Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Hapa Mkoani Kagera huduma ya msaada wa sheria kwa watu wasio na uwezo haipo. Katika hali hiyo tegemeo la mtu wa kawaida hasiyekuwa na uwezo wa kuajiri wakili msomi na mwenye leseni ilikuwa ni kutumia watu wenye ujuzi wa sheria kwa kuwapa viapo vya uwakilishi. Utaratibu huo ni halali chini ya sheria na ni haki ya msingi kikatiba. Kwa bahati mbaya, hivi majuzi siku ya Ijumaa tarehe 26/11/2010, Mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Bukoba imepiga marufuku utaratibu huo kwa shinikizo la mawakili wenye leseni ambao wanahisi kuwepo kwa watu hao kunawapunguzia biashara. Jambo la kusikitisha ni kwamba uamuzi huo ulifikiwa bila ya wahusika wanao wakilishwa kupewa fursa ya kusikilizwa. Matokeo yake ni kwamba hivi sasa hawajui hatma ya kesi zao zilizokuwa zinaendelea kwa msaada wa hao waliopigwa marufuku.