Gari la Waziri Ummy Mwalimu limepata ajali ambapo mwendesha baiskeli kagongwa na kujeruhiwa.
Kama ilivyo ada magari yao yakipata ajali dereva wao si wa kulaumiwa ila kina sisi.
Mwendo wao hakuna kikomo ila kwa akina sisi.
Hadi pale sheria barabarani zitakapo kuwa sawa sawa kwa kila mtu ni suala la muda tu, wala hakuna sababu ya kuchoka kutuma rambirambi.
======
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Simon Haule amesema gari hilo lenye namba za usajili STL 2777 Mali ya Wizara ya Afya likiendeshwa na Dereva Bw. Jumanne Ally amemgonga Marko Charles mkazi wa kata ya Busoka katika Halmashauri ya mji wa Kahama.
Amesema Waziri Ummy alikuwa akitokea wilayani Ngara kwenye ziara ya kikazi ya siku moja na kwamba Bw. Marco aliegongwa amepata majeraha kwenge bega na mkono wa kushoto na amelazwa hospitali ya mji wa Kahama.
Hata hivyo Kamanda Haule amsema baada ya ajali hiyo dereva ameruhusiwa kuendelea na safari kwani Waziri anaelekea Dodoma kikazi na uchunguzi bado unaendelea kwani ikithibitika dereva alifanya uzembe atafikishwa Mahakamani.