Kahaba, mzinzi, malaya, kiruka njia haya maneno yana maana gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kahaba, mzinzi, malaya, kiruka njia haya maneno yana maana gani?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by ummu kulthum, Feb 8, 2012.

 1. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  haya maneno yananichanga nimeyatoa jukwaa la mahaba hebu nijuzeni tafadhali, wana jf 4 real
   
 2. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,716
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  ummu kulthum,

  rejea mada yako hapo juu...siyo kahamba bali ni kahaba.

  kahaba na malaya ni maneno mawili yanayomaanisha sifa moja nayo ni mtu mwenye tabia ya kushiriki mapenzi na watu anuwai(wengi, tofauti tofauti). Mfano kama fulani mumewe au rafikiye wa kiume ni bwana X lakini pia anashiriki mapenzi na bwana Y, bwana Z n.k. akitumia kinga au asitumie, ameolewa au mjane bado ataitwa malaya kadhalika kahaba.

  sifa ya umalaya au ukahaba imekuwa ikinasibishwa zaidi na wanawake hasa kwa vile wanaume wamekuwa wakidai kuwa wao ni wa wake wengi kwa asili. lakini nadhani ni sahihi zaidi ikiwa maneno haya yatatumika pia kumaanisha wanaume wenye tabia hizo.

  bahati mbaya katika miaka ya karibuni maana ya maneno hayo imetoka katika asili(sijui kama ndiyo kukua kwa lugha au laa), bali hata mtu mfano mwanasiasa ambaye hatulii na chama kimoja, mwenye kuhama vyama kama nyumba za kupanga, amekuwa akiitwa malaya.

  haya maneno yameanza kupotea taratibu na imebaki kuwa ni misamiati inayotumiwa zaidi na wazee ambao kwa sababu zilizo wazi hawawezi kutumia lugha za msimu na hapa kwenye lugha za msimu ndiyo tunakuja kwenye maana ya neno kiruka njia.

  kiruka njia
  ni malaya au ukipenda kahaba. neno njia limetumika kumaanisha mtu mwenye kubadilisha njia kila mara, mfano unatoka magomeni kwenda kariakoo, leo unapita jangwani-fire-kkoo, kesho unapita jangwani-fire-bibi titi road-uhuru road-msimbazi roda-kkoo n.k. kiruka njia ni neno la msimu au kwa kiswahili cha wengi hasa vijana ni neno la mtaani. wakati jamii inaona ni sawa kubadilisha njia inapobidi lakini haikubaliani na fikra ya kubadilisha wenza mara kwa mara na ni kwa mantiki hiyo watu hao wanafananishwa na wabadilisha njia/viruka njia. Hata hivyo ni muhimu kujua pia kwamba asili ya lugha za msimu kama hii ni kujaribu kupunguza ukali wa maneno kwa kuficha maana halisi inayokusudiwa, inaitwa tafsida.

  mzinzi ni mtu muasherati. mtu mwenye kushiriki unyumba nje ya ndoa(kwa maana ya kwamba yeye hajaoa wala kuolewa). ilivyo ni kuwa kila malaya/kahaba ni mzinzi lakini si kila mzinzi ni malaya/kahaba. Mfano wa mahusiano ya ki-zinzi ni hii fesheni ya siku hizi ya mke na mume kuishi kinyumba kwa kisingizio cha kujuana tabia...hakika wanachoshiriki ni maisha ya uasherati, maisha ya uzinzi.

  natumai utanufaika walau kidogo.
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Kahaba ni yule anaejiuza kwa pesa tu. Kama halipwi hatowi mchezo.

  Malaya ni yule washawasha haijalishi analipwa au halipwi, yeye mradi afanye tu na yoyote na hawezi kujizuwia na malaya anaweza kuwa mwanamme au mwanamke
   
Loading...