Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani!

Discussion in 'Great Thinkers' started by Pascal Mayalla, Sep 2, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Pamoja na kupatikana ushahidi inaomuhusisha Rostam na Manji kwenye sakata la Kagoda ulioibuliwa na Msemakweli,

  Kagoda bado haitafikishwa mahakama kwa sababu....

  Alichokifanya Msemakweli ni kufuatilia procedures tangu za usajili wa Kagoda, asili ya jina, pesa zilichotwa lini na zikaingizwa wapi.

  Ambacho hakuweza kubaini ni fedha hizo zilifanya nini, yeye anaamini zilitoroshewa nje ya nchi kupitia duka fulani la kuuza fedha za kigeni.

  Kitu ambacho Msemakweli hakuweza kubaini ni the motive behind fedha za Kagoda na the real main players. Hao wote aliyowataja ni proins tuu kwenye hii game ya chess wahusika wakuu wote wako pembeni na hakuweza kuwabaini.

  Kwa wenye kumbukumbu watakumbuka Mama Meghji aliliambia nini Bunge letu pale Dodoma. Mama Meghji alikiri kuwa she was duped na waliomdupe sio Rostam wala Manji!. Tena alisema alinyanyua simu kuongea na wakuu wakamthibitishia hizo fedha ni kweli zinahitajika kwa madhumuni yaliyotajwa hivyo akaidhinisha!. Hii part Msemakweli haijui kwa vile kwenye maandishi haionekani popote.

  Msemakweli ameishia kwenye handling of transactions tuu na sio kwenye end use.

  Ile kamati ya uchunguzi inayajua yote aliyoyasema Msemakweli ila pia inajua the end use ya hizo fedha and as a result, Kagoda haitafikishwa mahakamani hata mara moja labda baada ya 2015 only if...siyo CCM tena!....
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pasco u r right lakini alichofanya Msemakweli kinapaswa kufanywa na any concerned citizens!!!!!! DPP alituambia hana ushahidi wa kutosha ku-prosecute hiyo Kagoda as if ni kampuni from the moon or Mars.

  Sasa Msemakweli amempa hizo docs and it 's in recordz kinachotakiwa sasa Feleshi awaambie watanzania hayo uliyoyasema hapo juu au achukue hatua and him too will be in recordz! Well he has an option for the easy one "USHAHIDI HAUTOSHI" lakini make no mistake naye hapo atakuwa ameingia rasmi kwamba ni mtetezi wa Kagoda.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nyambala, kutokufikishwa kwa Kagoda mahakamani hakutokani na kutotosheza kwa ushahidi bali lack of political will to prosecute kwa sababu wanawajua the true benefisharies wa fedha za Kagoda. DPP hawezi kukata tawi la mti alioukalia!.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pasco,

  Katika issue ya Kagoda hakuna kitu kinachoitwa political will. Hii inakuja endapo unaongelea suala ambalo serikali (Rais na watu wake muhimu) haina maslahi ila inasita kutekeleza. Lakini suala la Kagoda linaihusu serikali yenyewe na CCM na kwa hiyo hakuna mtu ndani ya hiyo serikali anayeweza kusimama akachukua hatua. Ni sawa na kunyoosha mkono wako wa kulia ukashika bastola ili ulipue mkono wa kushoto....Kwa akili ya kawaida haiwezekani kabisa...ni jambo ambalo linafanywa na kichaa!

  Hata hivyo nakubaliana na wewe kwamba mambo yote ya EPA na ufisadi mwingine wowote utaweza kutua mahakamani endapo CCM itakuwa haina tena nasaba na dola...iwe 2015 au baada ya hapo. Na hicho ndicho kinachoifanya CCM itumie kila mbinu (mf. ..kutishia raia kwa kutumia JWTZ ...akina Shimbo) kubaki madarakani.

  Hivi raia wa kawaida hawaruhusiwi kufungua kesi ya namna hii katika mahakama zetu????
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Dark City, sheria ya private prosecution ipo, ila one has to seek leave from DPP ndipo aweze kuendesha mashitaka. DPP akigoma kuwa hapo hakuna kesi, ni hakuna kesi kweli, sheria imempa DPP madaraka makubwa ya ajabu and there is no one to query.

  Kwa maoni yangu, baada ya madaraka ya rais, wa pili kwa madaraka sio spika wa bunge, wala sio jaji mkuu bali ni DPP. Huyu ana powers nyingine kubwa kabisa kuliko rais, kuliko jaji mkuu, kuliko mahakama yoyote, hii ni ile power ya 'Nolle Proseque' hizi ni nguvu za kuingilia kesi yoyote, ikiwa katika hatua yoyote, DPP anauwezo wa kuifuta bila kulazimika kutoa maelezo yoyote, bila kuhojiwa na yoyote.

  Ni kwa kutumia nguvu hizi kuzuia kesi ya Kagoda, hata kama private prosecutor ataomba kibali kuendesha mashitaka haya, DPP hatatoa kibali, maana kwake Kagoda haina kesi!.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mhhh,

  Hivi waliompa DPP madaraka makubwa namna hiyo walikuwa wanafikiri vizuri au nao ni wadau wa Meya wa jiji lenu ya Dar???

  Kwani kwa mujibu wa katiba, haiwezekana kufungua kesi ya kuomba mahakama kuu ipunguze madaraka ya DPP kwa vile yanapingana na misingi muhimu ya haki za binadamu???
   
 7. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu sheria hiyo ilipitishwa na bunge na wanajua waliompa DPP madaraka makubwa kiasi hicho ambayo hayahojiwi na mtu yoyote yeye akishaamua
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Dark City, hapa kwetu tuna mihimili mitatu mikuu ya dola, Serikali (The Executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary) ambavyo vyombo vyote hivi vitatu, vinatakiwa kufanya kazi kwa uhuru na mamlaka yake kamili bila kuingiliana (Principle of Separation of Powers), na wakati huo huo kila kimoja kikihakikisha kingine kisiende nje ya mamlaka yake, (checks and balance).

  Vyombo vyote hivi, vimepata mamlaka yake ndani ya katiba, hivyo huwezi kuitumia katiba hiyo hiyo kupunguza mamlaka ya chochote kati yake isipokuwa ni kufanya mabadiliko ya katiba. Mamlaka hayo makubwa na ya ajabu ya DPP amepewa na katiba, sio bunge wala mahakama zinaweza kuyapunguza, isipokuwa ni katiba hiyo hiyo, ndio maana pia tuna kilio kikubwa kuhusu mamlaka kubwa kupita kiasi aliyonayo rais wetu kwa mujibu wa katiba, yaani tunaongozwa na rais mwenye mamlaka ya kufanya anavyopenda.

  Lets hope katiba mpya itayapunguza sio tuu mamlaka ya kimungu mtu ya rais wetu na haya ya DPP ili tufike mahali, kama kuna solid evidence kuhusu jinai fulani kutendeka, DPP alazimishwe kufungua kesi, na hata ile mamlaka yake ya Nolle Proseque pia alazimishwe kutoa sababu, sio hali ilivyo sasa, hata ushahidi wa 100% ukipatikana kuhusu Kagoda, akiamua hafungui kesi na hakuna wa kumuuliza kwanini.
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza kufafanua hii sentensi hasa hapo kwenye red? What exactly do you mean by "motive behind fedha za Kagoda"? Nakumbuka niliiona hii post yako kwenye ile thread kuu (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/168829-nyaraka-mpya-za-kagoda-zawalipua-rostam-manji-18.html) post namba 347. Nilitaka nikuulize swali moja lakini nikakuta Mwanakijiji alishakuuliza kwenye post number 347: "Pasco, ili uweze uwe wizi ni lazima ujue fedha zilizoibwa zimetumika vipi? Je sheria ya Anti-money laundering inajali zilizotumwa zimetumika vipi?"

  Sasa badala ya kumjibu kwenye ile thread ukasepa. Ulichofanya ni ku copy post yako kwenye ile thread kuu na kuja kui-paste hapa kuazisha thread mpya. Kwa hiyo unataka na watu waliokuuliza maswali kwenye ile thread kuu kama akina Mwanakijiji nao wahamishe maswali waliyokuuliza kwenye hii thread? Na wengine wakinzisha thread mpya kwa ku copy na ku paste walichopost kwenye thread ile itakuwaje?

  Umenikumbusha kuna mdau mmoja alikuwa anaazisha thread juu ya mitazamo yake binafisi kwenye suala fulani wakati kuna thread inayojadili exactly the same thing. Mkuu sijaelewa kabisa "motive yako behind hii thread." Labda utufafanulie.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  EMT, kwanza asante kunikumbusha hivyo hoja nimesha zijibu.

  Motive ya thread hii ni kutofikishwa mahakamani kwa kesi ya Kagoda. Main thread ilihusu ushahidi mpya hivyo kujenga matumaini ya wengi kuwa sasa hatimaye Kagoda itatinga mahakamani. Ile thread ya msingi ni informative hii ya kwangu ni debatable na kuna nyingine ya Mzee Mwanakijiji akimtaka DPP kufungua mashitaka ya Kagoda na naamini nyingi nyingine zitafuatia.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Pasco kwa ufafanunuzi wako mzuri na wa kitaalamu.

  Binafsi bado naamini wananchi kwa umoja wao mmoja mmoja wanaweza kwenda mahakamani kuhoji kifungu cha katiba kama kinachukua uhuru wao wa kutendewa haki wakati kuna vifungu vingine vya katiba hiyo hiyo vinavyowapa uhuru huo!

  Labda ni umbumbu wangu lakini nahisi kama hilo linawezekana. Au ni ndoto tu!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kwa maelezo yako ndugu Pasco na kwa kuangalia utendaji wa hii serikali na ushiriki wake katika Rushw kubwa na ufisadi, nakubaliana na wewe kwamba Kagoda haiwezi kushitakiwa...na Kama alivyosema Pinda haikamatiki...Na pia kesi zote ambazo serikali inahusishwa kama Meremeta zitaendelea kuimbwa tu kama mashairi ya kwenye text books!!

  But.....Siku CCM ikiondoka madarakani patachimbika.....Kama wana akili (mafisadi wote na makuwadi wao) basi wahakikishe CCM inatawala milele!!
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hapa umesema sawia kabisa.
  Msemakweli ameonyesha kuwa kagoda ni kampuni yenye wakurugenzi wanaojulikana, ameonyesha kuwa imechukua fedha kutoka bank kuu akaunti ya madeni ya nje EPA, na kwamba fedha hizo zinaonyesha kutoka kwenye acounts za KGODA.

  Issue hapa sio, zilitoka kwenda wapi, bali Kadoga ili-forge documents na kujipatia fedha ....WALIIBA. walifanyia nini, walipeleka wapi fedha hizo sio issue. ushahidi ukionyesha umeiba kuku, haijalishi kama huyo kuku ulimla supu au ulimuuza kwa mama nyambilee.

  However, issue hapa ni kuwa-implicate hawa ma-king makers!! Rostam na Manji. Hapa kwa hawa wajamaa, ndipo panapohitaji political will, hapa ndipo panapohitaji mkono wa mkuu wa nchi, ambao kwa sasa, tusitegemee ukawepo..........lets hope for 2015......hope for change.

  otherwise..........we are F big time.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  CCM imejiandaa kutawala milele by hooks and crooks. Na kwa vile level ya awareness kwa waliowengi was low, CCM ikatake advantage ya uelewa duni huo kushinda chaguzi zote. Katika uchaguzi uliopita JK amepata kura milioni 4. Tovuti ya CCM inadai CCM ina wanachama milioni 4, hii inamaanisha wale wote ambao hawakupiga kura mwaka 2010, wakiamua kuivote out CCM, then 2015 CCM haina pa kutokea!.
   
 17. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Haya Mkuu. Now, what exactly do you mean by "motive behind fedha za Kagoda"?
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  EMT, motive behind fedha za Kagoda ndio sababu pekee inayopelekea Kagoda isishitakiwe. Hizo bilioni 40 za Kagoda zilifanya kazi fulani, fungu alilomega RA na fungu la Manji, walisharudisha ndio maana hawashitakiwa. Kumbuka ni kampuni 122 zilizochota EPA, wale wale waliorudisha, wamesamehewa na hawakushitakiwa, hata hao kina Jeethu na nduguye, walirudisha sum na wameshindwa kurudisha sum na kiasi hicho kidogo walichoshindwa kumalizia ndicho walichoshitakiwa nacho. Hii ya Kagoda ilienda kufanya kazi maalum, DPP Feleshi anaijua, ndio maana nikasisitiza, hawezi kulikata tawi alilokalia. Nakubalia na ile theory ya aliyekutwa na ngozi, ndio aliyekula nyama, kwenye Kagoda, hayo majina ya waliokutwa na ngozi ni maboya tuu, waliokula nyama ni wengine, DPP anawajua waliokula nyama, ndio maana hawezi kuwashitaki waiokutwa na ngozi, watawataja waliokula nyama na itakuwa soo.

  Hata BOT, hao washitakiwa ni makarani tuu, muidhinishaji ni mkurugenzi Peter Noni, fedha zilizorudishwa zimekabidhiwa TIB, Mkurugenzi muidhinishaji sasa ndie mkurugenzi mkuu TIB!.
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280

  DPP office has executed its duties diligently - AG

  26th August 2011


  The government has strongly defended the portfolio of the Directorate of Public Prosecutions (DPP)'s office, saying it has performed its duties diligently. Attorney General (AG) Judge Frederick Werema defended the portfolio of the DPP's office yesterday against allegations by Shadow Minister for Justice and Constitutional Affairs Tundu Lissu (Chadema) when he was presenting views of the opposition camp in Dodoma Wednesday. According to Lissu, the DPP's failure to take legal actions against some individuals, including government officials, involved in the misappropriation of public funds proved there was no need to retain the office.

  In his argument Lissu gave an example of a case of individuals involved in stealing money from the Bank of Tanzania ( BoT)'s External Payment Arrears (EPA) account, saying despite the outweighing evidence, some suspects had escaped the arm of the law. "The government has until today failed to take legal action against Kagoda Agricultural Limited, a company accused of pocketing over 40bn/- from the account on grounds of lack of evidence," he explained.

  Without mentioning the names of the culprits, Lissu also said the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB)'s and DPP's failure to institute legal actions against individuals involved in the controversial purchase of the military radar from BAE Systems, Dowans, Meremeta, TanGold and the privatisation of Kiwira Coal Mine raised doubts on constitutional powers bestowed upon the two organs. Lissu, in his speech, proposed for the establishment of a special court to look into the best way of removing the DPP from his office because of his unsatisfactory performance. He said such a court should be established by the president after being advised by the AG since the DDP had immunities and privileges bestowed upon him by the country's Constitution.

  Defending the DPP's office yesterday morning, Judge Werema said before filing any case in the court, the DPP had to gather satisfactory evidence so ensure the suspects' rights were not violated. According to Werema, out of the 30 files sent to the DPP of the cases involving high profile individuals, the DPP had given the green light to 13 cases after he went through the evidence and found it substantial and relevant. However, the AG could neither mention the cases nor the individuals involved.


  The Guardian
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Mwanzo nilisema kamwe haitafikishwa mahakamani, unless otherwise!, ile possibility ya otherwise sasa ndio ipo kiukweli kweli, hivyo wote wanaotaka kuiona Kagoda ikipandishwa kizimbani, tarehe 25 October, amueni!.

  Pasco
   
Loading...