Kagera: Magunia 515 ya kahawa yaliyokuwa yakisafirishwa kimagendo kwenye Uganda yakamatwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limekamata magendo ya kahawa katika kata ya Kemondo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera

Hayo yamebainishwa na mkuu wa kituo cha polisi Bukoba mkoani Kagera SSP Babusanare wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kwamba mnamo tarehe 24 Septemba mwaka huu askari waliokuwa doria walipata taharifa kuwa gari lenye usajili NO.T.205 DHX Mitsubishi Fuso lilikamatwa kwa kosa la kusafirisha kahawa bila kibali.

Ameongeza kuwa magendo hayo yalikamatwa katika maeneo ya Bulila, Kata Kemondo, Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ambapo yalikuwa yanapitia Mwalo wa Bilolo kemondo kuelekea nchini Uganda.

Bwana Babusanare amesema kuwa gari hilo lilikuwa na kahawa gunia 515 na kila gunia lina kilo 70 na kuongeza kuwa dereva wa gari iyo alitokomea kusiko julikana baada ya kuona anakamatwa na polisi na kuongeza kwamba jitihada za kumtafuta dereva huyo bado zinaendelea na kusema kwamba watuhumiwa wote wamekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi wilaya ya Bukoba kwa mahojianio zaidi.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na Sadick Charles, Jonizius Gerad na Lazaro Mdesa.

Kwa upande wake Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba DC Deodatus Kinawilo amepongeza juhudi za jeshi la polisi kukamata gari hilo na kuhakikisha kila aliyehusika katika kusafirishwa kwa magendo hayo ya kahawa sheria inafuata mkondo wake na kuwawajibisha ipasavyo.

“Dolia hii iwe endelevu hasa katika maeneo mnayoyadhania yanaweza kuwa na makosa ili kutetea juhudi za Rais wetu Mh.Dk.John Pombe Magufuli kutokana na makosa yanayojitokeza katika kahawa maana watu kama hawa wanarudisha maendeleo nyuma hawatakiwi kuachwa kabisa” Alisema Kinawilo.
 
Hii ndo hasara ya kuwa mkulima nchi hii. Hawajaliwi kabisa.

Bei ya kahawa Uganda ni nzuri na wanapata pesa yao bila ubabaishaji. Serikali ya Tanzania imekataza kuuza nje mazao na huku ndani bei ni za maumivu.

Hizo juhudi za Magufuli zingekuwa zinawanufaisha wakulima wasingeuza kwa magendo maana Uganda nao wanauza nje kama sisi.
 
Wawaruhusu wauze nje tu maana bei za ndani hazieleweki kabisa ni ndogo na ubabaishaji ni mkubwa.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limekamata magendo ya kahawa katika kata ya Kemondo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera

Hayo yamebainishwa na mkuu wa kituo cha polisi Bukoba mkoani Kagera SSP Babusanare wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kwamba mnamo tarehe 24 Septemba mwaka huu askari waliokuwa doria walipata taharifa kuwa gari lenye usajili NO.T.205 DHX Mitsubishi Fuso lilikamatwa kwa kosa la kusafirisha kahawa bila kibali.

Ameongeza kuwa magendo hayo yalikamatwa katika maeneo ya Bulila, Kata Kemondo, Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ambapo yalikuwa yanapitia Mwalo wa Bilolo kemondo kuelekea nchini Uganda.

Bwana Babusanare amesema kuwa gari hilo lilikuwa na kahawa gunia 515 na kila gunia lina kilo 70 na kuongeza kuwa dereva wa gari iyo alitokomea kusiko julikana baada ya kuona anakamatwa na polisi na kuongeza kwamba jitihada za kumtafuta dereva huyo bado zinaendelea na kusema kwamba watuhumiwa wote wamekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi wilaya ya Bukoba kwa mahojianio zaidi.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na Sadick Charles, Jonizius Gerad na Lazaro Mdesa.

Kwa upande wake Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba DC Deodatus Kinawilo amepongeza juhudi za jeshi la polisi kukamata gari hilo na kuhakikisha kila aliyehusika katika kusafirishwa kwa magendo hayo ya kahawa sheria inafuata mkondo wake na kuwawajibisha ipasavyo.

“Dolia hii iwe endelevu hasa katika maeneo mnayoyadhania yanaweza kuwa na makosa ili kutetea juhudi za Rais wetu Mh.Dk.John Pombe Magufuli kutokana na makosa yanayojitokeza katika kahawa maana watu kama hawa wanarudisha maendeleo nyuma hawatakiwi kuachwa kabisa” Alisema Kinawilo.
GUNIA 515 mara KILO 70 = KILO 36,050 = TANI 36.05
JE MITSUBISHI FUSO INA UWEZO WA KUBEBA MZIGO HUO KWA MKUPUO?
 
Bei ya kahawa Uganda ni nzuri na wanapata pesa yao bila ubabaishaji

hapo nakubaliana nawe tatizo ni kuwa wakulima wengine hukopa pesa ili warudishe baada ya kuuza kahawa kinachotokea baadhi huona kulipa deni ni mzigo baro abahatishe kutorosha kwani garama za kusafirisha kwa magendo hadi uganda ukibahatisha na ukiuza tofauti inakua ni kidogo sana au ikalingana na ulikotoka...
 
Ukibahatisha kuuza kahawa yako Uganda unakuwa tajiri haraka Sana maana bei Yao iko juu kuliko bongo.ndo maana Kagera bado wanagangania kulima kahawa.

Kilimanjaro naona wengi wanaachana na hio biashara
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom