Kagera: Ndugu watatu wadaiwa kumuua mama yao

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Polisi mkoani Kagera inawashikilia watu watatu wa familia moja kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya mama yao mzazi kwa kile kilichodaiwa walikuwa na ugomvi wa muda mrefu uliotokana na kumtuhumu kuwa mchawi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Tuntufye Mwakagamba amemtaja aliyeuawa kuwa ni Flazia Rukela mwenye umri wa miaka 99.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa leo Julai 10, 2021 amesema kuwa watoto hao Laurent Frances (60) na Alexasender Frances (55) pamoja na shemeji yao Agness Gidioni (70) wote wakazi wa Kijiji cha Nyabirungu wilayani Kyerwa, wanatuhumiwa kuhusika kwenye mauaji hayo.

Kamanda Mwakagamba amesema kuwa tukio hilo la mauaji limetokea Julai 7, 2021 katika Kijiji cha Mkombozi wakati Flazia akiwa amelala kwenye nyumba yake alivamiwa na watu wasiojulikana na kumkatakata kwa kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake.

Amesema mbali na kutekeleza mauaji hayo, watu hao pia walitenganisha sehemu mbalimbali za mwili wale na kuzitoa nje kisha kumtelekeza na kutokomea kusikojulikana.

Hata hivyo, Kamanda Mwakagamba ametaja sababu za kuwashikilia watoto wa marehemu kuwa ni kutokana na kuwepo kwa madai ya kuwepo kwa ugomvi wa muda mrefu na mama yao ambapo, wamekuwa wakimtuhumuwa kuwa ni mchawi.

Ameongeza kuwa, watoto hao wamekuwa wakimtuhumu mama yao kujihusisha na vitendo vya kishirikana na kwamba, amekuwa akiwaroga na familia zao hivyo kuamua kumtenga na kumuacha akiishi peke yake bila msaada.

“Kuna mtoto wa marehemu anaitwa Thomas Frances ambaye ndiye alikuwa akimhudumia mama yake, lakini aliachana na mkewe na siku hiyo alimtaka maneno kuwa, atakuja kufanya tukio ambalo halitasahaulika kwenye familia hiyo. Sasa tunamshikilia mke wa huyu Thomas kwa mahojiano zaidi.

“Pia, tunaomba mtu mwenye taarifa zaidi basi atusaidie ili kuhakikisha wahusika wote wanatiwa mbaroni na sheria kuchukua mkondo wake,” alisema Kamanda Mwakagamba.

Mwananchi
 
Hayo yote tatizo kuu ni umasikini na elimu duni, katika nchi yetu mtu anakaa na umasikini miaka 50 na zaidi anaanza kuamini kuna mkono wa mtu kumbe sio.
 
Hao wahaya wa kerwa wote ni wachawi na walikuja hapo kerwa kwa kufurushwa kutoka bukoba vijijini
 
Miaka 99? Mbona alibakisha padogo ili afe, wangemwacha tu ajifie mwenyewe kuliko kujichumia dhambi ya kuua. Sad news to wake up to
emoji17.png
 
Jamani ukiachwa achika, sio kuropoka ropoka. Sasa huyo mama kaponzwa na mdomo wake.
 
Back
Top Bottom