KAGERA: Watuhumiwa wa ujambazai wauawa na Jeshi la Polisi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa mkoani Kagera baada ya majibizano ya risasi kati ya maofisa wa Jeshi la polisi wakiwa chini ya ulinzi wakati wakiwapeleka polisi kuonyesha walipoficha silaha .

Tukio hilo limetokea katika eneo la Kiraka cheusi ,kijiji cha Nyamalagala , tarafa ya Rusaunga wilayani Biharamulo.

Akielezea tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo kamishina msaidizi Revocatus Malimi ametaja majina ya watu hao waliouawa kuwa ni Shabani Magote, Erick Samson raia wa Burundi na mwingine jina lake halikufahamika.

Kamanda Malimi amesema maofisa hao wakiwa njiani kwenda kuonyeshwa eneo zilipofichwa silaha hiyo ghafla walianza kurushiwa risasi kutoka porini na polisi kujibu mashambulizi.

ITV
 
Mhh, kuwepo na independent commission kwa ajili ya kufanya uchunguzi kwenye mauaji ya "watuhumiwa" wa ujambazi.. Jeshi la Polisi Tanzania limepoteza credibility ya kuaminiwa kwa habari wanazozitoa.. Zinaacha maswali zaidi kuliko majibu..
 
Naamini kwa 95% hao wanaoitwa majambazi wakauwawa na polisi kwa risasi ni raia wema waliogoma kutoa Chochote. Hivyo polisi wamewaua na baadae kuwalable Kama majambazi. Askari polisi wanaotegemewa kuwalinda watu na Mali zao ndiyo majambazi wakubwa.
 
Kama askari wameonekana kang'ata watu, wanatukana watu matusi ya nguoni, wanawabaka watuhumiwa vituoni, wanafia baa kwa ulevi, wanabambika kesi za mauwaji kwa watu wema wanauwa wauza madin nk lweje tuamini haya mauwaji ya holela. Halafu wote wanauawa wakati wanakwenda kuonyesha walipo wenzao.... Sawa vyeo watapandishwa lkn ipo siku wakumbana na majambazi wa kweli na hali itakuwa mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipewa maagizo ya kuua ili wapande vyeo Police wa Tanzania wamelaaniwa kabisa, ila malipo ni hapa hapa Duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acheni kuongea msilo lijua ndugu zangu mkoa wa kagera wilaya ya bihalamlo na icho kijiji cha nyamalagala ndio point yao kuu hao walundi majambazi wanapitia apo kwaajili ya kuteka magari makubwa yanayo peleka mizigo lwanda naisi madeleva wanao peleka mizigo uko watakuwa mashahidi sana

Ni mwezi wa pili tu wametoka kuteka magari ya mizigo apo kichaka cheusi ilikuwa saa 12 asubuh but askar wanao kaa point apo ndio walikuwa wanafika walipo waona wakakimbia uku wakilusha lisasi na siku hiyo akuna jambaz wala askar alie jeruhiwa na ndio mpaka Jana iyo walipo dakwa Hawa wenzao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamanda Malimi amesema maofisa hao wakiwa njiani kwenda kuonyeshwa eneo zilipofichwa silaha hiyo ghafla walianza kurushiwa risasi kutoka porini na polisi kujibu mashambulizi.

Kwahiyo waliouawa ni wale wa porini au wale waliokuwa wanakwenda kuonyesha silaha!?

Yasijekuwa yaleyale yaliyotokea Tabora na Mawasiliano Dar
 
Kama askari wameonekana kang'ata watu, wanatukana watu matusi ya nguoni, wanawabaka watuhumiwa vituoni,

Wengi wao ni failures shuleni na vyuoni na wengine ni wale wanaotumia vyeti visivyo vyao, yawezekana hata akili siyo zao
 
ila matukio ya ujambazi zimepungua sana dar..... awamu iliyopita mliman city, ilikuwa balaaa
 
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa mkoani Kagera baada ya majibizano ya risasi kati ya maofisa wa Jeshi la polisi wakiwa chini ya ulinzi wakati wakiwapeleka polisi kuonyesha walipoficha silaha .
Kamanda Malimi amesema maofisa hao wakiwa njiani kwenda kuonyeshwa eneo zilipofichwa silaha hiyo ghafla walianza kurushiwa risasi kutoka porini na polisi kujibu mashambulizi.

ITV

Hii imenichanganya kidogo. Inamaana kuna wahalifu waliokuwa wamekamatwa, na walikubali kuwapeleka polisi wakawaoneshe silaha zipokuwa zimefichwa, na walipokuwa njiani wakashambuliwa toka porini.

Je waliouawa ni wale waliokuwa porini au wale waliokuwa wameambatana na askari.
Je hizo silaha zilipatikana au?
 
acheni kuongea msilo lijua ndugu zangu mkoa wa kagera wilaya ya bihalamlo na icho kijiji cha nyamalagala ndio point yao kuu hao walundi majambazi wanapitia apo kwaajili ya kuteka magari makubwa yanayo peleka mizigo lwanda naisi madeleva wanao peleka mizigo uko watakuwa mashahidi sana

Ni mwezi wa pili tu wametoka kuteka magari ya mizigo apo kichaka cheusi ilikuwa saa 12 asubuh but askar wanao kaa point apo ndio walikuwa wanafika walipo waona wakakimbia uku wakilusha lisasi na siku hiyo akuna jambaz wala askar alie jeruhiwa na ndio mpaka Jana iyo walipo dakwa Hawa wenzao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna jambazi mrundi au mnyarwanda eneo hilo acheni kusingizia wakimbizi walikwisharudishwa makwao na kudhibitiwa mipakani, siku hizi polisi ndio majambazi hili halina ubishi hata kidogo.
Juzi waliokuwa wanatorosha madini kwa kushirikiana na wahindi ni wanyarwanda au warundi wa wapi?
Polisi Tanzania wameua sana kwa maelekezo ya amiri jeshi wao haiwezikani awamu hii iliyojaa umasikini isiyo na tajiri hata mmoja ndio iwe na majambazi wengi wanaouawa na polisi kila siku!!
Jifunzeni kuangalia matukio kwa macho yenye fahamu.
 
Tangu tukio la wafanya biashara wa mahenge litokee, huwa siwaamini askari wa Tanzania na sita waamini.
 
Back
Top Bottom