Kahama, Shinyanga: Lori la mafuta lateketea kwa moto na kupelekea utingo kufariki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
IMG-20190817-WA0033.jpg

Lori lenye shehena ya mafuta la kampuni ya Mount Meru Company limeanguka na kuwaka moto wilayani kahama mkoani Shinyanga na kusababisha kifo cha utingo wa lori hilo aliyefahamika kwa jina moja la Erik huku dereva wake Ibrahimu Issa akijeruhiwa kwa moto.

Lori hilo lenye namba za usajili RAD 416V na Tela namba RL 1950 likitokea Dar es laam likiekea nchini Rwanda likiendeshwa na Ibrahim Issa limepata ajali hiyo katika mtaa wa shunu usiku wa kuamkia leo na kulipuka wakati likikwepa gari dogo aina ya Toyota Voltz.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mtaa wa shunu, Kube Shija amesema baada ya tukio hilo kutokea alitoa taarifa kwa jeshi la polisi na walifanikiwa kuwazuia wananchi ambao walitamani kwenda kuiba mafuta lakini walifanikiwa kuwazuia.

Amesema ni vyema wananchi wakajifunza kutokana na majanga ya moto kama vile ajali ya morogoro ambapo watu wengi wamefariki dunia kwa kutokimbilia magari ya mafuta pindi yapo anguka ili kuzuia madhara kama vile vifo.

Frank kalebela na Asha Hamisi ni baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema ni vyema serikali ikatoa elimu juu ya majanga ya moto ili kuzuia vifo visvyokuwa vya lazima ambavyo vinasababishwa tamaa za kujipatia mali.

Ibrahimu Mussa ni dereva wa lori hilo ambaye anapatiwa matibabu katika hospiali ya Halmashauri ya mji wa kahama amesema ajali hiyo imetokea wakati akimkwepa dereva wa gari dogo ambaye alikuwa anajaribu kupita bila kuchukua tahadhari na kusababisha gari hilo kuanguka.

Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya kahama Dumma Mohamed amesema walifanikiwa kuuzima moto huo na kumwokoa dereva wa gari hilo ambaye mpaka sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama

Amewataka wananchi kutoa taarifa za majanga ya moto na kuacha tabia ya kupiga picha na kuzisambaza mtandaoni ili kuweza kuokoa mali za watu pindi moto unapotokea.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani shinyanga ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali.
 
Kuna watu uzembe wao unagharimu maisha ya wenzao,
ukiangalia
ajali ya sister wa kifungilo na dereva wake utaskia.....kukwepa.
ajali ya moro..... Kukwepa.
hii nayo .....kukwepa,
na nyingne nying sana,
kijitu na uzembe wake kimeteketeza watu karbun mia na wengne wanaungumia kwa mateso,

Mtu akijileta, kama anakupa wakat mgumu pita naye, unless kama kuna safe option.
lawama hapewi mbuzi,
 
Mtoa roho amekwisha wasiliana nawe tena! Loh...

Yaani pamoja na watu wa Moro kuteketea kwa moto juzi bado kuna watu huko Kahama walitaka kwenda kuiba mafuta baada ya ajali kutokea! Kweli kusikia kwa kenge...
Kwa akili zetu za kibongo za kupenda vya bure hata leo lorry la mafuta likianguka pale msamvu bado watu watajazana kuchota mafuta ila nadhani watakuwa makini sana kuwazuia mateja kuchomoa betri
 
Kuna watu uzembe wao unagharimu maisha ya wenzao,
ukiangalia
ajali ya sister wa kifungilo na dereva wake utaskia.....kukwepa.
ajali ya moro..... Kukwepa.
hii nayo .....kukwepa,
na nyingne nying sana,
kijitu na uzembe wake kimeteketeza watu karbun mia na wengne wanaungumia kwa mateso,

Mtu akijileta, kama anakupa wakat mgumu pita naye, unless kama kuna safe option.
lawama hapewi mbuzi,
Wangewaacha hatujachoka kusema RIP maana kenge huwa hasikii hadi damu imtoke
 
Sasa la bia limedodondoka jion hii njia panda ya Monduli, watu wanakimbilia kuiba bia duu hapana aisee....kwan watu wanafikir la bia ndo halitaweza leta athar, nimefurah coz limedondokea maeneo ya JWTZ makamanda walisimamia na kuwaondoa wote waliojifanya wanafaham ulev...mpaka muda huu bia zote zimekuwa transfered kwa gari nyingine kwa usimamiz na ulinz wa makamanda, na semi ndo inafanyiwa taratibu za kuvutwa sasa naona matukio yanazid tu.
 
Back
Top Bottom