Kahama: Rais Magufuli amsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri aliyenunua gari kinyume na utaratibu. Kahama yapandishwa hadhi kuwa Manispaa

Kahama ni mji unaokua kwa kasi kubwa sana nchini. Kwa mujibu wa taarifa serikalini, Kahama imekuwa ni halmashauri ya mji ambao umekuwa ukiongoza kimapato. Ni mji wenye idadi kubwa ya watu na ongezeko kubwa la watu wanaohamia na kupenda kuishi.

Pamoja na yote hayo, Kahama ni mji ambao uko busy sana kibiashara na ukiambatana na kila aina za biashara yoyote mtu anayoweza kufanya! Kila aina ya Bank zipo nk.

Licha ya sifa zote hizo za miaka mingi, Kahama ilikuwa haijapewa hadhi ya manispaa. Hatimaye mwezi January mwishoni, mwaka huu 2021, halmashauri ya mji wa Kahama umepewa hadhi ya manispaa na kuwa manispaa ya Kahama!

Kuna mwaka niliandika kuwa mji wa Kahama ulistahili hadhi hii kulingana na maendeleo yake. Kuna waliounga mkono, lkn baadhi waliibeza Kahama. Waliibeza kwa kujaribu kulinganisha Niombe, mara Tandaimba na kwingineko. Lakini, kwa tamko la Rais kuipa hadhi ya manispaa, ni kudhihirisha Kahama umepiga hatua kubwa sana kimaendeleo, hata hivyo ilicheleweshwa kupewa hadhi hiyo ya manispaa!

Kwa kasi iliyopo na mwamko wa wananchi, biashara zilizopo na ongezeko kubwa la watu likiambatana mzunguko wa pesa uliopo ambao unasukuma maendeleo kwa kiasi kikubwa, sisiti kusema kuwa miaka10-15 ijayo, Kahama itakuwa jiji.
 
Back
Top Bottom