JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,458
WATU wanane waliokufa kwenye ajali ya gari wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakiwemo watano wa familia moja wamezikwa katika Kijiji cha Nyamalagala, Kata ya Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Diwani wa Kata ya Lusahunga, Amos Madebwa alisema kijiji hicho kimepata simanzi kwa kupoteza watu wanane akiwemo mama na wanawe wanne.
Madebwa alisema taarifa alizozipata kwa majirani na marafiki wa karibu wa familia ni kuwa mama huyo, Jesca Leonard (45) alitoroka usiku na wanawe ili kumkimbia mumewe mwenye miaka 80 kutokana na masuala ya kifamilia.
Alisema Jesca hakuacha mtoto nyumbani kwa kuwa mwaka jana alifiwa na mtoto akabaki na watoto wanne ambao amekufa nao kwenye ajali.
"Majirani wanasema mama aliwakimbiza watoto kwenda Ngara ili kuepukana na ugomvi na mumewe ambaye kwa sasa ana miaka 80,” alisema.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, William Mwampaghale alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea Julai 11 saa moja usiku, eneo la Busiri, barabara kuu ya kutoka Lusahunga kwenda Kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo.
Waliokufa ni Nyawenda Bihela (35), dereva na mmiliki wa gari dogo, Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32) ambao walikuwa wasindikizaji.
Watoto waliokufa na mama yao wakienda Benaco wilayani Ngara ni Margaret Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6) na Vestina Sekanabo (4).
Chanzo: Habari Leo
Pia soma: Kagera: Ajali yaua watu nane wakiwemo watano wa familia moja Julai 12, 2022