Kagera haki ya kupata msaada wa sheria kwa mtu wa kawaida imeminywa.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Hapa Mkoani Kagera huduma ya msaada wa sheria kwa watu wasio na uwezo haipo. Katika hali hiyo tegemeo la mtu wa kawaida hasiyekuwa na uwezo wa kuajiri wakili msomi na mwenye leseni ilikuwa ni kutumia watu wenye ujuzi wa sheria kwa kuwapa viapo vya uwakilishi. Utaratibu huo ni halali chini ya sheria na ni haki ya msingi kikatiba. Kwa bahati mbaya, hivi majuzi siku ya Ijumaa tarehe 26/11/2010, Mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Bukoba imepiga marufuku utaratibu huo kwa shinikizo la mawakili wenye leseni ambao wanahisi kuwepo kwa watu hao kunawapunguzia biashara. Jambo la kusikitisha ni kwamba uamuzi huo ulifikiwa bila ya wahusika wanao wakilishwa kupewa fursa ya kusikilizwa. Matokeo yake ni kwamba hivi sasa hawajui hatma ya kesi zao zilizokuwa zinaendelea kwa msaada wa hao waliopigwa marufuku.
 
Mbunge wako yuko wap? yaani kwa jinsi huo mkoa ulivyo na wanasheria wengi inakuaje hauna wanasheria wenye utaratibu wa bure?
 
Hapa Mkoani Kagera huduma ya msaada wa sheria kwa watu wasio na uwezo haipo. Katika hali hiyo tegemeo la mtu wa kawaida hasiyekuwa na uwezo wa kuajiri wakili msomi na mwenye leseni ilikuwa ni kutumia watu wenye ujuzi wa sheria kwa kuwapa viapo vya uwakilishi. Utaratibu huo ni halali chini ya sheria na ni haki ya msingi kikatiba. Kwa bahati mbaya, hivi majuzi siku ya Ijumaa tarehe 26/11/2010, Mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Bukoba imepiga marufuku utaratibu huo kwa shinikizo la mawakili wenye leseni ambao wanahisi kuwepo kwa watu hao kunawapunguzia biashara. Jambo la kusikitisha ni kwamba uamuzi huo ulifikiwa bila ya wahusika wanao wakilishwa kupewa fursa ya kusikilizwa. Matokeo yake ni kwamba hivi sasa hawajui hatma ya kesi zao zilizokuwa zinaendelea kwa msaada wa hao waliopigwa marufuku.

Hili jambo na mimi nimelisikia kwa kutumiwa SMS na mtu ambaye simu yake haipatikani

Nitafuatilia jambo hili siku si nyingi nitakuwa na la kusema kupitia media

Inawezekana kuna issue ya kibishara au vinginevyo.TUSUBIRI KIDOGO

Byabato
 
Back
Top Bottom