Kahama: Gari la Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, limepata ajali

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Messages
1,148
Points
2,000

brazaj

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2016
1,148 2,000
Gari la Waziri Ummy Mwalimu limepata ajali ambapo mwendesha baiskeli kagongwa na kujeruhiwa.

Kama ilivyo ada magari yao yakipata ajali dereva wao si wa kulaumiwa ila kina sisi.

Mwendo wao hakuna kikomo ila kwa akina sisi.

Hadi pale sheria barabarani zitakapo kuwa sawa sawa kwa kila mtu ni suala la muda tu, wala hakuna sababu ya kuchoka kutuma rambirambi.

======

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Simon Haule amesema gari hilo lenye namba za usajili STL 2777 Mali ya Wizara ya Afya likiendeshwa na Dereva Bw. Jumanne Ally amemgonga Marko Charles mkazi wa kata ya Busoka katika Halmashauri ya mji wa Kahama.

Amesema Waziri Ummy alikuwa akitokea wilayani Ngara kwenye ziara ya kikazi ya siku moja na kwamba Bw. Marco aliegongwa amepata majeraha kwenge bega na mkono wa kushoto na amelazwa hospitali ya mji wa Kahama.

Hata hivyo Kamanda Haule amsema baada ya ajali hiyo dereva ameruhusiwa kuendelea na safari kwani Waziri anaelekea Dodoma kikazi na uchunguzi bado unaendelea kwani ikithibitika dereva alifanya uzembe atafikishwa Mahakamani.
 
Jr. Gong Mira

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Messages
1,147
Points
2,000

Jr. Gong Mira

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2017
1,147 2,000
Gari la Waziri Ummy Mwalimu limepata ajali ambapo mwendesha baiskeli kagongwa na kujeruhiwa.

Kama ilivyo ada magari yao yakipata ajali dereva wao si wa kulaumiwa ila kina sisi.

Mwendo wao hakuna kikomo ila kwa akina sisi.

Hadi pale sheria barabarani zitakapo kuwa sawa sawa kwa kila mtu ni suala la muda tu, wala hakuna sababu ya kuchoka kutuma rambirambi.
Pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAU 1

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
486
Points
250

TAU 1

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2013
486 250
Gari la Waziri Ummy Mwalimu limepata ajali ambapo mwendesha baiskeli kagongwa na kujeruhiwa.

Kama ilivyo ada magari yao yakipata ajali dereva wao si wa kulaumiwa ila kina sisi.

Mwendo wao hakuna kikomo ila kwa akina sisi.

Hadi pale sheria barabarani zitakapo kuwa sawa sawa kwa kila mtu ni suala la muda tu, wala hakuna sababu ya kuchoka kutuma rambirambi.
Hili ni tatizo kubwa sana na pengine watu wa magari ya viongozi na viongozi wao wataendelea kupata ajali! Inasikitisha sana kwamba sheria za barabarani na tochi za ma traffic police zinatuhusu tu sisi walala hoi,hata pale unapotakiwa kuendesha 50km per hr ukizidisha tu 51 unapigwa faini ila hao wenye nchi yao magari yao yanapita sehemu hiyo hiyo yakiwa na speed 140 km/hr lakini polisi hawawafanyi chochote! It is when rule of law shall be abided to everyone yaani sheria isitazame ni yupi kafanyakosa ila ichukue mkondo wake....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,390,496
Members 528,186
Posts 34,052,542
Top