Kagera: Ifahamu familia inayoamini kumiliki Simu, TV na kwenda Shule ni dhambi

Kuna mgombea wa uraisi alikua anaitwa Maganja atakua kaka wa mama mchungaji mtu anaitwa Maganja unategemea nn?
 
Familia ya Merchades Buberwa, mkazi wa Kasarani, Bukoba mkoani Kagera, imeeleza haina mpango wa kuwapeleka shule, lakini pia watu wa familia hiyo hawamiliki simu, hawaangalii televisheni na hawashiriki shughuli zozote za kijamii wakidai kuwa Mungu wao anakataza na kufanya hivyo ni dhambi.

Hayo yote yanajiri baada ya Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro, kumwagiza afisa elimu ya msingi wa manispaa hiyo, kuwakamata na kuwapeleka shuleni kwa nguvu, watoto watatu wa familia hiyo ya anayejiita mchungaji aliyekataa kuwapeleka watoto wake shule kwa madai ya kuwa kufanya hivyo ni dhambi maana maandiko ya Mungu hayaruhusu watoto kwenda shule.

Familia hiyo inao watoto watano na wote hawasomi na mkubwa kati yao ni wa kike mwenye umri wa miaka 13, mbali na kutokwenda shule, wakiwa wadogo hawajawahi kupelekwa kliniki na pia wakiumwa hawapelekwi hospitali, ambapo mkuu huyo wa wilaya amesema baba huyo akiendelea kushikilia msimamo wake wa kuzuia watoto kwenda shule atakamatwa na kushtakiwa.

Baba wa watoto hao Merchades Buberwa ambaya amesema ni mchungaji wa kanisa la wakristo washikao amri za Mungu, ambalo makao yake makuu yako mbinguni, amesema hayuko tayari kuruhusu watoto wake kutenda dhambi kwa kwenda shule, huku mkewe Agripina Maganja, akimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa Mungu atasimama kuwatetea.


Hebu fikiria nchi ina watu milioni 72 wenye imani za namna hiyo , nchi itatawalika kweli? Hilo ndilo tatizo alilokuwa nalo president Biden wa Marekani na hao wanaoitwa White supremacists[ Q non] wanaoamini kuwa Trump ndiye bado Rais wa Marekani na kwamba Uchaguzi tao ulikuwa wa magumashi!!!! Kazi anayo!!
 
Anasimamia mstari upi kutoka kwenye Bible unaosema watoto wasipelekwe shule?
Kumbe kuna baadhi ya Wahaya wako kwenye stone age
Mkuu ulikuwa unatuonaje Wahaya, type zote za watu zipo kabila kubwa hili. Sio kila mhaya ni Ruge au Rugemalira.
 
Duniani watu wameshaharibikiwa akili bila wao kujua ...
Huyo mwenye hiyo familia yupo sahihi ..
 
Huezi amini licha ya ukanjanja huu,wapo watu watakwenda kujiunga kwa mchungaji huyu wawe washirika wake,dunia haiiishi maajabu.
Kama Nabii Tito alikuwa na waumini anajaza kanisa sembuse huyu
 
Ikiwa kanisa husika wanakatazana kusoma(akiwemo na Mchungaji), mistari ya biblia wameijuaje bila ya kusoma? Yaani, wakubwa walijuaje kusoma hata wakajua kusoma biblia na kuiona mistari inayokataza kusoma?
 
Back
Top Bottom