Kahama: Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga azuiwa kuingia mgodi wa Bulyanhulu

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,388
24,947
Kahama. Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack umezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini(TMAA).

Maofisa hao waliondoka mara baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu kupokelewa na Rais John Magufuli.

Akizungumza kwa njia ya simu jioni hii, Tellack anayefanya ziara ya kikazi wilayani Kahama amesema ameagiza jeshi la polisi kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Mapema leo, mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.

Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
sababu?
Maana hii habari imekaa kihoax hoax kweli.
Haina kichwa wala miguu inhang tuu
Mkuu dadavua basi tupate full details
 
Haya sasa! Tatizo la dhahabu ni kwamba wanaojua thamani yake ndio hao wanaotengeneza mitambo ya kuichimba na hata ukiichimba wewe unalazimika kuwauzia wao then wanageuka wapangaji wa bei.
 
Sijawahi kuwa muumini wakujiletea maendeleo kwa njia ya mateso sitawahi kuwa maisha yangu yote hayo mambo wanaweza timu mkuu,

Yaani ilitufikie maendeleo ndo ayo maumivu watanzania wavumilie waliambiwa kwani atuwezi kuwa na njia za maana zisizo na taabu

Na subiri majibu ya wavivu wa kufikiri
 
Ya kweli lakini au hadithi za abunwasi?? Mbona wamechelewa saana tu. Kama kweli, tani hizo zilikutwa kwenye mchanga lundikwa, hakuna haja ya kumjali mwizi. Liwalo na liwe tuuu. Kama mbwayi nii mbwayii
 
Nimekumbuka Fao la kujitoa lilifikia wapi jamani kama ni mpaka miaka 60 twafya!
 
Back
Top Bottom