Kahama: Rais Magufuli amsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri aliyenunua gari kinyume na utaratibu. Kahama yapandishwa hadhi kuwa Manispaa

Mapank

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,682
2,000
Idadi ya watu Kahama inakaribia laki 3 ni mji wa nane kwa wingi wa watu nchini kwa mujibu wa sensa ya 2012

Mapato inachangia 50% ya mapato yote ya mkoa..wa Shinyanga.

Inaendesha miradi mingi kwa fedha za ndani kwa hiyo sio tegemezi..

Asilimia zaidi ya 50 ya wakazi wake wameajiriwa katika sekta ya biashara na sekta nyingine rasmi.. kwa hiyo hawategemei kilimo.

Kwa kawaida hivyo ndio vigezo muhimu
Wilaya ya Kahama ina watu 1.2m na Manispaa ndio ina 320k kwa makadirio ya mwaka 2021
 

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,882
2,000
Kama mada inavyojieleza,

Tunaona suala la ununuzi wa magari ya Wakurugenzi kwa bei ya anasa limezimwa.
Wazalendo tunajiuliza maswali mengi sana; huenda ni kweli kuwa mheshimiwa Rais amewaogopa Wakurugenzi au Jaffo au PM
Sasa tunaomba tujue, kati ya hawa ni nani uliyemuogopa?.

Tunaumia sana mali zetu zinapotumika vibaya halafu mlinzi mkuu wa mali zetu anakaa kimya na anasamehe bila sababu mmoja wa watuhumiwa (DED wa Kahama). Mheshimiwa, tuambie.

Unamwogopa yupi?
 

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,589
2,000
Mi nadhani Kuna Mambo makubwa ambayo huyu DED aliyafanya,kwa kujitoa au hata kuhatarisha maisha yake,na huenda yalikuwa hayafahamika kwetu.kama alivyosema jpm asijisahau sikunyingine akarudia ujinga huu.
 

Kiwoso 1

Member
Jan 30, 2021
58
150
Anaogopa kivuli chake kummbuka Hawa wagurugenzi ndio wenye Siri kuu ya ushindi wake hapo mwaka jana
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,101
2,000
RC, DED, DAS, RAS, RC, RPC, RAC, DAC etc piga mahesabu wote wana KILIMO KWANZA V8 kama Maputo bei zaidi ya 300m piga mahesabu Nchi nzima kuna ma RC , RAS , DC, DAS etc wangapi na wote wana hizo ndinga.

Ukija kwenye mashirika ya umma ni mwendo huo huo ,kwenye majeshi mwendo huo huo!!

Ni upuuzi kuwa na migari kibao na midege halafu hakuna ventileta wala panadol hospitalini.
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,101
2,000
Halafu unamkuta mbele ya hadhara akijisifia eti yupo kwa ajili ya wanyonge!! Msafara wake wenyewe tu ni kufuru tupu.

Yaani viongozi wa kiafrika wanaongea tofauti na wanayofanya ,wafanyakazi wa makampuni binafsi wanaolipwa 1.2m hadi 3m wanamiliki magari wananunua kwa pesa zao ,sasa inakuwaje viongozi wakubwa wa serikali.

wanaolipwa mamilioni ya shilingi wasiweze kujinunulia magari yao wenyewe mpaka serikali iwanunulie magari ya milioni 300? Inatakiwa tupate raisi mzalendo atkayekuja kufuta huo ujinga na fedha ikawekezwa kwenye afya,elimu,maji,umeme,barabara etc
 

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
4,241
2,000
Hao DED, MD nk nk nk ni Watanzania wenzako kama wewe. Acha kulala ukiumia juu ya Cheo cha Mwenzako na kumwombea Njaa! Pambana Familia yako Watoto Wasome Kisawa sawa shule za Maaana.

Pambana uwe na Pesa Chaffu halafu utapata Connection then wanao ndio Watakuwa hao hao Wenye ma V8 VXR! Kulalalamika lalamika na kuombea wengine njaa ni ishara ya Umaskini na Uchawi Mkuu. Pambana mpaka kieleweke acha wivu!
 

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,332
2,000
RC,DED,DAS,RAS,RC,RPC,RAC,DAC etc piga mahesabu wote wana KILIMO KWANZA V8 kama Maputo bei zaidi ya 300m piga mahesabu Nchi nzima kuna ma RC ,RAS ,DC,DAS etc wangapi na wote wana hizo ndinga....
Sio kwel kuna madas wanatembelea gar za kawaida tena za donors tu na wala sio V8
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom