Kagera: Moto wa ajabu waibuka Mleba, Wakazi wazikimbia nyumba zao

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Wakazi wa Ibila Kagera wakimbia nyumba zao kuhofia kuungua moto ambao chanzo chake hakijulikani.
DC8BiN7W0AAXlrA.jpg

Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Ibila kilichoko katika kata ya Mayodwe iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera wameanza kuzikimbia nyumba zao za makazi kwa hofu, kufutia matukio ya mara kwa mara ya baadhi ya nyumba za wananchi katika kitongoji hicho kuendelea kuteketea na moto unaozuka ghafla majira ya mchana ambao hadi sasa chanzo chake hakujajulikana.

Moto huo unaoteketeza nyumba za makazi ulitokea kwa mara ya kwanza katika kitongoji hicho Mei 4, mwaka huu na hadi sasa umeishateketeza nyumba 12 za makazi ya wananchi ambao wanaishi katika mazingira magumu, wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeteketea na wale waliokimbia nyumba zao kutokana na hofu ya moto, wameyahusisha matukio hayo na masuala ya imani za kishirikina huku mmoja akieleze namna alivyoinusuru nyumba yake ambayo ilikuwa imeanza kuteketea usiku wa kuamkia.

Kufuatia matukio hayo ya moto mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango ambaye amekutana na viongozi wa madhehebu ya dini, waganga wa tiba za asili na wazee wa kilmila na kuzitembelea familia zilizoathirika na moto huo pamoja na kutoa maelekezo ya kukabiliana na moto huo amesikitishwa mtu mmoja ambaye baada ya nyumba yake kuanza kuteteketea kwa moto alifanya kazi ya kumnusurui mtoto wake aliyekuwa akiugulia ndani ya nyumba hiyo ambaye baadae alipata mshtuko na kufariki dunia.

Chanzo: ITV
 
MOTO UNAOZUKA MCHANA GHAFLA.CHANZO CHAKE HAKIJULIKANI.
ngoja nimalize kula futari yangu
 
Waache matambiko ya kishirikina. Wahaya nao hawajambo. What happens when you make a pact with devil?
 
Kama wana maujuzi hayo si wayatumie kwa aliyebugia rambirambi zao?
Waaya kwa sifa za hapa na pale hawajambo!!!
 
Majibu ya Kisayansi ya matukio ya mkoani Kagera

Moto wa ''ajabu'' unatua juu ya paa, ngurumo kama ya ndege inatua na moto unatoka angani na kutua tangu tarehe 4 May 2017.

  1. Matokeo ya matetemeko ya ardhi yaliyoikumba eneo hilo la Kaskazini Magharibi ya Tanzania na ukanda wa Ziwa kwa ujumla
  2. Pia inaweza kuwa dalili kuwa kuna tetemeko lingine la ardhi linaweza kutokea katika maeneo hayo ya kanda ya Ziwa (Victoria).
Wakati kipande kikubwa cha ardhi ya dunia katika eneo Fulani mfano mkoa wa Kagera kikiwa kina hama au kusuguana na kipande kingine cha ardhi basi hutokea miali ya mwanga (wa moto) kama wa radi usiokuwa na ngurumo. Miali hii ya mwanga ina uwezo wa kusababisha moto au mioto midogo midogo.

Miali/ Mwanga huu huwa unauwezo wa kuchoma nyumba, mazao na hata mwili wa mnyama au binadamu. Vilevile msuguano huu wa vipande vya vikubwa vya eneo la ardhi huja na ngurumo kama ndege inatua.

Matokeo mengine ya msuguano huu wa vipande vikubwa vya ardhi ya dunia ni kusababisha ghafla mto wa maji kutokea pale ambapo kulikuwa hapana mto au dalilli za mto. Pia kama upo jirani na Ziwa unaweza kuona kisiwa kimezuka toka chini ya kina cha maji sehemu ambayo kulikuwa hakuna dalili ya kisiwa kuwapo.

Dalili zingine za uwezekano wa tetemeko kutokea katika muda mfupi ujao ni binadamu kusikia pressure za miili yao inapanda, kuumwa kichwa au wanyama na mifugo kama kuku , bata n.k kuanza kuonesha dalili za kuweseka au kutaharuki bila dalili ya hatari kuonekana kwa macho.

Hii inatokana na viumbe miili yao kuhisi mabadiliko ya ghafla katika mazingira yao kama ukimya usio wa kawaida wa mazingira yao, nguvu ya electromagnetic signals zinazoletwa na msuguano wa kipande kikubwa cha ardhi ya dunia kusuguana na kusigana kabla au baada ya tetemeko la ardhi.

Mwisho msuguano huu wa vipande vikubwa vya ardhi ya dunia inaweza kuwasabisha miale hiyo ya moto bila tetemeko kutokea kwa vile eneo hilo la dunia baada ya tetemeko linakuwa linajiweka sawa (ji-balance) baada ya mfululizo wa matetemeko yaliyofanya eneo hilo kubakia katika hali isyo sawa.

Hii ya moto kuunguza nyumba na migomba tu vipi??

Source: Millard Ayo

Electromagnetic signals “can predict earthquakes”
By David Appell
Strange electromagnetic signals were detected two months before a major earthquake hit Japan. The signals support controversial work by Greek researchers, who say they could one day be used to predict earthquakes. Read more: Electromagnetic signals “can predict earthquakes”

Bizarre Earthquake Lights Finally Explained

Historic Sightings

Over the centuries, there have been many reports of earthquake lights, both before and while the ground is shaking.

Just seconds before the 2009 L'Aquila, Italy, earthquake, people saw four-inch (ten-centimeter) flames of light flickering above a stone street.

On November 12, 1988, people reported a bright purple-pink globe of light along the St. Lawrence River in Quebec, 11 days before a powerful quake.

People also reported seeing a faint rainbow of light before the great 1906 quake in San Francisco and lights before the devastating 1811-12 New Madrid earthquakes in Missouri.

Freund and colleagues studied such historic accounts going all the way back to the year 1600 and published their findings in Seismological Research Letters.
Source: Bizarre Earthquake Lights Finally Explained

c.c Daudi Mchambuzi ; figganigga ; rubii ; Rweye ; Tangawizi ;
 
Back
Top Bottom