Kagoda wamerudisha fedha, bado mnataka kuwajua?

Mzee,

Uwezi kustua gari lilo-knock Engine. Hapo ndiyo mwisho wake! Kama pato linaruhusu nunua gari nyingine au vipi endelee kutembea kwa miguu mpaka sori za viatu siishe ebo!

Na kuendelea kutumia gari lililo choka gharama zake zitakuwa kubwa sana. Tupilia mbali nunua jingine
 
Manji alirudisha fedha kwa niabaya "Kagoda" akidai kuwa aliyehusika ni marehemu baba yake. Serikali ikapokea fedha hizo na kuzijumlisha kwenye ile jumla ya Rais.

a. Kama wamerudisha fedha na serikali imekubali kupokea kuna haja ya kujua nani alifanya kosa kweli?

b. Kama serikali imekubali kupokea fedha hizo ina maana imekubali maelezo ya Manji na hivyo "case closed"?

c. Kama fedha zilizochukuliwa kwa kiasi kikubwa ndizo zilizotumika kumuingiza JK madarakani na sasa kazirudisha bado mnataka kumbana?

d. Rostam ndiye aliyehusika na kutumiwa kama alivyohusika kwenye Dowans na kutumiwa kwanini ni nani anaweza kumnyoshea kidole wakati wao wanajua bila yeye wasingeweza kuingia madarakani? NI kweli huwezi kumgusa Rostam bila kugusa karibu nusu ya Wabunge na Rais na huwezi kumuachilia bila kuachikilia kesi kadhaa za kifisadi! So what do you do?

e. Je kwa kujaribu kujifanya wanaichunguza Kagoda wakati tayari wanajua ni nani (ni wao wenyewe!) kwanini wasije tu na kusema mbele ya wananchi kuwa "Kagoda ndiyo sisi! hatukujijua na tumegundua kuwa tulikuwa tumezichota wakati tumelala, lakini tumezirudisha yaishe"!? vinginevyo kwanini wanajifanya kana kwamba hawajui Kagoda ni nani wakati wamepokea fedha kutoka kwake!?

f. Je wananchi wanasababu yoyote ya kujua Kagoda ni hata kama wamesharudisha fedha na fedha zishaliwa? Manake hawawezi kumkamata Manji (aliyerudisha) wala Rostam (aliyechukua kwa kutumia vyombo vyake kwa niaba yake na ya chama chake (hakufanya kama charity work!)

g. Sasa kwanini DPP asije tu na kusema kuwa hili haliwezi (kwani linamgusa Rais moja kwa moja!).

h. Kwanini Wabunge na watu mashuhuri ndani ya CCM au wana CCM hawaandamani kutaka Kagoda ifiikishwe mahakamani na wahusika wote wafikishwe mahakamani kama wanavyoshangilia kina Mramba kufikishwa mahakamani. Je mtu anaweza kuufikisha mkono wake wa kushoto mahakamani bila ye yeye mwenyewe kuwa huko huko mahakamani?

La Kagoda tulimalize vipi baada ya kujua kuwa fedha zimerudishwa, wezi wanajulikana, zilipita wapi inajulikana na zirudi nchini kwa namna gani inajulikana?

well... I was just thinking out loud. Nauliza nilivyowahi kuuliza huko nyuma kwenye hili la Kagoda tukubali yaishe? Au tuendelee kugangamala huku tukijua "haliwaki" hata tulisukume na "kushtua"?

Wanasema hakuna ushahidi...So what to do ni kutoa ushahidi utakaoweza kuwafikisha mahakamani,zaidi ya hapo wataendeleza siasa hapa, na wakifanya hivyo tuombe wananchi waamini kuwa ni kweli kuna mfisadi wasiofaa kuiongoza nchi yetu na wananchi wakiamini then ni mapinduzi.
Kama wananchi wameendelea kulala,then wazalendo walioko kwenye nafasi za kuhakikisha haki inatendeka na kuisambaratisha ccm na ngome yake ya mafisadi.
 
ni kweli. kama tukipata mabadiliko katka uongoz wa nchi hii na tukapata watu wenye 'integrity' na tume ikiundwa inaweza kutusaidia sana.

kwasasa dalili nyingi zinaonyesha jmk ataendelea mpaka 2010 na mpaka 2015.
halafu baada ya hapo 'mafisadi' watafanya juu chini raisi na wabunge wake wapatikane kwa njia za ovyo ovyo ili waogope kuwabana mafisadi kwani nao watakuwa hawakupata nafasi zao kwa taratibu zinazotakiwa.

hebu chukulia hata jkm akiishia 2010 lakin mafisad waki mfinance mtu wao na akawa raisi. wanaweza hata kucheza rafu staili ya zamani. wana sababu zote za kufanya hivyo. kwa hiyo hata miaka ijayo tunaweza kuwa na raisi na wabunge waliopatikana kwa hila. viongoz kama hawa hawawez kuwa na kauli dhidi ya mafisadi

tutaepukaje kupata viongozi kwa njia za ovyo kesho?
 
Tatizo siyo kwamba ndoto haitimiliki, watu wamepeleka mtu mwezini itakuwa kuiondoa CCM katika nchi yenye umasikini kama Tanzania? Tatizo strategy hamna, hamna upinzani, watu hawajaelimika, umasikini umetawala mpaka inatisha, hata alternative ya kuchukua nchi hamna, haya ndiyo matatizo.kwa hiyo lets focus kujenga a strong opposition CCM inatusaidia yenyewe kujiengua, otherwise tunacheza kama unavyosema.Lakini I would rather advance slowly than give up.

But strategically. If we decide today, I believe we CAN!

Kikwete anatolewa na ethical propaganda zitakazowafungua watu macho.Wapinzani wana mpango gani wa kuanzisha vituo vya televisheni vya kanda na kuonyesha TV bure kwenye public places? Vipi kuhusu vijarida? Vipi kuhusu kufanya a permanent campaign ambayo ina lengo la kuzidisha wanachama na wapiganaji wake vijijini? Vipi kuhusu kuwa na uongozi unao inspire watu? Vipi kuhusu kusambaza kanda za hotuba? Wapinzani wetu wanafanya yote wanayotakiwa? Vipi move ya kubadili katiba na kuwa na tume huru ya uchaguzi, sisikii kitu.Kuna mengi sana ya kuvalia njuga ambayo hayajafanywa kiasi siamini mtu akisema "regime change is out of the question" tatizo letu tuko softies, hatujui guerilla warfare, tumepewa uhuru on a silver platter, kutoka hapo tumekuwa bulldozed literally na Nyerere na hatukusema kitu.Too weak to act, too docile to protest, too quick to proclaim we can't.

Mbaya zaidi tunasumbuliwa na njaa ya siku moja! Hebu angalia watu kama Lamwai, Kabour, Mtemvu n.k. Hakuna anayefikiria kuwa unaweza kufa masikini lakini ukaacha watanzania wakiwa matajiri. Amini watakuenzi milele. Ila mbaya zaidi ni kwamba tunaendelea kushughulika na mamluki! Juzi nimepata habari za kushtua sana kwamba hata Lipumba ni mzee wa UWT. Kama ni kweli basi kazi ipo!
 
kama kweli zile hela zilitumika kwenye uchaguzi kuisaidia ccm ishinde basi kuna uwezekano mkubwa wabunge tulionao wengi wa ccm hawakustahili kuwa wabunge. huenda hata jmk hakustahili ushindi wa kishindo

raisi na wabunge wake wanaweza kuona ni vigumu sana kuachia madaraka kwasasa.

lakini lazima waone umuhimu wa kuzuia mambo kama yale kutokea miaka ijayo. hii ifanyike kwa ccm kutuomba msamaha. waseme kiasi cha pesa kilichochukuliwa, kiasi gani kiligharamia nini au mbunge yupi na kiasi gani kilitumika kugharamia ushindi wa raisi.

wakishamiliza watuambie wanafanya nini au wamefanya nini kuhakikisha miaka ijayo watakuwa hawajichukulii hela watakavyo. pia watuambie mipango yao ya kutafuta hela za kugharamia chaguzi zao. wasipokuwa na mipango mizuri na endelevu ya kutafuta hela wataendelea kutuibia
 
Mwanakijiji,

Majibu kwa maswali yako hayawezi kupatikana au kuleta maana ikiwa CCM bado itaendelea kuwa madarakani.

CCM wamenufaika ama kwa kudhamiria/kujua au bila kudhamiria/kutokujua, kwa kipindi kirefu kwa matumizi ya pesa ambazo hazikupata kihalali au zilitumika isivyopaswa.

Mfano, kama Kagoda walikopa hizo pesa wakadanganya wanazitumia kulipia malighafi lakini wakazipeleka CCM, basi ni dhahiri mkopo ulichukuliwa kwa ulaghai. Swali ni wapi Kagoda walipata pesa kurudisha deni lao? Je ni mkopo mwingine wa Mradi wa kuzindika umeme au ni pesa za uhalifu kama madawa ya kulevya na hongo ya kuingia mikataba isiyo na manufaa kwa Taifa?

Sikubaliani na FMES katika majibu yake kwenye hoja moja kuwa CCM ina watu wachache wabovu. kama ni wachache, kwa nini bado wako ndani ya Chama chenye wanachama milioni 5? Iweje watu 100 au tuseme 10000 ambao ni wabovu katika CCM wawe na nguvu na sauti kubwa na yenye maamuzi makubwa kuliko wanachama 4,990,000 !

Kama hawa wachache wanaendelea kuwa na nguvu na kunufaika kwa kuliingiza taifa letu hasara, basi ni wazi hao waliowengi wameridhika na maovu ya wenzao wachache na ndio maana hawataki kusimama na kuwaondoa kutoka chama chao.

Jibu ni moja kwa Tanzania kuweza kuendelea na kuwa na mazingira ya demokrasia ya kweli, uwajibikaji, uadilifu na haki yanayoambatana na Utawala bora, Uongozi bora na Siasa safi, nalo ni kuiondoa CCM madarakani.
 
Kweli kabisa Bwana Mchungaji. Kwa miaka kibao mimi nimekuwa nikilisema hilo na baadhi ya watu kunipinga. These guys (CCM) need to go. Kutegemea kuona mabadiliko kutoka kwenye chama kile kile tokea uhuru ni kuota njozi tu.
 
kama kweli zile hela zilitumika kwenye uchaguzi kuisaidia ccm ishinde basi kuna uwezekano mkubwa wabunge tulionao wengi wa ccm hawakustahili kuwa wabunge. huenda hata jmk hakustahili ushindi wa kishindo

raisi na wabunge wake wanaweza kuona ni vigumu sana kuachia madaraka kwasasa.

lakini lazima waone umuhimu wa kuzuia mambo kama yale kutokea miaka ijayo. hii ifanyike kwa ccm kutuomba msamaha. waseme kiasi cha pesa kilichochukuliwa, kiasi gani kiligharamia nini au mbunge yupi na kiasi gani kilitumika kugharamia ushindi wa raisi.

wakishamiliza watuambie wanafanya nini au wamefanya nini kuhakikisha miaka ijayo watakuwa hawajichukulii hela watakavyo. pia watuambie mipango yao ya kutafuta hela za kugharamia chaguzi zao.
wasipokuwa na mipango mizuri na endelevu ya kutafuta hela wataendelea kutuibia

Kwani CCM wamebadili mipango yao ya kutawala milele? Kama bado wanayo basi hayo yote ni wish list kama ahadi za JK wakati wa kampeni!!:rolleyes:
 
Wakushukuriwa ni Mzee Ali hassan mwinyi kwa kuliuwa Azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar Athari zake zinaendelea kuteketeza TANZANIA
 
MKJJ naomba ulifikirie hili kwa makini
kama unavyosema hizo hela zimetumika katika kampeni CCM, inamaanisha zimetumika hazikuwekwa benki ili zizae riba.

swali gumu, wamepata wapi hizo hela nyingine za kurudisha?

CCM/manji/ra/kagoda wamepata wapi $30m walizorudisha?
ku raise $30m in TZ sio mchezo?

Nakukatalia hela haijarudishwa zimechukuliwa sehemu moja zikapelekwa kwingine wazungu wanakuambia "creative accounting"

"MKJJ umezungushwa kwenye roundabout ya samora"

mtihani, hela iliyorudishwa imetoka wapi? shimo limeachwa wapi?
maana yake hela yote ilitumika katika kampeni...

mchana mwema....

Mkjj, hakuna hata senti moja iliyorudishwa hili ni changa la macho tu kutaka kujisafisha kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao, kama imerudi basi wamechukua hazina...wamekupua hazina maana kuchukua ni neno ambalo halionyeshi hali halisi. Huwaoni hadi hii leo wamekuwa mabubu kutoa details za tarehe iliyorudishwa pesa hiyo na iliwekwa katika bank ipi na account number ipi. Sasa kwa kuwa hawana hizo info wameamua kuwa mabubu. Wizi mtupu!!!!! :(
 
Haitoshi kunuia na kutamania. Haitoshi kusema CCM iondoke au iondolewe; haitoshi kuombea kuwa CCM ibadilishwe na uje utawala mwingine. Let me do some reality check:

a. Chama kikuu cha upinzani Tanzania hakina Mbunge hata mmoja Tanzania bara licha ya mabilioni ya fedha. Na uchaguzi mdogo wa Geita huko wala msitarajie kupata chochote.

b. Chama kikuu cha upinzani tanzania bara hakina mbunge hata mmoja Tanzania Visiwani na kwa muda kimekuwa na matatizo yake ya ndani.

c. CCM bado inapata wanachama wengi wa kutosha kubadili matokeo yoyote ya uchaguzi. Na wanaendelea kuandikisha wanachama wapya na sitoshangaa tunapoelekea uchaguzi hata baadhi ya waliokuwa upinzani watahama na kurudi CCM! Wapinzani wamepewa miaka miwili ya kupata wanachama wapya hadi leo wameshindwa hata kuanzisha matawi nje ya nchi wakati CCM inaendelea kama kawaida! Wamepewa nafasi tatu za kihistoria za kuingiza wanachama wengi lakini wameshindwa kuzitumia na wamebakia "maslahi ya taifa". Gharama yake ni kushindwa uchaguzi mkuu ujayo may be not to the same extend kama 2005.

d. CCM bado ina miundo mbinu na nyenzo nyingi za kutosha na mitandao yake ya kisiasa ni imara zaidi na mara nyingi zaidi kuliko chama kingine chochote kile.

e. Kuombea kuwa mabadiliko ya kisheria yafanyike, Katiba ibadilishwe ili x, na y yatokea maana yake ni kukiomba chama chenye wabunge wengi zaidi na kilichoshikilia serikali kibadilishe sheria za mchezo ili timu nyingine ishindwe! Ni sawa na kumwambia papa atoe mafuta yake halafu ayaweke kikaangoni huku yeye mwenyewe akifuatia! CCM imejifunza vizuri kutoka Zambia na Kenya na hata Malawi na haitafanya kosa hilo.

f. Bila kashfa upinzani Tanzania unakufa.
 
Katiba ya nchi hii inawalinda viongozi sio wananchi. Ndiyo maana viongozi wetu hawako tayari kubadilisha katiba. Kwa mfano rais ana madaraka makubwa mno ambayo katiba imempa kiasi kwamba anayatumia vibaya. Tukibadili katiba (viongozi walio madarakani hawapendi) tutafanikiwa kukomesha uchafu unaojitokeza kila siku. Je tuna uwezo wa kudai katiba mpya? Je tufanye nini ili watawala wetu watoe mwanya wakutunga katiba mpya?
 
TANNZAANIIA TANZANIA..NAKUPENDA KWA MOYO WOTE..NCHI YANGU TANZANIAAAAAA, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
PESAAAA ZAKO TANZANIAAA NI ZA WACHACHE TANZANIA, KAMA VILE KAGODA TANZANIA.
NIKUONAPO TANZANIA, MOYO WANIUM TANZANIAAA
TANZANIA TANZANIA, NITABEBA BOKSI MPAKA KUFAAA..
ILI TANZANIA, NISIKAMATWE NA MAFISADI..

IKOOO SIKU TANZANIA, MWANAKIJIJI ATAWATOA AIBUUU..
NAO WENGINE TANZANIA, HAPA JF WATAJIUNGAAAAA...
TUKUKOMBOE TANZANIAAAA, TOKA MIKONONI MWA MAFISADIIII..

(RUDIA KIBWAGIZO MARA 2)

By the way kama kuna mtu anatengeneza beats namtafuta tutoe hii single :)
 
Mimi nataka Serekali ikemee mahovu haya ya Kagoda na iweke wazi jinsi gani hatua zimechukuliwa kuhakikisha halitokei tena.
 
But strategically. If we decide today, I believe we CAN!

Mbaya zaidi tunasumbuliwa na njaa ya siku moja! Hebu angalia watu kama Lamwai, Kabour, Mtemvu n.k. Hakuna anayefikiria kuwa unaweza kufa masikini lakini ukaacha watanzania wakiwa matajiri. Amini watakuenzi milele. Ila mbaya zaidi ni kwamba tunaendelea kushughulika na mamluki! Juzi nimepata habari za kushtua sana kwamba hata Lipumba ni mzee wa UWT. Kama ni kweli basi kazi ipo!

Of all people Mtemvu amerudi CCM, mtu huyu ambaye jina lake liko deeply rooted katika opposition politics (I am talking the original opposition parties in the 60s, before multiparty politics was banned, I am talking chama cha Congress, ANC ya Tanzania, such legacy ya opposition!)

Inahudhunisha.
 
Last edited:
Ndiyo ninayoyasema haya; siyo kwamba sitamani mnachotamani. Swali ni jinsi gani tusababishe mabadiliko tuyatakayo kwa muda mfupi zaidi lakini kwa ufanisi zaidi na katika kufanya hivyo bila kuwashirikisha CCM (maana ndiyo tunataka waondoke so hawawezi kuwa sehemu ya huo mchakato).
 
Haitoshi kunuia na kutamania. Haitoshi kusema CCM iondoke au iondolewe; haitoshi kuombea kuwa CCM ibadilishwe na uje utawala mwingine. Let me do some reality check:

a. Chama kikuu cha upinzani Tanzania hakina Mbunge hata mmoja Tanzania bara licha ya mabilioni ya fedha. Na uchaguzi mdogo wa Geita huko wala msitarajie kupata chochote.

b. Chama kikuu cha upinzani tanzania bara hakina mbunge hata mmoja Tanzania Visiwani na kwa muda kimekuwa na matatizo yake ya ndani.

c. CCM bado inapata wanachama wengi wa kutosha kubadili matokeo yoyote ya uchaguzi. Na wanaendelea kuandikisha wanachama wapya na sitoshangaa tunapoelekea uchaguzi hata baadhi ya waliokuwa upinzani watahama na kurudi CCM! Wapinzani wamepewa miaka miwili ya kupata wanachama wapya hadi leo wameshindwa hata kuanzisha matawi nje ya nchi wakati CCM inaendelea kama kawaida! Wamepewa nafasi tatu za kihistoria za kuingiza wanachama wengi lakini wameshindwa kuzitumia na wamebakia "maslahi ya taifa". Gharama yake ni kushindwa uchaguzi mkuu ujayo may be not to the same extend kama 2005.

d. CCM bado ina miundo mbinu na nyenzo nyingi za kutosha na mitandao yake ya kisiasa ni imara zaidi na mara nyingi zaidi kuliko chama kingine chochote kile.

e. Kuombea kuwa mabadiliko ya kisheria yafanyike, Katiba ibadilishwe ili x, na y yatokea maana yake ni kukiomba chama chenye wabunge wengi zaidi na kilichoshikilia serikali kibadilishe sheria za mchezo ili timu nyingine ishindwe! Ni sawa na kumwambia papa atoe mafuta yake halafu ayaweke kikaangoni huku yeye mwenyewe akifuatia! CCM imejifunza vizuri kutoka Zambia na Kenya na hata Malawi na haitafanya kosa hilo.

f. Bila kashfa upinzani Tanzania unakufa.

Which means nothing will ever be resolved until CCM is out, even if it will take us 100 years!
 
Which means nothing will ever be resolved until CCM is out, even if it will take us 100 years!

Mchungaji, if you are a betting man, don't bet on that.. watoto wa watoto wao na wajukukuu wa wajukuu zao watakuwa madarakani na wataendelea kutamani vile vile tunavyotamani sisi.
 
Mchungaji, if you are a betting man, don't bet on that.. watoto wa watoto wao na wajukukuu wa wajukuu zao watakuwa madarakani na wataendelea kutamani vile vile tunavyotamani sisi.

Thelaw of entropy does not support that, when the Portuguese were in Mozambique and FRELIMO was fighting for independence, the Portuguese told them it would take the Mozambicans 500 years to get independence.

Wamarekani walivyokuwa wanaanza vita vya ukombozi dhidi ya the mighty British Empire hawakuwa hata na Jeshi la maana (David McCullough 1776) walikuwa hata hawajiamini, walikuwa na ragtag soldiers, walikuwa na mgawanyiko, lakini walijitosa katika vita, wakaji organize, wakamtoa mkoloni.Napenda kuurudia mfano wa ufalme wa Uingereza kwa sababu kuna parallel ya cabal like monopoly on power on both sides.

Juzi juzi tu hapa in the mid eighties watu tulikuwa tunafikiri multiparty politics would take a century or so, if viable at all.Angalia ilivyokuja kama manna kutoka angani.

I agree under the existing conditions kuiondoa CCM ni vigumu, lakini we cannot give up, we have to build a network from the ground up, we have to embolden an alternate government.

Kusema haiwezekani kuiondoa CCM ni defeatist attitude, sababu pekee ya kutufanya tusiweze kuwaondoa CCM ni kwa vile hatujajiandaa vilivyo, sio kwa sababu CCM is all that invincible.
 
Back
Top Bottom