figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,491
- 54,884
Wakazi wa Ibila Kagera wakimbia nyumba zao kuhofia kuungua moto ambao chanzo chake hakijulikani.
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Ibila kilichoko katika kata ya Mayodwe iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera wameanza kuzikimbia nyumba zao za makazi kwa hofu, kufutia matukio ya mara kwa mara ya baadhi ya nyumba za wananchi katika kitongoji hicho kuendelea kuteketea na moto unaozuka ghafla majira ya mchana ambao hadi sasa chanzo chake hakujajulikana.
Moto huo unaoteketeza nyumba za makazi ulitokea kwa mara ya kwanza katika kitongoji hicho Mei 4, mwaka huu na hadi sasa umeishateketeza nyumba 12 za makazi ya wananchi ambao wanaishi katika mazingira magumu, wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeteketea na wale waliokimbia nyumba zao kutokana na hofu ya moto, wameyahusisha matukio hayo na masuala ya imani za kishirikina huku mmoja akieleze namna alivyoinusuru nyumba yake ambayo ilikuwa imeanza kuteketea usiku wa kuamkia.
Kufuatia matukio hayo ya moto mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango ambaye amekutana na viongozi wa madhehebu ya dini, waganga wa tiba za asili na wazee wa kilmila na kuzitembelea familia zilizoathirika na moto huo pamoja na kutoa maelekezo ya kukabiliana na moto huo amesikitishwa mtu mmoja ambaye baada ya nyumba yake kuanza kuteteketea kwa moto alifanya kazi ya kumnusurui mtoto wake aliyekuwa akiugulia ndani ya nyumba hiyo ambaye baadae alipata mshtuko na kufariki dunia.
Chanzo: ITV