Kagoda, EPA zatajwa muswada wa uchaguzi


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,347
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,347 280
Exuper Kachenje, Dodoma
SUALA la wizi wa fedha katika akaunti ya madeni ya nje (Epa), na Kagoda, jana liliibuka na kuzua zogo wakati kambi ya upinzani ilipokuwa ikitoa maoni yake kuhusu muswada wa sheria ya gharama za uchaguzi iliyowasilishwa bungeni na serikali jana mjini Dodoma.

Kuzuka kwa suala hilo kulifuatia kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria kuwasilisha maoni yake na ndipo Halima Mdee aliyesoma maoni ya kambi ya upinzani aliibua suala hilo.

Akisoma maoni hayo, Mdee alisema "Sote tulishuhudia jinsi ambavyo fedha za Epa(Bot) zaidi ya Sh 40 bilioni zilizochukuliwa na kampuni hewa ya Kagoda na fedha nyingine nyingi wa wafanyabiashara mbalimbali walio na wasio halali ndani na nje ya nchi zilivyofanikisha kwa kiasi kikubwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani,"alisema Mdee katika maoni ya kambi yake.

Kauli hiyo ya Mdee ilimfanya Dk Raphael Chegeni kuinuka na kusema, "Taarifa, mheshimiwa Spika."

Hali hiyo ilimfanya Mdee kusita kuendelea kusoma maoni hayo ndipo naibu Spika Anne Makinda aliyeongoza kikao hicho alipompa nafasi Chegeni ya kuzungumza ambaye naye alisema kuwa maneno ya Mdee hayana uhakika na ukweli wake una utata akitaka ayafute katika taarifa hiyo ya upinzani.

"Maneno anayosema mheshimiwa hayana uhakika na ukweli wake una utata ayaondoe," alisema Dk Chegeni na kauli yake kuungwa mkono na naibu Spika aliyemtaka Mdee kwenda kwenye hoja ya msingi na kuacha hoja hiyo aliyosema haina mantiki.

Hata hivyo Mdee alikataa kufuta maneno hayo huku akidai ni ya uhakika na yenye ushahidi unaoweza kuwasilishwa.

"Siwezi kuyaondoa kwa sababu nina hakika na ushahidi upo," alisema Mdee na kuendelea kusoma maoni hayo kwa niaba ya kambi yake.

Alisema kambi yake inatambua umuhimu wa uwepo wa sheria hiyo yenye lengo la kudhibiti matumizi ya fedha wakati wa kampeni, lakini upinzani ndiyo umekuwa mwaathirika mkuu wa fedha chafu na safi wakati wa uchaguzi na kubainisha kuwa ni wao kwa miaka mingi wamekuwa wakidai uwepo wa sheria hiyo.

Mdee alisema ingawa muswada huo unaelezwa kuwa na lengo la kudhibiti fedha chafu na haramu, lakini hakuna kipengele kinachoharamisha matumizi ya fedha zinazotokana na dawa za kulevya, kampuni za kigeni yaliyo ndani na nje ya nchi pamoja na zilizopatikana kiharamia na wizi wa fedha za umma.

Aliongeza kuwa muswada huo umewanyima fursa Watanzania wanachama wa vyama vya siasa kuchangia na kwamba pamoja na malengo yake kuzuia fedha za nje ili kuzuia ushawishi wa nje, muswada huo unatambua na kuhalalisha matumizi ya fedha hizo zinazoingizwa nchini siku 90 kabla ya uchaguzi.

"Jambo la msingi la kuhoji, kama kweli dhamira ni kuzuia fedha kutoka nje ili kuepuka ushawishi wa mataifa ya nje ama wachangiaji mmoja mmoja kutoka nje iweje leo kuwe na mipaka ya muda utakaozihalalisha fedha hizo, …Uharamia ni uharamia, haijalishi kama umefanyika usiku au mchana," alisema.

Muswada huo uliwasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo.

Akichangia muswada huo naibu kiongozi wa upinzani bungeni Dk Wilbroad Slaa alisema kambi ya upinzani inataka fedha zinazotumika katika uchaguzi zijulikane, fedha zote haramu zisiingie kwenye uchaguzi na zibainishwe wazi na sheria hiyo.

Katika mchango wake Fred Mpendazoe alishauri nguvu za msajili wa vyama zielekee katika kudhibiti matumizi ya fedha kwa vyama badala ya wagombe.

"Siku zote tunasema, chama legelege huzaa serikali legelege. Chama kisichokula rushwa hakizai serikali inayokula rushwa. Msisitizo wa kudhibiti rushwa uanzie kwenye siasa kwani chama kinachoingia madarakani kwa rushwa huzaa serikali inayokula rushwa," alionya Mpendazoe.
http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17900
 

Forum statistics

Threads 1,236,240
Members 475,029
Posts 29,251,215