Kagera: Waziri Ndalichako akagua ujenzi wa Chuo kipya cha VETA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekagua mradi wa ujenzi wa Chuo kipya cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) katika Mkoa wa Kagera.

Profesa Ndalichako amefanya ukaguzi huo Januari 9, 2021 wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo ambapo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi huo ambao umefikia asilimia 50.7 ili kukamilika na ubora wa majengo yanayojengwa katika eneo hilo.

Waziri Ndalichako amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema ili ifikapo mwezi wa nane mwaka huu uwe umekamilika.

"Kukamilika kwa mradi huu kutafanya Serikali iendelee kutimiza azma ya kuhakikisha inatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wengi zaidi wa Kitanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda.

Naye Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi nchini, Pancras Bujulu amemweleza Waziri Ndalichako kuwa utekelezaji wa ujenzi wa majengo umefikia asilimia 50.7 na kwamba majengo yote yamekamilika yakisubiri kazi ya uezekaji paa huku kazi ya kusawazisha ardhi na mazingira ikiendelea.

Bujulu amesema ujenzi wa wa chuo hicho unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu China kwa gharama ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 22.
IMG-20210109-WA0023.jpg
IMG-20210109-WA0022.jpg
IMG-20210109-WA0021.jpg
IMG-20210109-WA0020.jpg
IMG-20210109-WA0024.jpg
IMG-20210109-WA0025.jpg
 
Tunelipataga mtu msimamizi mzuri wa Matumizi ya fedha za serikali kama ilivyo leo Kwa Magufuli, tokea kipindi cha kina mwinyi Hadi leo, tungekuwa mbaaaaali Sana aisee
 
Tunelipataga mtu msimamizi mzuri wa Matumizi ya fedha za serikali kama ilivyo leo Kwa Magufuli, tokea kipindi cha kina mwinyi Hadi leo, tungekuwa mbaaaaali Sana aisee
Kati ya Nyerere na Magufuli nani ana uwezo mzuri wa kusimamia fedha za nchi?
Leo hii mishahara yao mikubwa, kununua wapinzani,magari ya kifahari,n.k
 
Juhudi kubwa ingeelekezwa kada hii.Masomo primary na sekondari olevel yaunganishwe, A level wachache na vyuo vikuu pia wachache.80% waende vyuo vya ufundi.Uchumi wetu utapaa haraka zaidi, tatizo la ajira litapungua kwa asilimia kubwa sana.
 
Kati ya Nyerere na Magufuli nani ana uwezo mzuri wa kusimamia fedha za nchi?
Leo hii mishahara yao mikubwa, kununua wapinzani,magari ya kifahari,n.k
Ukitoa jiwe ulilomeza kifuani kwako ndipo tuongee vizuri, kwa sasa siwezi kukujibu Maana jiwe limekukwama
 
Back
Top Bottom