Kahama, Shinyanga: Lori la mafuta lateketea kwa moto na kupelekea utingo kufariki

Hilo la shunu lilianguka na kulipuka hapohapo so wasigelisogelea nashangaa wanaposema kuwa polisi walimuokoa dereva wakati walikuta kaishatolewa
Nimeiona habari mashuuda wa ajali zote mbili (Isaka na Shunu) wanasema raia walikimbia baada ya ajali. Lori moja ndio lililoungua.
Nafikiri mtoa mada kaongeza chumvi tu
 
Walitamani ?

Hiv kwa vifo vinavyoendelea muhimbili bado watu wanatamani?
Si aliyeripoti kasema limeanguka na kuwaka moto? Sasa hao waliotamani na kuzuiwa na polisi walitamani saa ngapi, maana hatujaambiwa ulipita muda gani tangy kuanguka na kuwaka moto
 
Hilo la shunu lilianguka na kulipuka hapohapo so wasigelisogelea nashangaa wanaposema kuwa polisi walimuokoa dereva wakati walikuta kaishatolewa
Hata Mimi naona hapa Luna makosa kwenye uwasilishaji wa taarifa
 
Lori la mafuta ya mawese? ya kujichua? ya transfoma? ya vaseline? ya karanga? ya taa? ya pamba, ya diesel, ya samli, ya petroli, ya ndege, ya alizeti ????

Waandishi wa media zetu shule ndogo sana.
 
Nilikuwa naingia kwenye keepleft ( round about) bibi mmoja na kikapu chake akawa anakatiza katikati ya roundabout. Ikanibidi nisimamishe gar ili apite. Sasa ist lililokuwa mkono wa kulia ikaja moja kwa moja na kunigonga ubavu kwa nyuma.

Kwa kuwa gar yangu ipo juu na ngumu, damage haikuwa kubwa kwangu. IST iliyonigonga ikawa imechakalika shoo ya mbele. Sasa akageukia mimi ndye nimlipe.

Tukaenda hadi police. Police wakatoa amri kuwa mimi ndye nimlipe coz yeye alikuwa mkono wa kulia na hairuhusiwi kusimama kwenye round about.

Sasa mpaka leo huwa najiuliza, hivi nisingesimama na ningemngonga huyu bibi kwenye round about kesi ingekuwaaje?
Ungepita tu na huyo bibi, mimi huwa sirembi nanyooka tu, atajuana na nduguze, ***** zake
 
Lori la mafuta ya mawese? ya kujichua? ya transfoma? ya vaseline? ya karanga? ya taa? ya pamba, ya diesel, ya samli, ya petroli, ya ndege, ya alizeti ????
Waandishi wa media zetu shule ndogo sana.
Hatakuandika LORI mkuu wanashindwa. Nimejisikia aibu kusoma andiko la mleta mada. Nini maana ya ROLI?? Anyway tusihukumu.
 
Si aliyeripoti kasema limeanguka na kuwaka moto? Sasa hao waliotamani na kuzuiwa na polisi walitamani saa ngapi, maana hatujaambiwa ulipita muda gani tangy kuanguka na kuwaka moto
Hebu soma vzr habari
 
Mtoa roho amekwisha wasiliana nawe tena! Loh...

Yaani pamoja na watu wa Moro kuteketea kwa moto juzi bado kuna watu huko Kahama walitaka kwenda kuiba mafuta baada ya ajali kutokea! Kweli kusikia kwa kenge...

wabongo ni vichwa wa wendowazimu
 
Kumetokea ajali mbili za malori ya mafuta zilizosababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi kadhaa huko Kahama mkoani Shinyanga.

Katika kile kinachoonekana kama kueleweka kwa somo la kuchukua tahadhari juu ya hatari ya moto, wananchi walitimua mbio wakiacha mafuta ya petroli kutoka kwenye lori mojawapo yakimwagika mtaroni.

Moja ya malori hayo ya mafuta yaliyopata ajali usiku wa jana liliwaka moto na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyekuwa abiria kwenye lori hilo.

Chanzo: ITV Habari
Petro, Dadavua issues za sheria, acha huu uandishi wa darasa la saba failures. Wewe tunakutegemea kutoa elimu ya sheria for this forum, siyo hii habari uchwara. hii waachie akina Pascal Mayalla and the like! We need thought provoking themes from you! Nasikia GPA yako ni matata! tena from UDSM. Sasa why engage in these petty issues!
 
Hatakuandika LORI mkuu wanashindwa. Nimejisikia aibu kusoma andiko la mleta mada. Nini maana ya ROLI?? Anyway tusihukumu.

Sasa msikilize huyu mheshimiwa wa TBC anatoa coverage mubashara kutoka eneo la tukio la kuliondoa lori...




...mwandishi anasema kama wakiliinua tanker wakakuta bado lina mafuta tafsiri yake ni moja tu, lori litalipuka! (hahahaaaa....sasa mbona kalikalia beneti na ana interview raia hapo hapo kama linaenda kulipuka sekunde yoyote endapo watakuta ndani lina mafuta???)

...anasema wanachi wengi wako hapa wanashuhudia zoezi la uondoaji wa tanker... baadae akasema hapa tumeruhusiwa waandishi tuu, hamna raia hapa!.. hahahahaaa.... we si umesema watu wapo wanashuhudia???

...anasema "cha kufurahisha ni kwamba madaktari wa Muhimbili washafika hospitali ya rufaaa Morogoro"!

Hivi kuna nini cha "kufurahisha" wakati wa msiba?? Kuna maneno huwa hayapaswi kutumika nyakati fulani, na hili ni la busara za kawaida tu, halifundishwi chuo cha uanahabari...

Mzee wa TBC kaongea pumba tupuuuuuu!
 
Roli la mafuta linalomilikiwa na Kampuni ya Interpetrol ya Burundi limepinduka maeneo ya jirani ya Isaka.

Kwa mazingira yalivyokuwa pale eneo la tukio iliniwia vigumu kupata japo picha maana Vyombo vya Ulinzi na usalama walizuia.

Jambo la kupongezwa INASEMEKANA POLISI NA ZIMAMOTO WA ENEO HILO WAMEVUNJA REKODI YA KUWAHI ENEO LA TUKIO!
waambie wafyatue bomu la machozi
 
Back
Top Bottom