Kahaba apewa kichapo kikali baada ya kunaswa akijuza jirani na msikiti

Status
Not open for further replies.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,477
33,440
[h=3][/h]


Kahaba mmoja alijikuta akiambulia kichapo kikali toka kwa vijana wa kiislamu baada ya kunaswa akijiuza karibu na msikiti wao.....

Tukio hilo lilishuhudiwa na wanahabari wetu majira ya usiku jirani na msikiti huo uliopo nyuma ya Corner Bar, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke huyo na wenzake walikamatwa na baadhi ya vijana waumini wa Kiislamu waliokerwa na kitendo cha wao kutoa huduma haramu ya ngono maeneo hayo.


Baada ya wenzake kufanikiwa kutoka nduki mwanamke huyo alishuhudiwa akila bakora kisha akapelekwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar akaunganishwa na wengine waliokamatwa usiku huo.

Ilielezwa kuwa wanawake hao wamekuwa wakiuza miili kwa wanaume karibu na msikiti huo na pembezoni mwa baa hiyo.

Ilisemekana kuwa kumekuwa na kawaida ya wanawake hao kusimama maeneo ya nyumba hiyo ya ibada na kufanya biashara hiyohuku wakichafua mazingira kwa kutupa ovyo kondomu na kujisaidia maeneo hayo.
Wakati mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.

Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.

“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.

Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia waandishi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

Habari zilizotufikia ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.


GPL


KAHABA APEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUNASWA AKIJUZA JIRANI NA MSIKITI - MPEKUZI HURU
 
Kwani waislam hawanunui makahaba ama wamewatandika kwa kuwa wanajiuza karibia na msikiti
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom