Kahama: Rais Magufuli amsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri aliyenunua gari kinyume na utaratibu. Kahama yapandishwa hadhi kuwa Manispaa

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,882
2,000
Hao DED, MD nk nk nk ni Watanzania wenzako kama wewe. Acha kulala ukiumia juu ya Cheo cha Mwenzako na kumwombea Njaa! Pambana Familia yako Watoto Wasome Kisawa sawa shule za Maaana.

Pambana uwe na Pesa Chaffu halafu utapata Connection then wanao ndio Watakuwa hao hao Wenye ma V8 VXR! Kulalalamika lalamika na kuombea wengine njaa ni ishara ya Umaskini na Uchawi Mkuu. Pambana mpaka kieleweke acha wivu!
Wewe ni mnufaika wa mfumo huu.
Lakini mwisho wenu umewadia.
 

Camp 05

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
1,373
2,000
Kama mada inavyojieleza,

Tunaona suala la ununuzi wa magari ya Wakurugenzi kwa bei ya anasa limezimwa.
Wazalendo tunajiuliza maswali mengi sana;huenda ni kweli kuwa mheshimiwa rais amewaogopa Wakurugenzi,au Jaffo,au PM
Sasa tunaomba tujue,kati ya hawa,ni nani uliyemuogopa?.

Tunaumia sana mali zetu zinapotumika vibaya,halafu mlinzi mkuu wa mali zetu anakaa kimya,na anasamehe bila sababu mmoja wa watuhumiwa (DED wa Kahama). Mheshimiwa, tuambie.

Unamwogopa yupi?
Kwani hujui kuwa hao ndo waliosimamia wajumbe kushinda uchaguzi
 

Dig the EA

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
222
250
Kahama ni mji unaokua kwa kasi kubwa sana nchini. Kwa mujibu wa taarifa serikalini, Kahama imekuwa ni halmashauri ya mji ambao umekuwa ukiongoza kimapato. Ni mji wenye idadi kubwa ya watu na ongezeko kubwa la watu wanaohamia na kupenda kuishi.

Pamoja na yote hayo, Kahama ni mji ambao uko busy sana kibiashara na ukiambatana na kila aina za biashara yoyote mtu anayoweza kufanya! Kila aina ya Bank zipo nk.

Licha ya sifa zote hizo za miaka mingi, Kahama ilikuwa haijapewa hadhi ya manispaa. Hatimaye mwezi January mwishoni, mwaka huu 2021, halmashauri ya mji wa Kahama umepewa hadhi ya manispaa na kuwa manispaa ya Kahama!

Kuna mwaka niliandika kuwa mji wa Kahama ulistahili hadhi hii kulingana na maendeleo yake. Kuna waliounga mkono, lkn baadhi waliibeza Kahama. Waliibeza kwa kujaribu kulinganisha Niombe, mara Tandaimba na kwingineko. Lakini, kwa tamko la Rais kuipa hadhi ya manispaa, ni kudhihirisha Kahama umepiga hatua kubwa sana kimaendeleo, hata hivyo ilicheleweshwa kupewa hadhi hiyo ya manispaa!

Kwa kasi iliyopo na mwamko wa wananchi, biashara zilizopo na ongezeko kubwa la watu likiambatana mzunguko wa pesa uliopo ambao unasukuma maendeleo kwa kiasi kikubwa, sisiti kusema kuwa miaka10-15 ijayo, Kahama itakuwa jiji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom