wa Jambo Leo, Simon Dioniz wa Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani.
 
Wanahabari wanne wa vyombo mbalimbali vya habari wilaya ya Kahama wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujipatia Sh1milioni kutoka kwa mganga wa jadi baada ya kujifanya maofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza leo Januari 10, 2018 Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amewataja waandishi hao na vyombo vyao katika mabano kuwa ni Paul Kayanda (gazeti la Uhuru), Shaban Njia (Nipashe), Simon Dionis (Radio Kwizera) na Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo, huku mmoja akikimbia.

Amesema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo jana Januari 9 saa 7 mchana katika kitongoji cha Ng’wande kijiji cha Bani wilayani Kahama baada ya kumtishia mganga huyo, Jane Mbeshi (46) kuwa wao ni maofisa usalama kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kagera, Shinyanga na Kahama.

Amebainisha kuwa baada ya kujitambulisha, walimtaka mganga huyo kuwapa kiasi cha Sh2 milioni ili wasimtie mbaroni kwa kosa la kupiga ramli chonganishi.

“Januari 6 watuhumiwa walipokea Sh1 milioni kutoka kwa mganga huyo kwa makubaliano kuwa kiasi kingine kilichosalia wangepewa siku nyingine,” amesema Haule na kuongeza,

“Baada ya kupokea taarifa hizo polisi waliweka mtego na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa watatu kati ya watano waliofika nyumbani kwa mganga huyo kupokea kiasi cha fedha kilichosalia.”

Amesema waliokamatwa kwenye eneo la tukio ni Kayanda, Njia na Dionis huku Mihayo akijisalimisha mwenyewe polisi jana, kwamba mtuhumiwa wa tano, George Maziku anaendelea kusakwa na polisi.
 
View attachment 672573
. KAHAMA, SHINYANGA: Jeshi la Polisi limewakamata waandishi wa habari 5 kwa tuhuma za kujifanya usalama wa taifa na kutapeli fedha kiasi cha Sh. milioni moja kutoka kwa mganga wa kienyeji.

Waandishi hao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru, Raymond Mihayo wa Habarileo, Shaban Njia wa Jambo Leo, Simon Dioniz wa Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani.
Njaa kali sana gazeti la uhuru .
 
Back
Top Bottom